Serikali ya CCM haya ndo maisha bora kwa mshahara wa 180, 000/= nyie mnalipana ngapi Bungeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya CCM haya ndo maisha bora kwa mshahara wa 180, 000/= nyie mnalipana ngapi Bungeni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 9, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Source mwananchi

  NI BAADA YA MAJADILIANO YA SERIKALI NA TUCTA
  Waandishi Wetu
  KUNA taarifa kwamba Serikali imekubali kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa kati ya asilimia 20 na 33.3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13.Hatua hiyo inamaanisha kwamba kima cha chini cha mshahara sasa kitakuwa kati ya Sh180,000 hadi Sh200,000 kutoka Sh150,000 zinazolipwa sasa.Vyanzo vya habari kutoka serikalini vimeeleza kwamba nyongeza hiyo ya kati ya Sh30,000 hadi Sh50,000 ni matokeo ya mazungumzo kati ya Serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta).Mbali ya kutaja kima hicho, vyanzo hivyo vimeeleza kuwa nyongeza hiyo inaweza kuvuka Sh50,000 kutegemea uwezo wa Serikali.

  Hata hivyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), George Yambesi alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo alijibu kwa kifupi kuwa hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia hilo.

  “Sipo katika ‘position’ (nafasi) nzuri ya kuzungumzia hilo, nadhani suala la mishahara. Mheshimiwa Rais alishalizungumzia kwenye hotuba yake ya Sikukuu ya Wafanyakazi,” alisema.

  Katika hotuba yake kwenye kilele cha sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali inatambua mazingira magumu ya kazi waliyonayo wafanyakazi na kwamba ipo tayari kuyaboresha.

  Alisema imesikia madai ya wafanyakazi na itaendelea kuyafanyia kazi. Madai aliyoahidi kuyafanyia kazi ni pamoja na kupunguziwa kodi ya mapato.

  Kwa upande wa Tucta, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicolaus Mgaya alipoulizwa jana alisema hajui Serikali itaongeza mshahara kwa kiasi gani lakini akasema anaamini kuwa ni sikivu.

  Alisema kwa miaka mingi wafanyakazi wamekuwa wakilalamikia mishahara midogo ambayo haikidhi mahitaji, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa migongano ya hapa na pale na Serikali akasema kutokana na hali hiyo, wanaamini kuwa wataongezewa.

  “Tunaamini linaweza kutekelezeka (suala la kuongezewa mishahara), lakini hakuna anayejua nyongeza hiyo itakuwa ni kiasi gani, kwa hiyo ukinitajia kiwango nashindwa kuelewa umekitoa wapi,” alisema Mgaya alipoulizwa kama nyongeza hiyo ni kati ya Sh30,000 na 50,000.

  Mgaya alisema mbali na kuomba nyongeza mshahara, Tucta pia imeiomba Serikali kupunguza gharama za tozo za mifuko ya hifadhi ya jamii huku ikienda pamoja na udhibiti wa mfumuko wa bei ambao umekuwa kikwazo kwa wafanyakazi na kuwafanya kuishi katika mazingira magumu kiasi cha kushindwa kujituma ipasavyo na wengine kukimbilia kwenye sekta binafsi.

  “Wafanyakazi ni tabaka kubwa, lakini limesahaulika. Hii inatokana na Serikali kushindwa kusikiliza kilio chao cha kuwaongezea mishahara jambo ambalo limechangia kulipwa ujira mdogo na kusababisha wengi wao kukimbilia kwenye sekta binafsi, kutokana na hali hiyo tunaamini kuwa Serikali itasikilia kilio chetu,” alisema.

  Madai ya wafanyakazi

  Sakata la mshahara wa wafanyakazi liliibua mgogoro mkubwa baina ya Serikali na Tucta na mwaka 2010, Shirikisho hilo liligoma kumwalika Rais Kikwete kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa kama ilivyokuwa utamaduni wake.

  Hatua hiyo ya Tucta ilitokana na kile lilichodai kuwa Serikali siyo sikivu na lilitumia siku hiyo kujadili na kutoa tamko la kuitaka kutangaza kima kipya cha mshahara cha Sh315,000 ndani ya siku mbili la sivyo wafanyakazi wa umma wangeingia katika mgomo nchi nzima.

  Hatua hiyo ilimlazimu Rais Kikwete kuitisha mkutano na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mei 3, 2010 na kujibu hoja mbalimbali za Tucta na kuweka msimamo wa Serikali kuwa haiwezi kulipa kiasi hicho cha fedha.

  Rais Kikwete aliwatuhumu viongozi wa Tucta kuwa ni waongo na kwamba walikuwa hawasemi ukweli juu ya kile walichokuwa wanabaliana katika vikao vyake na Serikali.

  Alisema Serikali ikifanya kima cha chini kuwa Sh300,000 kwa watumishi wa umma, itabidi iwalipe Sh6.9 trilioni kwa mwaka wakati makadirio ya makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2010/11 ni Sh5.8 trilioni.
   
 2. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Nicholous Mugaya bado yuko ngangari? au Magamba yalishamteka. Kwani siku hizi haonekani tena kupambana kama zamani. hata Madaktari walipokuwa wanadai haki zao aliwakana!
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Keshapewa chake huyo haiwezekani mchele wenyewe 3,000/= unga 1,400/= tunaenda wapi jamani bado umeme na maji duuuuuuh
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Watanzania tumekuwa watabiri sana badala kujikita katika shguli za maendeleo matokeo yake tunabaki kulalama. Tulisema Rais kashindwa kushughuliia mgomo wa Madaktari, akamumaliza tena kimya bila manung'uniko. Tukasema Rais kashindwa kuwashughulikia Mawziri wanaotuhumiwa, katunyamazisha na hatuna la kusema tena. Tumeanza tena hili za nyongeza ya mishahara kabla hata bajeti haijasomwa bungeni. Tufanye kazi jamani, haya maneno ya kulambishwa midomoni ya kuwaza kuongea mambo ambayo hayajengi ni kudhoofisha juhudi za Serikali za kupambana na hali ngumu ya maisha ya wananchi wake.
   
 5. n

  ng'wabuki Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyongeza ya nini mheshimiwa rais wakati ule mshahara wa mpya wa mwaka jana bado tunadai na hatujalipwa ule wa mwezi wa julai na agosti? Au ndo mmeamua kuwastua wafanyabiashara wapandishe bei ya vitu vyao kuwakomoa wanaodai nyongeza ya mshahara kila mwaka?

  Mheshimiwa rais utambue kuna watu hata wakiwa promoted na taasisi zao wanakaa zaidi ya mwaka hawajawahi kulipwa pesa hiyo wanaambiwa tu kuwa kwakuwa mlishajaza salary arrears claims form mtalipwa tu wakati wowote hadi leo zaidi ya mwaka na nusu tangu wawe promoted. Sasa mishahara mipya ya nini wakati hata hatulipwi kwa wakati pesa yenyewe?
   
 6. n

  ng'wabuki Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyongeza ya nini mheshimiwa rais wakati ule mshahara wa mpya wa mwaka jana bado tunadai na hatujalipwa ule wa mwezi wa julai na agosti? Au ndo mmeamua kuwastua wafanyabiashara wapandishe bei ya vitu vyao kuwakomoa wanaodai nyongeza ya mshahara kila mwaka?

  Mheshimiwa rais utambue kuna watu hata wakiwa promoted na taasisi zao wanakaa zaidi ya mwaka hawajawahi kulipwa pesa hiyo wanaambiwa tu kuwa kwakuwa mlishajaza salary arrears claims form mtalipwa tu wakati wowote hadi leo zaidi ya mwaka na nusu tangu wawe promoted. Sasa mishahara mipya ya nini wakati hata hatulipwi kwa wakati pesa yenyewe?
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hii ndioari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi......
  Karibuni mang'ula tulime mpunga.....

  Mgaya na wenzie washawezeshwa hawana time.....
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hili la mshahara itakuwa ni kuwahadaa wafanyakazi kwa kipindi hiki tujaribu kuangalia hali ya maisha ilivyo tatizo siokupandisha mishaharabali ni ugumu wa maisha unasababishwa na mfumko wa bei. naomba kwanza waanze na mfumko wa bei ndio waje malizie na ongezeko la mishahara
   
 9. o

  oakwilini Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba mwanaasha mil 20,000,000 walalahoi 180,000.Hili halikubaliki wasubiri tutacheza nao kwenye sanduku la kura 2015.INANIUMA SANA Ndg zangu watz.
   
 10. Bebrn

  Bebrn Senior Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  plus sukari,mafuta kweli inchi imeuzwa
   
Loading...