Serikali ya CCM haina pesa ya Uchaguzi ndio maana wanalilia mkopo wa WB. Miradi imekausha Hazina, wanawaza Uchaguzi na fedha ya nyongeza ya mishahara

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Naomba nieleweke na atakayetaka kuamini sio jukumu langu ni lake kutafakari na kuona facts.

Rais Magufuli alidanganya umma kuwa tunajenga kwa fedha za ndani ukweli ni kwamba tumekopa sana kwa ajili ya miradi mikubwa mingi isiyo katika bajeti wala uwezo wetu wa kuijenga kwa pupa kiasi hicho kwa mifano ifuatayo;
1. SGR inayogharimu tril 7
2. Stieglers gorge inayogharimu tril 6.7
3. Ununuzi wa ndege unaogharimu tril 1.9
4. Ununuzi wa ndege binafsi za rais unagharimu bil 500
5. Unenji wa madaraja unagharimu zaidi ya tril 1

Tukumbuke tuna deni la taifa linazidi tril 55 ambalo kila mwaka lazima lilipwe riba na rejesho huku kodi na mapato kwa nchi ukiweka na matumizi huwa tunabaki na nakisi (madeni)

Na kwa ufupi mapato na matumizi havilingani kwa nchi yetu. Sisi ni matajiri ila utajiri wetu wa mdomoni. Kwa vitendo zero kabisa ni umangungo tupu.

Kikubwa zaidi mapato na.mikopo yetu tunayoiweka kwenye miradi karibia 80% ya matumizi yake yanaenda nje ya nchi kwa sababu wakandarasi wote ni raia wa nje, hapa bongo fedha haikai, kuanzia ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli hata ujenzi wa Stiegler fedha zinaenda nje.

Na kinachoangaliwa na serikali hii kwa mwaka huu ni kuongeza mishahara na uchaguzi fedha hazipo ndio maana wanatoa jicho wakope kokote ili waondokane na aibu ya kujiita matajiri na sio kingine.

Awamu hii sio kwa hali hii ya kulilia mikopo inayojimwambafai kukusanya kuliko awamu zilizopita.
 
Tanzania yetu ina wachumi kila sehemu!

Huyu mleta mada naye ni mchumi mwenye uwezo wa kudadavua masuala ya kiuchumi na kufikia hitimisho kuwa serikali haina pesa za Uchaguzi Mkuu!

Huyu mleta Mada inawezekana ni University graduate lakini ukichunguza kupitia mada yake utagundua ujinga wake niwa kiwango cha elimu ya sekondari (O-level) na sio A-level!
 
Ngoja nione jiwe litakavo pasuka!!!Mi nadhani jpm keshafanya kampeni kwa ziara zake mikoani kwa miaka minne!!Shida ipo kwa wabunge!je wabunge wa ccm wanaweza fanya kampeni bila msaada wa jiwe?Hofu nyingine kwa jpm ni wapinzani maana wanaweze kumfuta kabisa jiwe kwenye mind za watanzania kwa kuanika utekaji,ufisadi wa fedha na n.k!!Hapo ndio kazi inakuwa ngumu kwa CCM!!
 
Tanzania yetu ina wachumi kila sehemu!

Huyu mleta mada naye ni mchumi mwenye uwezo wa kudadavua masuala ya kiuchumi na kufikia hitimisho kuwa serikali haina pesa za Uchaguzi Mkuu!

Huyu mleta Mada inawezekana ni University graduate lakini ukichunguza kupitia mada yake utagundua ujinga wake niwa kiwango cha elimu ya sekondari (O-level) na sio A-level!
Ungejibu hoja yake, pengine watu wengine wangepata shida ya kutambua ni nani mjinga kati ya wewe na mleta hoja. Lakini kwa namna ulivyomjibu mleta hoja, umewarahisishia watu kuujua ujinga wa kwako kuliko wa mleta hoha.
 
Hata mimi nilitaka wajue hivyo hivyo unavyosema!

Siwezi kujibu hoja ya mtu ambaye hajui kiwango cha ujinga wake!
 
Kawaida ya mjinga kutoa mipasho, ungekuwa na akili ungejibu hoja, kwa sababu hakuna mradi mkubwa unafanywa na wazawa na materials tunaagiza nje. Hela za ndani zinaenda nje, hapa bongo mmeuza nn kama koroshow zipo gharani
 
Mleta mada anaweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani. CCM hawajawahi kosa pesa ya kupigia kampeni, wakiamua miezi 2 tu hiyo kazi wakawapa traffic police pesa itapatikana ya kutosha. Kinacho wasumbua ni pesa ya nyongeza ya mishahara ambayo ni continuously, kama kweli Jamaa kaamua kuongeza mishahara.
 
Naomba nieleweke na atakayetaka kuamini sio jukumu langu ni lake kutafakari na kuona facts.

Rais Magufuli alidanganya umma kuwa tunajenga kwa fedha za ndani ukweli ni kwamba tumekopa sana kwa ajili ya miradi mikubwa mingi isiyo katika bajeti wala uwezo wetu wa kuijenga kwa pupa kiasi hicho kwa mifano ifuatayo;
1. SGR inayogharimu tril 7
2. Stieglers gorge inayogharimu tril 6.7
3. Ununuzi wa ndege unaogharimu tril 1.9
4. Ununuzi wa ndege binafsi za rais unagharimu bil 500
5. Unenji wa madaraja unagharimu zaidi ya tril 1

Tukumbuke tuna deni la taifa linazidi tril 55 ambalo kila mwaka lazima lilipwe riba na rejesho huku kodi na mapato kwa nchi ukiweka na matumizi huwa tunabaki na nakisi (madeni)

Na kwa ufupi mapato na matumizi havilingani kwa nchi yetu. Sisi ni matajiri ila utajiri wetu wa mdomoni. Kwa vitendo zero kabisa ni umangungo tupu.

Kikubwa zaidi mapato na.mikopo yetu tunayoiweka kwenye miradi karibia 80% ya matumizi yake yanaenda nje ya nchi kwa sababu wakandarasi wote ni raia wa nje, hapa bongo fedha haikai, kuanzia ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli hata ujenzi wa Stiegler fedha zinaenda nje.

Na kinachoangaliwa na serikali hii kwa mwaka huu ni kuongeza mishahara na uchaguzi fedha hazipo ndio maana wanatoa jicho wakope kokote ili waondokane na aibu ya kujiita matajiri na sio kingine.

Awamu hii sio kwa hali hii ya kulilia mikopo inayojimwambafai kukusanya kuliko awamu zilizopita.

Mtu yeyote mfuatiliaji wa mambo lazima angeona uwezekano wa serikali hii kuishiwa. Huko nyuma serikali ilikuwa inapewa up to 40% donor support kwa ajili ya recurrent expenditure budget na zaidi ya 70% ya development expenditure budget. Wafadhili wameitwa mabeberu na wakakata misaada sasa mbuzi jike wanahaha.

Kujua kwingi mwisho giza.
 
Ok. Tuamini mchumi mubobezi wa jf kwa post yako kuwa sawa.
Je miradi hiyo uliyotaja hata kama ni kwa mikopo ile value for money ipo haipo?
Je miradi hiyo ina manufaa hata kama sio leo ila kesho au hakuna?
Nani atathirika kama uchaguzi ukiahirishwa kwa kukosa pesa?
Je lini nchi yako haikuwahi kukopa WB ktk awamu zilizopita?
Je deni la 55tril kama ulivyosema limekuwa genereted awamu hii tu au linaongezeka kwa maana limerithiwa?

Salute kwako mkuu kwa bandiko fikirishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom