Serikali ya CCM chanzo cha migogoro kati ya wananchi na wawekezaji

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Kadiri siku zinavyopita ndivyo migogoro ya kati ya wananchi na wawezekezaji inavyozidi kuongezeka. Kwa maoni yangu, chanzo cha matatizo ni serikali ya CCM, ambayo imeshindwa kusimamia vizuri sheria za nchi na hivyo kusababisha wananchi kuendelea kukosa haki zao za msingi. Inapotokea wananchi wameingia mkataba na mwekezaji bila ya wao wenyewe kushirikishwa na kuridhia isipokuwa viongozi wachache wenye uchu wa kujilimbikizia mali kufanya hivyo, hatusikii kama viongozi hao wanawajibishwa ili liwe fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia kama hiyo. Zoezi la kuwahamisha wananchi ili kupisha mwekezaji, ambaye amepewe eneo lao kuliendelea linafanyika kwa ubabe na kuacha machungu mengi kwa wananchi husika, kama vile uhalibifu wa mali na fidia ndogo isiyoendana na hali halisi ya maisha na isiyolipwa kwa wakati.Mwekezaji anapata kibali cha kumiliki ardhi na kuiendeleza kwa urahisi zaidi kuliko mwananchi anayeomba hicho kibali kwa madhumuni yaleyale.Kuendelea kuwaomba wawekezaji kuja kumiliki maeneo mkubwa ya ardhi kwa kisingizio kuwa “hakuna maendeleo bila wawekezaji” na wananchi kuendelea kukosa fursa hiyo kunasababisha wananchi waone wanafanywa wageni ndani ya nchi yao kwa kuendelea kukosa ardhi maana kwao masharti ya kuipata ni magumu na hata wakiipata wanaweza wakashindwa kuiendeleza kwa muda uliopangwa kwa vile bado wanakusanya nguvu kutokana na kipato kuwa kidogo. Lakini mwekezaji mwenye mtaji mkubwa yeye hili siyo tatizo hata kidogo kwa maana yeye alishajiandaa muda mrefu.Wananchi wengi wanapata ajira zisizo endelevu kwa maana kwamba ni ajira zenye kipato kidogo na zinawafanya waishi “at or below the subsistence level”. Kwa hali ya namna hii, ni dhambi kujivunia kuwa wananchi wameajiriwa kwa sababu mtu anayeishi “at or below the subsistence level” hawezi kufanya “savings” za aina yoyote zitakazoweza kumsaidia kuwa na miradi ya kujiendeleza na kuindeleza familia yake.Kwa hali kama hii, ni wazi wananchi wataendelea kuona wawekezaji si watu wa kuwaletea maendeleo bali wa kuwaongezea dhiki katika maisha yao. Ili kuondokana na hali hii serikali ya CCM isiwaaminishe tu wananchi kuwa “wawekezaji watawaletea maendeleo” bali pia isimamie sheria za nchi vizuri na iweke mazingira ambayo yanawanufaisha wananchi na wawekezaji na siyo kudhani tu kuwa wawekezaji ndio watakaoleta maendeleo ya wananchi maana hata wao wamekuja kuchuma kwa ajili ya mahitaji yao na ya familia zao.
 
JK katoa mpia juzi kuwa Tanzania kamwe haiwezi kuendelea bila wawekezaji! Tunatakiwa tukumbuke Baba wa Taifa letu alivyokuwa anatukumbusha mara mara kuwa raslimali zetu heri zibaki ardhini mpaka watoto wetu watakapokuwa na uwezo wa kuvuna wenyewe. Alijuwa fika ukiwaruhusu hao wanaoitwa wawekezaji wananchi hawataambulia lolote bali ni kuendelea kuwa masikni tu wakati raslimali zao zinapayushwa juu kwa juu. MAONO YAKE ndiyo yanajidhihirisha sasa. Wananchi kunyanyaswa ndani ya nchi yeo na hao waitwao wawekezaji!
Hii serikali hakuna namna inaweza kubadilika na kuwatetea wananchi wake at the expense ya wawekezaji. HAIWEZKANI. Angalia kinachotokea huko kusini mwa nchi kuliko na madini ya uranium. The so called mwekezaji kapewa kibali cha explore kama uranium ipo cha miaka mitano akigundua ndiyo waingie mkataba wa uchimbaji! Tunajua fika uranium ipo lakini hiki kinafanyika. Wamejenga kiwanja cha ndege na madege makubwa kutoka nje kila siku yanachukua mizigo yanaondoka na baada miaka mitano uranium imekwishazolewa yote. Mfano mwingine mwekezaji kwenye sukari aliyegundua eneo lake la mashamba ya miwa lina dhahabu amejenga uwanja wa ndege na anachimba kwa kwenda mbele na kupayusha na pipa!
Hiyo ni mifano michache kati ya mingi inayouma sana na viongozi wetu wanajua fika kinachoendelea as they are part of the conspiracy to loot our resources. Hapo unategemea huu uongozi uwaonee wananci huruma mbele ya wawekezaji? No way! The way out is to take immediate action of correcting this situation as it is within our capability! Otherwise tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe. CCM must go in order save ourselves. No wonder Gadaffi alipouawa wamepiga kelele sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom