Serikali ya awamu ya tano na mfano wa Mtihani wa NECTA

Haya Ni maneno tu ya kawaida Kama stori nyingine tu. Ila ukweli Ni kuwa JPM KIboko ya mafisadi,KIboko ya waiza wa rasilimali zetu, KIboko ya wauza unga,KIboko ya waliohodhi ardhi
Nyie ni mashine za kusifia..mmewekwa kwa kazi hiyo....wala hamtubabaishi

Hivi ile mahakama ya Mafisadi imeshamtia hatiani nani ..?? Ipo wapi...??

Hii mahakama kama itakuwa ya Kudumu basi inaweza mrudi mtu huko mbeleni.....Upotevu wa 2.4 Trillio.,Manunuzi ya hovyo yasiyo fuata utaratibu..

Naona kabisa shimo alilochimba kuwazika wengine ndio litakuja kumzika yeye.....Nakuombea uhai ili ushuhudie
 
Haya Ni maneno tu ya kawaida Kama stori nyingine tu. Ila ukweli Ni kuwa JPM KIboko ya mafisadi,KIboko ya waiza wa rasilimali zetu, KIboko ya wauza unga,KIboko ya waliohodhi ardhi
Hapo umepatia sana. JPM asilimia tisini na tisa (99%) anawaza kuzuia na asilimia moja (1%) kuendeleza hasa linapokuja swala na maendeleo ya watu.

Nikupe mifano michache: -.
Anawaza kufukuza wafanyakazi kuliko kuajiri;

anawaza kukusanya mapato kuliko kukuza uchumi;

kwenye kupata habari na kutoa maoni anawaza kufungia na kuzuia kuliko kupokea;

Kutafuta fursa, anawaza kuzuia akiamini kuwa kila fursa ni dili;

Mishahara, anawaza kuizuia isipande au kuipunguza akiamini kuwa watu wanafaidika sana na hiyo mishahara.

Korosho, mpaka anawatangazia wanajeshi kuwa hataki wafanyabiashara wajihusishe kabisa wasije wakapata hata senti tano.

Yaani huyu mtu wenu ni kiboko. Akiendelea kuchekewa na kusifiwa ataua kila sekta. Ajaye ataanza upya kufufua nchi iliyokufa.
 
mh umesahau . ukaguzi vyet ek kabla ya kumaliza ikabainika miongoni mwao hawana vyeti wakabadili utaratibu wao wakatunga utaratibu waoeti rais wa Dar yeye anatakiwa ajue kusoma na kuandika tuuu? pia kulikuwa na ukame na jaa ikaibuka katika swali hilo ikajikuja kukokotoa jibu likagoma ili kutoacha swali bila kujibu eti ikawa serikali haina shamba? hapo ikapata maks 0%
 
Najaribu kujiweka katika nafasi ya huyo mwanafunzi nimeshindwa kumaliza uzi mkuu yaani hapa natetemeka mwili mzima
 
Wacha longolongo wewe msifia chochote, walipeni kwanza wakulima wa korosho korosho zao

Hiyo ya mwaka 2020 Jijazieni hiyo mikura yenu hata kama mpate100%, lakini haiondoi ukweli kuwa nchi imewashinda!, mmechemsha!. Uhalali wenu ni Polisi, Tume na Usalama wa Taifa tu lakini hamna legitimacy mbele ya umma kama uchaguzi unakuwa wa huru na haki!


Hahahaaaa, kuna hii comment nimeiona huko previous page

Nanukuu "hao ni wazee wa pindua pindua wanaweza pindua samadi ya binadamu kuwa keki na watu wakashangilia"
 
Atleast uzi wa kufungia mwaka umepatikana mapema tu

Hahah, Serikali hii inachoweza ni propaganda na kucheza rafu kwenye haki za watu.
Umebaki mwaka mmoja ufike uchaguzi mkuu.
Vitu tangible vya kutuonyesha kuwa wamefanya ni vichache vichache mno, Ila propaganda zao sasa duh, utadhani bongo kama New york
 
Hahah, Serikali hii inachoweza ni propaganda na kucheza rafu kwenye haki za watu.
Umebaki mwaka mmoja ufike uchaguzi mkuu.
Vitu tangible vya kutuonyesha kuwa wamefanya ni vichache vichache mno, Ila propaganda zao sasa duh, utadhani bongo kama New york
Afu hizi propagandaa zao hawajui zinawachosha watu,yaan kila siku n yale yale,stiglerz,ndege stgr,imekua kama mwalimu anaeifanyia topic moja revision more thanb10 times,wanafunz wataona hakuna tena jipya n michosho tu.....nayo ndo serikali hii inafanya,watu wanataka kuskia kitu kipya ila wao n vile vle tu wanarudia..shame on this gvrnt
 
Serikali ya awamu ya tano inanikumbusha enzi zetu tunajiandaa na NECTA. Kabla ya Necta ukipewa test darasani ukafeli unajipoza kwa kujiambia kuwa hii siyo NECTA, NECTA ikija nitakuwa nshakuwa fiti nitapasua tu.

Mara siku zinakwenda zinasogea mara NECTA hiyo!, Paper ya Kwanza unakuwa makini kwelikweli, unasoma Instructions zote ili usije ukakuta ile Instruction labda imeandikwa "DONT ATTEMPT ANY QUESTION" halafu ukafeli!. Unajiridhisha kuwa hiyo instruction haipo!.

Ghafla unaruhusiwa kufunua pepa ili uanze mtihani,Kitu cha kwanza unagundua lile feki ulilolipata kutoka wajanja wa shule ya Jirani ni famba, unapaniki kidogo lakini ghafla unakutana na kiswali fulanifulani hivi kirahisi Unakitembeza fasta, sasa inakuja Muda kila Swali unalogusa HALITEMBEI!!, Unafunua Section B ndo balaaa, yaani mtu unajiona unataga hivihivi!, Section A pa moto, SECTION B ndiyo balaa

Sasa basi unaanza kugusa swali hili, haligusiki, unahama unagusa swali jingine ndiyo balaa!. Ukiinua Shingo kuwaangalia rafiki zako hakuna wa kukusaidia!. Unaomba kwenda Toileti unasindikizwa na afande, haja ndogo haitoki unarudi kukaa Invijileta kakutolea macho!. Yaani Unajiona hivihivi mzee unazunguusha!.

Sasa kadri siku zinavyosonga, mitihani umeshaizoea, unaanza kuichukulia poa, unafanya bora liende, hauna umakini tena
Mara tahamaki NECTA imeisha, Matokeo yanakuja UMEZUNGUUSHA!

Sasa Serikali hii ya awamu ya Tano haina tofauti na mwanafunzi huyo hapo juu, iliingia kwa mbwembwe huku ikiwa na Feki lake (ILANI), kufika kwenye Chumba cha mtihani (KUONGOZA) ikabahatika kukuta ishu nyepesi za sherehe ya Uhuru, ikaahirisha kusherehekea, Ikakuta ishu nyingine nyepesi ya kujenga hosteli fasta ikatembeza hilo basi Ikaona sasa mambo safi, Itapiga WANI , Thubutu!. Haijakaa sawa ikapigwa swali la Tetemeko Kagera, Ikapigwa swali la Sukari, Ikapigwa swali la nyongeza na stahiki za wafanyakazi, Hapa ikaanza kuchanganyikiwa!, Ikaanza kugusagusa tu maswali na kukosa majibu, mara Mbaazi chali, Mara Makinikia Chali, Mara kukamata Almasi Airport chali, Mara Kikokotowo chali, Mara Korosho Chali, Mikopo, Ajira kwa wananchi chali.

Baada ya Pepa kuwa ngumu ikaaza kujitungia maswali ambayo hata hayamo kwenye NECTA, Imejitungia Swali la Kuhamia Dodoma lakini hata ilivyolijibu imekosa!.

Swali la ndege iliamini imepata, ila naona polepole kumbe imeanza kugundua kuwa badala ya kufanya kuwa ni kipeo (Square), yenyewe imechukua Kipeuo (Square-root), Confidence zimeanza kushuka!

Imeacha maswali ya msingi kwenye pepa kama vile KATIBA MPYA maana hili kwa mujibu wa sheria ya mabadiriko ya Katiba ni Compusory!.

Sasa inafanya swali la SGR na Stieglers, Hebu ngoja tuone ila naona INVIJILETA ameshaanza kuangalia saa yake na kusema "TIME LEFT is one year and few months"

Na kwa jinsi pepa ilivyo ngumu imeanza kufikiria kuchora kwenye answersheet katuni ya "ZOMBI HAJAVAA VIATU!

serikali hii kwa namna inavyoshuka hili pepa, mimi naona ITAZUNGUUSHA TU!!!, It is a matter of time!
Kwa taarifa yako, Dkt Magufuli hajawahi kufeli, na hii NECTA ya uongozi mpaka sasa ana single digit (A zoote), tunawasubiri nyie watabiri fake muumbuke maana watanzania tunamuamini kwa 100% na kila nchi duniani inatamani rais wao awe Dkt Magufuli!
 
Back
Top Bottom