Serikali ya awamu ya tano inatutenda vibaya watumishi wa umma

Nilicheka pale mukulu aliposema ili kuwapunguzia mzigo watumishi nashusha Jodi hadi 9% watu oyoooooo... Usaniii mtupu
 
Kwa hiyo walimu wakigoma wanamkomoa nani? Watawahumiza ndg Zao masikini ambao hawana uwezo Wa kupeleka watoto wao Canada. Sasa hv imeshakuwa tatizo tutulie tufanye kazi hakuna namna, hakuna atakayekuthamini wala kukusikiliza. Tujenge msingi bora Wa taifa litakalojitegemea. Siungi mkono migomo eti ndiyo solutions Za kuinua hali ya watumishi Wa umma.

tutakuwa hatufikiri sawasawa tukikidhani waliosoma Canada hawawahitaji waliosoma shule za hovyohovyo hapa kwetu. Migomo imesaidia sehemu nyingi. Na ni unyonge mkubwa kupunjwa maslahi na ukaendelea kuvumilia kwasababu unazozitaja. Waliosomeshwa na walimu wasomeshe watoto wao Canada na mwalimu huyo huyo ashindwe hata kumpa mahitaji sitahiki mtoto wake aliyeko shule ya kata. Halafu aendelee kuvumilia sababu ya taifa. Huyo anayepeleka mtoto wake Canada hili si taifa lake? Walimu nao ni watu, tuwapende na kuwajali.
 
?
tutakuwa hatufikiri sawasawa tukikidhani waliosoma Canada hawawahitaji waliosoma shule za hovyohovyo hapa kwetu. Migomo imesaidia sehemu nyingi. Na ni unyonge mkubwa kupunjwa maslahi na ukaendelea kuvumilia kwasababu unazozitaja. Waliosomeshwa na walimu wasomeshe watoto wao Canada na mwalimu huyo huyo ashindwe hata kumpa mahitaji sitahiki mtoto wake aliyeko shule ya kata. Halafu aendelee kuvumilia sababu ya taifa. Huyo anayepeleka mtoto wake Canada hili si taifa lake? Walimu nao ni watu, tuwapende na kuwajali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali hii mpya iliyoaminiwa na umma wa Tanzania imetugeuka watumishi wa umma kwa namna isiyoelezeka,rais aliahidi kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kwa nguvu zote lakini mambo yamekuwa tofauti:

i)hakuna nyongeza ya mishahara
ii)hakuna kupandishwa Madaraja
ii)uhamisho umezuiliwa n.k

Napenda kuikumbusha serikali kutosahau kundi hili la watumishi wa umma hasa wa kada za chini,juu ya mchango mkubwa walioutoa na wanaoendelea kuutoa kunyamaza kimya haimanishi hoja hazipo au matatizo yamekwisha

serikali ndio yenye wajibu wa kutekeleza ahadi zake ilizozitoa isikimbie kivuli chake kwa kukwepa wajibu wake kwa kisingizio cha uhakiki tulioaminishwa utaisha baada ya miezi miwili lakini sasa ni mwaka unaenda,

sisi watumishi wa umma wengi wetu tunaweka nguvu na akiri zetu kwenye majukumu haya ya serikali na si vinginevyo hivyo ni vema maslahi yetu yaangaziwe kwa jicho pevu,shime serikali mficha maradhi kifo humuumbua.
Kufanya kazi serikalini awamu hii inatakiwa uwe polisi, jeshini au TISS wengine ombeni msaada kwa mungu hamna tija wala faida
 
Tatizo viongozi wa vyama vya wafanyakazi na vyama vyenyewe ni wanyonyaji wakubwa na wao huongeza maumivu kwa kuwaibia wafanyakazi 2% ya mishahara kila mwezi.MF mtu anayepata 500,000 hukatwa na mavyama haya ya kinyonyaji shs 10,000 kila mwezi ...na fedha hii haijulikani inafanya nini zaidi ya kuongeza ukubwa wa mitumbo ya wanyonyaji wachache !!
Tatizo viongozi wao wenyewe wamekua kimya.Malalamiko ya m1 m1 hayana nguvu ila kama vyama vya wafanyakazi vikiamua kulalamika watasikilizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adui wa mtumishi ni mtumishi mwenzake. Anawaza atajinyenyekeza vipi kwa mtukufu anko apate allowance mwisho, anaishia kutumika kama toilet paper anaanza kulia lia. Sijui alienda shule kufanya nini..ni ujinga ujinga tu.
Mi naamini kama utajitoa katika kazi yako na ukajitoa kwenye shughuri zako binafsi sidhani kama utakuwa na mda wa kutafuta sympathy kwa watu wengine. 🙏🙏🙏
 
Watumishi wa serikali leteni mrejesho wa uvumilivu hapa na mtupe tathmini na msimamo wenu October 2020
 
nasema magufuli,majariwa etal vaeni viatu vyetu,kumbukeni mlikotoka nyie pia mlikuwa watumishi inawauma nini leo kuboresha maslahi ya watumishi,mishahara,uhamisho,madaraja n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom