Serikali ya Awamu ya Sita wekeni taa Uwanja wa Ndege wa Bukoba, msisubiri vifo na majanga

Yusuf Kashaju

Member
Oct 20, 2019
57
89
Chonde Chonde Serikali ya Awamu ya 6 wekeni taa katika uwanja wa ndege wa Bukoba, msisubili vifo na majanga yatokee ndiyo taa hizo ziwekwe. Tatizo hili limekuwa la muda mrefu na sijui tatizo liko wapi, ambapo uwanja wa ndege wa Bukoba ni kati ya viwanja vichache nchini vyenye habiria wengi na hivyo unajiendesha kwa faida. Pesa hiyo inayopatikana inapelekwa wapi mbali ya kutumika kulinda maisha ya abiria na wananchi wa Bukoba!

Mara nyingi nimemsikia Mkurugenzi Mkuu wa ATCL akilalamika kuhusu ndege kushindwa kutua katokana na mawimbi yanayosababisha marubani kutoweza kuona vizuri na kulazimika au kurudi Mwanza au kusubili angani, his ni hatari kubwa sana kwa usalama wa abiria na wananchi wa Bukoba waolioko chini, Serikali ichukue hatua za dharula kumaliza tatizo hilo, tunawaomba na kuwasihi Serikali kuweka taa haraka tena katika bajeti ya mwaka 2021/22.

Wabunge wa Bukoba wanaowajibu wa kushikilia mshahara wa waziri wa ujenzi na uchukuzi wakati bajeti yake itakapoletwa bungeni!

Jana pia nimemsikia Mkurugenzi Mkuu wa ATCL akieleza tatizo hili mbele ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama kawaida sikuona kama lilichukuliwa kwa uzito wake hasa kuzingatia hatari iliyopo kwa maisha ya wananchi wanaotumia uwanja huo

Rais wetu wa Awamu ya 6, Mheshimiwa Samia Suluhu Hasan okoa maisha ya watu hawa kabla ya janga kubwa kutokea.
 
Na ulivyo karibu na makazi ya watu siku ndege ikianguka hapo ni majanga.
 
Back
Top Bottom