Serikali ya awamu ya nne na uhodari wa viporo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Tamko lililotolewa leo na jukwaa la wakristo nchini na reaction ya watanzania limenifanya nikumbuke utitiri wa matukio ambayo umma wa watanzania ulipaza sauti kutaka serikali ichukue hatua lakini bila mafanikio.

Hata hivyo,nimejikuta na orodha ambayo naweza kuita orodha ya viporo licha ya watu kulalamika, kushauri,kutoa maoni na matamko na pia hata kuandamana.Leo limekuja tamko la jukwaa la wakristo ambalo nalo litapita kama yalivyopita mengine ya awali.Lakini ipo siku tutajuta kwa kuacha mambo haya kama viporo.

Orodha ya viporo hivyo vilivyotia fora mpaka sasa katika awamu hii ya nne ni hivi vifuatavyo:-
1.Matatizo/kero za muungano
2.Kashifa ya richmond/Dowans k
3.Mgao wa umeme
4.Mateso/kupigwa kwa Dr.Ulimboka
5.Migomo ya walimu na madaktari
6.Kashifa ya Jairo
7.Mabilioni ya uswisi
8.Vurugu za kidini(uchomaji makanisa)
9.Polisi kuua raia hovyo hovyo
10.Mauji yenye sura za kisiasa.

Ukiangalia katika orodha hiyo mambo yote hayo yameachwa kama viporo.Sasa swali mpaka awamu hii ya nne ifikie tamati huo mzigo wa viporo utakuwa mkubwa kiasi gani!Je mzigo huo utabebwa na awamu ijayo?

Wacha tusubiri,maana wao wameshika mpini na sisi tumeshika kwenye makali.
 
Hapo ongeza Mgodi wa Kiwira na ishu ya Meremeta,na kifo tata cha balali pamoja na babu wa Loliondo
 
Ongeza na hizi:-

Uchunguzi na kusimamishwa kazi KWA Blandina Nyoni na Deo Mtasiwa
 
Back
Top Bottom