Serikali ya awamu ya 5 kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa utoaji haki

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,485
18,045
Utawala huu wa awamu ya tano umekuwa utawala wa hovyo sana toka nchi hii kupata uhuru wake, ni utawala unaotoa haki kwa double standard sana

Wakati anaingia madarakani Rais Magufuli alianza kuvunja katiba na sheria za nchi kwa kupiga marufuku shughuli halali za vyama vya siasa (upinzani) maana ccm wao waliendelea kuzunguka nchi nzima pamoja na yeye Rais Magufuli alikuwa anazunguka nchini kwa mwamvuli wa ziara za kiserikali, lakini ukweli hazikuwa ziara za kiserikali maana alikuwa anapokea wanachama wapya wa ccm kutoka vyama pinzani.

Mara baada ya uchaguzi mkuu 2015 aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema kwa muungano wa Ukawa Edward Lowassa alitaka kuanza ziara nchi nzima kuwashukuru wapiga kura wake milioni 6, lakini alipigwa marufuku kufanya hivyo kwa sababu za kijinga kwamba siasa hadi 2020.

Leo hii Edward Lowassa amerudi ccm ameruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa sababu yuko ccm! Lakini Wapinzani wanaambiwa wafanye mikutano kwenye majimbo yao ya uchaguzi pekee vinginevyo wataishia jela, hii ni hatari sana kuwa na rais anayenyima haki wananchi wake.

Tumeona mahakama ilivyogeuka kuwa sehemu uporaji haki kwa wakosoaji wa serikali hii, wale mahakimu/majaji wenye kukandamiza haki za wapinzani wamekuwa wakizawadiwa nafasi za juu zaidi maana msimamizi wa haki amegeuka kuwa mporaji wa haki za wananchi.

Tumeona wapinzani wakipigwa, kujeruhiwa na hata kuuawa lakini hakuna siku Rais aliwahi kunyanyua mdomo wake na kuviagiza vyombo vya usalama kukomesha matukio hayo, kwenye tukio la kupigwa risasi Mh Lissu aliishia kutweet tu kana kwamba halikuwa tukio la kusikitisha.

Wakosoaji wakubwa wa serikali hii wamekuwa wakipitia maisha magumu sana kwa awamu hii, wako watu wamefilisiwa, kuuawa, kujeruhiwa na wengine kubaki na vilema vya maisha lakini vyombo vya usalama vimekuwa na makengeza juu ya matukio hayo.

Tukio la kushambuliwa Mh Lissu na serikali kukataa kumpa haki zake za matibabu pamoja na kukataa kufanya uchunguzi wa tukio hilo ni ushahidi wa wazi kuwa serikalini kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa utoaji haki nchini.

Tumeona rangi yao halisi hakuna jambo jema na lenye maana kama kuongea ukweli usiowapendeza watawala wasiotenda haki katika jamii.

Tunalazimishwa kuwa kimya kwa sababu eti kuna maendeleo yanafanywa! Huu ni aina ya ukoloni kama ule wa kabla ya uhuru 1960, binadamu hakuumbwa kula na kufanya kazi tu, hata katiba inatoa uhuru wa watu kuongea, kukosoa na kukosolewa na haki ya kwenda popote, haki ya kukutana na kukusanyika.

Wakoloni walijenga miundo mbinu, hospital, shule n.k lakini tuliwakataa kwa sababu walitunyima haki yetu ya asili, haki ya kujiamulia, kushirikishwa, kusikilizwa, kulindwa na kukusanyika, leo haya yote tumenyimwa kwa kigezo kile kile cha kikoloni kujengewa reli na barabara, tunataka sheria na katiba iwe ndio muongozo wa kitaifa, hatuhitaji urais wa kifalme katika karne hii ya 21 wakati sisi ni democratic society.

Tunahitaji kuona mamlaka ya nchi ikipambana na hali mbaya ya;

Uchumi
Elimu bure mbovu
Biashara kudorora
Usalama wa raia
Kilimo
Umoja wa kitaifa
Utawala bora
Haki za binadamu
Deni la taifa
Uduni wa maisha
Diplomasia ya kimataifa, n.k

Bado ccm ni ile ile haina dhamira ya kweli kujenga taifa lenye watu wema na waadilifu wanaoweza kujitoa muhanga kulinda maslahi ya umma kwa gharama ya kukosa.
 
Toka mwaka 1995 mnadai mnanyimwa haki....Mwinyi,Mkapa na kikwete wote hawa mlisema hawawapi haki.!!
Acheni ulaghai wenu pambaneni na mwenyekiti wenu aliyefanya biashara mwaka 2015 sasa mmekula hasara.
 
MTU ambaye hafuati katiba na sheria atatendaje haki ,mbaya zaidi waliompa madarakani hayo hawamwambii ,hawamkosoi ,hawamwelekezi kuwa anakosea sana ,na nchi imemshinda kabisa kabisa .
 
Hilo suala la kijenga miundo mbinu lisiwe utetezi wa kuvunja haki za binadamu

Je katika bara la Afrika kuna miundo mbinu ya hali ya juu zaidi ya ile iliyoko Afrika Kusini??

Hata hivyo enzi zile za utawala wa ubaguzi wa rangi, dunia haikujali hayo maendeleo waliyokuwa wakiyaleta hao makaburu wa Afrika Kusini,badala yake dunia nzima iliungana katika kuiwekea vikwazo hao makaburu

Ni muda muafaka kwa Jumuiya ya kimataifa kuanza kuiwekea vikwazo serikali hii ya awamu ya 5 kutokana na kuisigina waziwazi Katiba ya nchi na kufanya upendeleo wa waziwazi kwa wanaccm, na kuwaona wapinzani wa nchi hii kama wakimbizi "haramu" ndani ya nchi yao!

Wala huo ujenzi wa reli ya Standard Gauge na hui umeme kutoka kwenye maporomoko ya mto Rufiji isiwe sababu za kututia upofu wa TZ, kwa kuwa hata wale makaburu walifanya maendeleo makubwa sana kwa nchi ya Afrika Kusini, lakini haikuwa excuse ya kutowwkewa vikwazo vya kiuchumi
 
NAOMBA BEI YA HIZI BUNDUKI; AK 47, SMG, REVOLVER, PISTOL kwani nimegundua kuna upande flani tu ndo unamiliki ndo maana tunasumbuana
 
HALI ITAZIDI KUWA MBAYA KUFUGA HILI BUNDI LITATUFYEKELEA MBALI NAOMBA AJITOKEZE MUUNGWANA ATULETEE MASHINE TUZAME PORI TUANZE KUWATUNGUA MMOJA BAADA YA MWINGINE MIMI NIPENI KAZI YA KUBEBA KICHWA CHA BASHITE
 
MNAJUA WANAPOUA WATU HALAFU TUPO KIMYA WATAOTA MAPEMBE HEBU MASHINE ZILETWE TUZAME PORI TUWANYIME RAHA MAANA HAIWEZEKANI WATU WAMEPAKATA MABINTI HUKU WAKINYONYA CHUCHU SAA SITA HALAFU WENGINE WANAUGULIA MAUMIVU YA RISASI KIUKWELI INAKERA NAFIKIRI HEBU TUANZE MCHAKATO WA KUZAMA PORI ILI WAKIMPOTEZA AU KUUA MMOJA BASI NAO KADHAA WAPOTEE BAADA YA HAPO WATAKOMA HUU UPUMBAVU MAANA HAWAWEZI KUACHA KIRAHISI KWAKUWA WAMESHAKULA NYAMA YA MTU HAHWEZI KUACHA
 
Wala huna haja ya kuwa na wasiwasi mkuu , kila dhuluma italipwa , tena si muda mrefu
 
Toka mwaka 1995 mnadai mnanyimwa haki....Mwinyi,Mkapa na kikwete wote hawa mlisema hawawapi haki.!!
Acheni ulaghai wenu pambaneni na mwenyekiti wenu aliyefanya biashara mwaka 2015 sasa mmekula hasara.
We kweli jingalao.
 
Back
Top Bottom