Serikali ya Awamu 5 yapania kuokoa maisha ya wanawake nchini kupitia mpango wa damu salama kwa kukusanya chupa 32,700

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
263
500
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) umesema unatarajia kukusanya chupa za damu 32,700 nchi nzima ili kuokoa maisha ya akinamama wanaojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Akizungumza na MTANZANIA katika Mahojiano maalum, Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji damu, Dk Aveline Ngasa alisema ukusanyaji damu huo unaambatana na kampeni iliyoanza jana Septemba 21 hadi 25 kwa kulenga maeneo yote ya mijini na vijijini.

Alisema katika kampeni hizo za ukusanyaji damu kauli mbiu ni ‘Damu salama Uhai wa Mama’

“Ukosefu wa damu unasababisha vifo vya kinamama ambapo moja ya tatu ya vifo hutokea kwasababu hiyo na ripoti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kuna vifo 556 kwa kila kizazi 100,000 na vifo hivyo ni asilimia 18 ya vifo vyote vya wanawake wenye umri chini ya miaka 15-49.

“Mama napoenda kujifungua katika kituo cha afya anaweza kupata shida ya kuvuja damu na akahitaji kuongezewa lakini kama haipo ataongezwa nini? Hii husababisha kupoteza maisha,” alisema Dk Aveline.

Alisema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujitokeza kuchangia damu na kufikia lengo la ukusanyaji damu katika kampeni hizo.

“Hadi sasa kiasi cha mwitikio sio kidogo watu wanajitokeza kuchangia damu lakini tunataka kufikia matarajio yetu hivyo tutaendelea kuhamasisha watu wajitokezwa zaidi.

“Kila mwaka uhitaji wa damu ni chupa 550,000 hii ni sawa na asilimia moja ya idadi ya watanzania na tumejigawa kwa timu ya Halmashauri 185 wanatakiwa kukusanya chupa 150 kwa kila mmoja,hospitali za kanda chupa 500,timu ya mikoa chupa 150 na timu ya damu salama vituo vya kanda chupa 500,” alisema Dk Aveline.

Alisema Kanda ya kusini imehamasika zaidi katika zoezi la uchangiaji damu hivyo yapo maeneo ya vijijini yanahamasa kubwa.

Dkt. Aveline alitoa wito kwa jamii kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kufanikisha kampeni hizo.

“Jamii hasa vijana wajitokezea kuachangia damu kuanzia umri wa miaka 18 hadi 65 ndio wanaruhusiwa kutoa damu, uzito unaotakiwa ni kuanzia kilo 50 na mchangiaji asiwe na ugonjwa wowote,” alieleza.

Chanzo: Mtanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom