Serikali, Wenye Hisa za NICOL ndio wameliwa au...?

Humu kwenye NICOL na Mengi si yumo?and he is among the directors wanaotaka ku resign?teh teh kazi anayo mwaka huu
 
Ndugu zangu habari za leo!!!Napenda kufahamishwa kuhusu lile kampuni ya NICOL ambayo ilianza kwa nguvu kubwa mbona sijaisikiia teena!!!!
 
Ndugu zangu habari za leo!!!Napenda kufahamishwa kuhusu lile kampuni ya NICOL ambayo ilianza kwa nguvu kubwa mbona sijaisikiia teena!!!!

Hivi ukichangia harusi, halafu harusi ikafanyika lakini ndoa ikavunjika, unaweza kurudishiwa mchango wako? Ha Ha Ha, walionunua hisa NICOL wahesabu maumivu.
Japo ninaamini kuwa ndani ya uongozi wa NICOL kuna watu wapo serious lakini walilaghaiwa na baadhi ya miomgoni mwao na hatimaye kufanya maamuzi yaliyoiangamiza NICOL. Maamuzi kama haya hufanyika kila leo katika Mashirika na Taasisi za Umma lakini hakuna anayeumia moja kwa moja ndiyo maana hakuna kelele, na hakuna wa kuhoji.
 
UFISADI MKUBWA TANZANIA FISHRIES DEVELOPMENT COMPANY LTD
KIWANDA TANZU CHA NICOL.

Inasikitisha kuona kuwa hata sisi watanzania wenyewe tunafanyiana ufisadi bila aibu. NICOL ni kampuni ya uwekezaji ambayo maelfu ya watanzania ni wanahisa, Na hii ni baada ya msukumo wa nguvu uliofanywa na baadhi ya watanzania kwa lengo zuri na propaganda ya “Tuungane pamoja tuumiliki uchuni wetu”. Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa kauli mbinu hiyo imebakia kwenye makaratasi baada ya miradi iliyoanzishwa na hao waheshimiwa kuonyesha udhaifu mkubwa mpaka tunajiuliza huu uchumi tutaumiliki kwa staili hii?

Baada ya kushindwa kwa NICOL kufanikiwa katika biashara tutamkumbuka sana Rais Mstaafu Mh Benjamin William Mkapa ambaye kwa nguvu zote aliwakatisha tamaa kuwa miradi kama hiyo kwa silka ya watanzania ama waafrika haiwezi kuendelea. Leo hii tunajionea wenyewe kushindwa kwa kiwanda cha madawa Moshi ambacho kimeshafungwa, na pia kiwanda cha samaki Mwanza ambacho kimekwisa simama uzalishaji mwaka mzima uliopita na tayari bank ya ABC imeshatangaza kukiuza baada ya kushindwa kurejesha mkopo.

Lakini madhumuni ya kuandika habari hii ni ufisadi wa kutisha uliofanywa na maofsa wa NICOL na TFDC katika kiwanda cha Samaki Mwanza (Tanzania Fisheris Development Company LTF). Kiwanda hiki kilikuwa kinaongozwa na raia wa India, Ndugu Awadsh Shrivastava, ambaye mpaka leo inashangaza ni kwa nini alipewa wadhifa huo wa kuendesha kiwanda cha wazawa, na sasa ametoroka nchini baada ya kuhakikisha kuwa kiwanda kimekufa. Hivi ni kweli katika zama hizi hakuna mtanzania anayeweza kuwa Meneja Mkuu wa kiwanda mpaka tuajiri kutoka nje?. Kweli tunawahitaji wageni waje kutusaida, lakini nadhani katika nyadhifa za utaalamu ambapo hakuna mzalendo anayeweza kufanya.

Lakini baya zaidi ni namna ambavyo mhindi huyu analivyonyanyasa watanzania. Mpaka sasa kuna watanzania wataalamu sita ambao ama wameondoka wenyewe kukimbia manyanyaso ama wamefukuzwa kazi bila sababu zozote za msingi. Na jambo la kushangaza ni namna uongozi wa NICOL ulivyomlinda wakati hata tija yake haionekani kama nitavyoanisha hapa chini. Kuna haja ya watanznia kuamka na kusema wageni waje lakni kunyanyaswa hapana.

UFISADI

Mradi huu toka uanze mpaka sasa tunapozungumza umegubikwa na ufisadi wa kutisha, jinsi ambavyo raia wanchi hii, wanahisa wanavyoibiwa mchana mchana tena kwa bahati mbaya na watanzania wakishirikiana na huyu mhindi. Hapa chini nitaainisha mambo kadhaa ambayo nadhani ni vyema wanahisa wakayajua haya. Kwa taarifa tu ni kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari-June 2009 kiwanda kimefanya hasara ya zaidi ya shs 1.5b/=. hii ikupe picha ya aina ya uongozi iliyokuwapo pale.



  1. UJENZI WA KIWANDA.

Inasikitisha kuwa ujenzi wa kiwanda kilichogharimu zaidi ya Shilingi Bilion sita kufanywa kiholela na hasa ikitiliwa maanani kuwa kiasi cha shs 4b/= ni fedha za mkopo kutoka banki (ABC). Hapakuwa na mkandarasi maalum aliyepewa tenda ya kujenga na badala yake wakawa wanaweka mafundi uchwara wa mitaani kujenga majengo. Matokeo yake ni kuwa ujenzi umefanywa chini kabisa ya kiwango.

Labda jambo la kushangaza ni kuwa inawezekanaje kampuni ya umma kama ilivyo TFDC ikajngwa na kutumia mabilioni ya fedha bila kufuata SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA? Vifaa vya ujenzi vilkuwa vinanunuliwa kiholela tu kwa wahindi jijini Mwanza bila hata utaratibu unaoeleweka. Hii iliweka mianya ya rushwa na huo ndio ukweli wote. Inashangaza kuona Mkurugenzi wa Fedha wa NICOL akihamia Mwanza eti kusimamia ujenzi. Si hivyo tu inashangaza kumwona hata Mwenyekiti mwenyewe wa NICOL akihamia Mwanza kwa wiki tatu ama mwezi eti kusimamia ujnzi. Tulishuhudia jinsi Meneja MKuu na maofisa wa NICOL wakipigana vikumbo kudai 10% zao kutoka kwa wahndi. Kutokana na ununuzi huo holela, mpaka hii leo kiwanda kinadaiwa zaidi ya Shs 500m/= kwa wahindi zilizotokana na ununuzi holela wa vifaa vya ujenzi.

Katika barua ya wakaguzi kwa utawala (Managemnt Letter)(imeambatanishwa) ya ukaguzi wa mahesabu kufikia December 2007 ulibaini kuwa zaidi ya shs 200m/= zililipwa wakati wa ujenzi bila kuwa na vithibitisho ( Supportive documents), kwa maana rahisi ni kuwa hizo fedha zililipwa bila maelezo yoyote. Hiki ni nini? Watanzania maskini waliochanga fedha zao ndogo ndogo leo wanaibiwa hivi hivi. Ufisadi wa kutisha. Labda jambo la kushangaza zaidi ni ukweli kuwa hata wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi hawana taarifa hii, ina maana wamefichwa ukweli huu. Kiwanda sasa kimelemewa na madeni makubwa na kinaendeshwa kwa hasara kubwa.

Mashine kukuu za kufulia nguo zililetwa toka Osterbay Inn Hotel, Dar Es Salaam ambayo ni hotel ya afisa wa ngazi ya juu wa NICOL. Mashine zilikuwa mbovu na hazikufanya kazi kwa takriban mwaka mzima. Kwa maagizo ya afisa huyo kiwanda kikagharimia zaidi ya shs 7m/= kukarabati. Pamoja na kukarabati mashine hizo bado huyo mheshimiwa aliendelea kudai shs 30m/= kama gharama za hizo machine. Kwa shs 30m/= tungeweza kupata machine mbili kubwa na mpya. Huu kama si ufisadi ni nini?

  1. MWANZO WA UZALISHAJI

Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alikifungua rasmi kiwanda hiki tarehe 12/05/2008 na jambo la kushangaza ni kuwa hata baada ya kukifungua kwa mbwembwe nyingi bado hakuna uzalishaji wowote uliofanyika. Hii inatokana na mipango mibovu isiyokuwa na mwelekeo ya Ndugu Felix MOsha na wenzake.

Ilisubiriwa mpaka mwezi November 2008 ndipo uzalishaji ukaanza baada ya kupata fedha za mkopo ka ajili ya uendeshaji kutoka ABC Bank. Hata hivyo uzalishaji ulianza bila kuwa na soko la kuuzia bidhaa hizo, matokeo yake store ya minofu ikajaa na kufurika na uzalishaji ukasimama tena. Mipango mibovu. Inawezekanaje tukawa kama vipofu tunapoendesha kiwanda kama hiki huku tukijua kuwa maelfu ya watanzania wanatamani kuona ufanisi wake kama kiwanda pekee kitakachowahakikishia gawiwo kila mwisho wa mwaka?

  1. MKATABA KATI YA NICOL NA CAMS.

NICOL iliingia mkataba mbovu na kampuni ya CAMS ya Uingereza ambayo ilikuwa na jukumu la kuishauri NICOL katika hatua za ujenzi na ununuzi wa mashine za kiwanda. Pia mkataba ulikuwa unawapa CAMS utawala wa kiwanda na kutafuta masoko ya minofu ya samaki katika soko la ulaya. Ujenzi wa kiwanda haukukamilika kama makubaliano yalivyokuwa, CAMS hawakufanya kazi ya kutafuta masoko na pia hawakukubali kuchukua uongozi wa kiwanda. Yakawa ni malumbano tu yasiyoisha na hakuna kitu kiliendelea.

Hata hivyo NICOL ikakurupuka kuvunja mkataba bila kujua madhara yake, na sasa kiwanda kimekufa. Baya zaidi ni NICOL kumwamini huyo Meneja Mkuu raia wa India Awadesh Shrivastava kama ndiye moyo wa kiwanda wakati kila mmoja alijua kuwa yeye ndiye mwizi no 1. Huyu jamaa aliletwa na CAMS hapa nchini, na ni yeye aliyeweka fitina na kugombanisha NICOL na CAMS, alifanya hivyo akijua kuwa kama ndoa ya NICOL na CAMS itavunjka basi yeye atafanya kazi chini ya NICOL, kwa kuwa CAMS walishamchoka na walidhamiria kumuondoa. Alifanikiwa katika njama zake hizo na mpaka sasa yeye ndiye bosi hapo na anafanya anavyotaka.

  1. UENDESHAJI WA KIWANDA BAADA YA MKATABA WA CAMS NA NICOL KUVUNJIKA.

Mara baada ya mkataba huo kuvunjika Bwana Awadesh akaachiwa kufanya apendavyo. Sasa akaanza kufanya vita na wazalendo ambao walikuwa wanazuia njama zake za kutaka kuchuma kupitia kiwanda hiki. Kama ilivyoelezwa hapo awali wizi wa jamaa ulianzia wakati wa ujenzi wa kiwanda akishirikiana na wahindi wenzake hapa Mwanza. Yeyote aliyeonekana ni tishio na anauliza maswali ilikuwa ni lazima aondoke. Afisa Ununuzi, Afisa Usafiri na mipango, Fundi wa mitambo ya barafu, Afisa Rasilimali watu, Meneja mkuu mpya, na mwisho mneja mpya wa ununuzi wote hawa walitimka baada ya kuona hapakaliki. Huyu ndugu Awadesh hakuishia hapo, akaidanganya Bodi ya Wakurugenzi na kumfukuza kazi Meneja Utawala na Fedha, na meneja Ununuzi, kwa sababu zisizo za msingi.

Huwezi kuamini kuwa huyu mhindi ndiye aliyetafuta masoko ya minofu, yeye ndiye aliyekuwa anasimamia upakiaji wa minofu ya samaki kwenda nje na yeye ndiye aliyekuwa anaandaa Ankara (invoice), na yeye peke yake ndiye aliyekuwa anwasiliana na wanunuzi wa bidhaa. Hakuna mzalendo yeyote aliyeruhusiwa kuwasiliana na wanunuzi wa nje. Baya zaidi ni ukweli kuwa hapa anatudanganya kuwa bei ya kilo moja ya minofu ya samaki ni kati ya $ 5-6 katika soko la ulaya, wakati kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa kilo moja ya samaki kwnye soko hilo ni $ 7-9. Na hapa kuna wizi mkubwa uliofanyika dhidi ya maslahi ya wanahisa wanyonge watanzania. Wasiwasi wetu ni kuwa tofauti ya bei hapa ilikuwa inakwenda katika mfuko wake mwenyewe huenda na Mosha, na ndiyo maana alifanya siri kubwa kwa wazalendo kuwasiliana na wanunuzi wa minofu ulaya. Utashangaa kusikia kuwa katika kipindi cha miezi sita tuu, Jan-June 2009 kiwanda kilifanya hasara ya zaidi ya shs 1b/=. Sababu ni dhahiri, bei ya kuuzia ni ndogo ukilinganisha na gharama za uzalishaji. Hii sio hasara halali bali ni matokeo ya kuibiwa fedha zetu kwenye bei tunayouzia minofu ulaya.

Mfano mdogo wa sababu ya hasara hii ni kama tukio hili. August 12, 2009 kiwanda kilinunua tani 3 za Fresh chilled Fillet kutoka kiwanda cha Nile Pirch kwa $ 5.40 kwa kilo ili kupeleka kwa masoko yaliyo tayari ulaya. Jumla ya shs 21m/= zililipwa tena kwa fedha taslimu, hakuna Ankara (invoice ) yoyote kutoka katika kiwanda hicho, wala hakuna stakabadhi inayoonyesha kuwa fedha hizo kweli zimepokelewa kule. Kinachopatikana ni GRN (Goods Received Note) ya kiwandani kwetu inayoonyesha kuwa mzigo umepokelewa kiwandani. Utashangaa kusikia kuwa Ndugu Awadesh na Ndugu Akonaay wao wawili ndio walienda kulipia huo mzigo. Hiki ni kituko cha ajabu. Lakini baya zaidi ni kujua kuwa minofu hiyo iliuzwa kwenye soko la ulaya kwa $ 5.65 kwa kilo. Hii maana yake ni kuwa tunapata faida ya awali ya $ 0.25. Kwa kilo 3000, faida ni $ 750. Hapa hujazungumzia gharama ya kukodi gari kwenda Nairobi, hujazungumzia Royalty ambayo lazima ilipwe serikalini, hujaulizia gharama za mpakani, hujawapa posho madereva. Hii ni biashara kichaa, na haitakiwa iendelee hivi.

Ili ujue kweli huyu mhindi alipanga kuiba, alipanga safu ya wahindi wenzake katika sehemu nyeti za kiwanda. Kwenye upokeaji wa samaki kaweka mhindi, kwenye ukataji wa samaki yuko mhindi, kwenye usindikaji yuko mhindi, kwenye stoo ya minofu yuko mhindi, wakati wa upakiaji hakuna mzalendo anaruhusiwa kuwepo, Ankara anatengneza yeye, mawasiliano nje ni yeye. WATANZANIA TUNAIBIWA MCHANA KWEUPE!!. Kuanzia mwezi wa 7 2010 kiwanda kilisimama kuzalisha kwa kisingizio kuwa hakuna fedha za kununulia samaki. Tunachojiuliza fedha za mauzo ya samaki ziko wapi? Zinakwenda India bila sisi kujua. Tulishuhudia mawakala wa kuleta samaki wanapopewa cheque feki na usumbufu usio wa kawaida.

Kituko kingine ambacho inasikitisha Mosha kulibariki ni pale ambapo kiwanda kilishindwa kuwasilisha makato ya kodi za wafanyakazi TRA. Huyo mhindi akatoa fedha za ofisi Shs 6m/= na kutoa hongo kwa maofisa wa TRA, deni hilo likafutwa kwenye vitabu vya kampuni kana kwamba kiwanda hakidaiwi. Suala hili lilitolewa taarifa TAKUKURU na haijulikani kilichoendelea, sitashangaa kusikia kuwa hata TAKUKURU walikula rushwa.

  1. WIZI WA PESA KWA KUGHUSHI

Katika mwezi wa tano na sita fedha zinazokadiriwa kufikia Shs 40m/= ziliibiwa kwa kughushi sahihi ya meneja mkuu na wajanja wakaondoka na fedha. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa samaki hewa walionunuliwa ni wengi zaidi ya hao waliogundulika. Baada ya kuwafukuza kazi Meneja wa Fedha na Meneja Ununuzi yeye (Awadesh) akabakia kuwa pekee anyetathimini (verify) na kuidhinisha malipo yote, hapakuwa na mtu mwingine wa pili kuthibitisha usahihi wa nyaraka kabla ya malipo, na hii ndiyo sababu hasa ya sintofahamu iliyotokea. NA BADO MTU ALIYEISABABISHIA KAMPUNI YA WAZAWA HASARA YA KIASI HICHO CHA FEDHA ANALINDWA NA BADO YUPO MADARAKANI. Labda jambo jingine la kuchekesha ni kuwa aliamua kuchukua hundi zote na kukaa nazo mwenyewe, na hakuna mhasibu wala cashier aliyeidhinishwa kuulizia chochote banki. Sasa iko wapi dhana ya uwajibikaji?


  1. UTAWALA NA UENDESHAJI WA KIWANDA

Inasikitisha kuwa kiwanda kipya kama hiki kinakabidhiwa kwa MHINDI ambaye hajawahi kupitia elimu ya utawala, wala hajawahi kuwa meneja mkuu popote pale. Njooni mfanye utafiti wa namna kazi inavyoendeshwa. Kwake yeye hakuna mtu mwaminifu hasa wazawa.

Unapokuwa na meneja mkuu mgeni wa nchi hii ambaye hata anathubutu kubeza sheria za nchi na kusema kuwa watanzania hawana akili hii ni hatari. Na kwa kweli tunapenda wageni wataalamu waje kutusaidia lakini si wa aina hii. JE SISI WATANZANIA TUTANDELEA KUWA WATUMWA KATIKA NCHI YETU WENYEWE MPAKA LINI? Baya sana ni ukweli kuwa NICOL ni kampuni ya wazawa tena wengi wa kipato cha chini kabisa, waliotegemea kuwa propaganda za Bwana Mosha na wenzake zingewafaidia kwanza kuumiliki uchumi wetu na pia maendeleo binafsi. Sasa jambo la kushangaza ni kuwa hata watanzania wenzetu tuliowapa dhamana ya kusimamia pesa zetu, wametugeuka na kufanya ufisadi wa kutisha.


MUNGU IBARIKI TANZANIA


 
NBAA na Capital Market zilitilia shaka hesabu za NicoL..
Tunasahau kwamba tutawaachia shida tupu wajukuu zetu siku za usoni kwa ulafi wa sasa..
Tz kweli shamba la bibi...
 
Mkuu mbona wengi tulishawashtukia line up ya wakurugenzi wa NICOL.Jamaa hawa pseudo-politicians wote ni wajanja na walaji, hakuna kitu hapo!
Tunawapa pole wale walioingiza pesa yao NICOL,fedha hazitarudi hizo.
Mfano kama uliotolewa hapa ni matokeo ya ujanja ujanja wa kizila pesa za hizo za wananchi zilizopchangwa kupitia NICOL.
 
Hawa viongozi wa NICOL wote wanatakiwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuwatapeli wananchi. Hii wanayowafanyia wananchi ni pure fraud!! Mpaka leo hawajawasilisha hesabu kwa wanahisa walizoambiwa wazitengeneze na AGM yao iliyopita na ndio maana shares zao haziuzwi pale DSE!
 
Ndugu zangu wapendwa,napenda kufahamishwa kuhusu kampuni ya Wazawa iliyoanzishwa kwa ajili ya kufanya wazawa kumiliki uchumi(NICOL).Hivi kampuni hiii imeishia wapi?
 
hivi kampuni ni kijiwe cha wazee wanaojiita SENIOR CITZEN. kwa sasa mwelekeo wa kampuni ni wa kusuasua sana kwani hata CMSA wameonyeshaa wasiwasi na utendaji wa kampuni hii ambayo ipo DSE.

Jamani hivi hatuwezi hata kuiga kaufanisi ka TRANSCENTURY ya majairani zetuuu??? vijana tuwe mabadilko sahihi kwani hawa wazee wanategemeaa kubebwaa tuu na sio kazii
 
hivi kampuni ni kijiwe cha wazee wanaojiita SENIOR CITZEN. kwa sasa mwelekeo wa kampuni ni wa kusuasua sana kwani hata CMSA wameonyeshaa wasiwasi na utendaji wa kampuni hii ambayo ipo DSE.

Jamani hivi hatuwezi hata kuiga kaufanisi ka TRANSCENTURY ya majairani zetuuu??? vijana tuwe mabadilko sahihi kwani hawa wazee wanategemeaa kubebwaa tuu na sio kazii
typical wabongo, mnafikiria success inakuja over a night! yanayotokea NICOL ni kawaida kwa makampuni mengi tu EA na hata duniani! inaonyesha watu wana agenda zao dhidi ya NICOL ila sishangai kinachotokea ukiangalia wnalipa kodi wakati biashara za kigeni zina misamaha ya kodi! kama Barrick gold
 
Pamoja na ufafanuzi wako Geza Ulole lakini nikiwa kama mwana HISA hakika ukimya umezidi toka kwa viongozi wetu na hata sikumbuki lini nilipata gawio. Unajua siyo wote tunaufahamu unaolingana juu ya uendeshaji wa Kampuni, lakini wengi wetu tulinunua hisa kwa matarajio ya kupata faidi. Sasa hata kama biashara imekwenda alijojo vyema watuhabarishe...
 
na mara nyingi kampuni iliyojiandikisha katika soko la hisa uwazi ni sifa ya kwanza katika utendaji wake..NICOL kwa hilo wamepotezaa maanaa..
 
Jamani kama kuna mtu anafikiria kuhusu NICOL namshauri aanze kusahau, inaelekea kufa kabisa, Kiwanda cha Madawa Moshi kiko chini ya mufilisi, kiwanda cha samaki Mwanza kimesimama kwa karibu mwaka sasa na Banki ya ABC wametangaza kukiuza baada ya kushindwa kulipa deni la karibu 5b. Hali ni mbaya, tumeibiwa pesa zetu, pesa pekee salama zilizobaki ni hisa zilizo NMB, basi. Tuangalie mengine tu lakini uhuni uliofanywa na hao wazee unatisha.
 
Welcome to NICOL
this page will probably help you...

kama TFDC haifanyi vizuri haina maana umeibiwa bali management imefanya wrong investment decision.
Nadhani nicol inasafa sana kwa ajili ya mengi. TFDC ni mradi mzuri sana na serikali ilitakiwa iwape support


moz-screenshot.png
clip_image002.jpg
clip_image002.jpg
hela yako iko humu
clip_image004.jpg




clip_image002.jpg
clip_image002.jpg
 
Baada ya NICOL nani atafuata? tumelizwa TOL,DECI,NICOL nk nini kosa letu. Kinachouma zaidi wanaosababisha mikenge yote hii hawafanywi cho chote cha kujutia kosa lao.
 
Jamani kama kuna mtu anafikiria kuhusu NICOL namshauri aanze kusahau, inaelekea kufa kabisa, Kiwanda cha Madawa Moshi kiko chini ya mufilisi, kiwanda cha samaki Mwanza kimesimama kwa karibu mwaka sasa na Banki ya ABC wametangaza kukiuza baada ya kushindwa kulipa deni la karibu 5b. Hali ni mbaya, tumeibiwa pesa zetu, pesa pekee salama zilizobaki ni hisa zilizo NMB, basi. Tuangalie mengine tu lakini uhuni uliofanywa na hao wazee unatisha.

Tulionya hapa hapa JF juu ya utapeli wa NICOL na wengine walidiriki kutuita kuwa ni watu tusiojiamini kwa kushabikia tu uwekezaji wa kigeni.
Kwa misingi yote ya biashara NICOL ni utapeli wa aina yake, pale ilikuwa si ununuzi wa hisa bali kuwachangia wale WAZEE WASIO NA UZOEFU WOWOTE WA KIBIASHARA, zaidi ya siasa!!!!
Ile pesa watu waliyochanga haikuingia kwenye profitable businesses bali miradi iliyokuwa inakaribia kufa ya hao wazee.Si ajabu kuwa hata mahesabu ya mwaka imeshindikana kuyatayarisha.
 
Watu wakisema wazee wang'atuke kwenye mambo ya kiutawala na uendeshaji wa makampuni inakuwa nongwa,kwa hakika ukiangalia hao wazee wa Nicol ni wazee ambao hawana usongo wa kufanikiwa kimaisha ,kwani tayari kama fweza wanazo,nilitegemea Nicol ingeendeshwa na vijana waliobobea katika uendeshaji wa shughuli za kibiashara ,ikitiliwa maanani kuwa ulimwengu wa kibiashara umebadilika sana na unahitaji nguvu,akili,na vision.Kwa hao wazee wa Nicol hayo mambo kwao ni historia,hata kuchanganyua mizania ya mahesabu inakuwa mbombo ngafu
 
Well Said ILULU, at least tujue kwamba ndio tayari tumeula wa chuya!

Pamoja na ufafanuzi wako Geza Ulole lakini nikiwa kama mwana HISA hakika ukimya umezidi toka kwa viongozi wetu na hata sikumbuki lini nilipata gawio. Unajua siyo wote tunaufahamu unaolingana juu ya uendeshaji wa Kampuni, lakini wengi wetu tulinunua hisa kwa matarajio ya kupata faidi. Sasa hata kama biashara imekwenda alijojo vyema watuhabarishe...
 
Hapo ndipo hasa ninapoanza kuamka na kuona waziwazi kwamba mchezo wa hisa ni sawa na bahati nasibu - get it or loose it. Nakubali huo ni mchezo unaowafaa wenye pesa kubwa, sio wanaookoteza mkate wa kila siku. Binafsi naanza kuona ni dhambi kubwa kwa masikini kuingia mchezo huo hapa nchini. Ikiwa kweli ukitaka kuuza hisa zako huna control kupata pesa yako ila akitokea yeyote anayetaka kununua, tena mwenye kampuni halazimiki kukupa pesa yake kuzinunua hisa zako, mkulima wa Lusonga na Magagula atamudu mambo hayo kama sio kukata tamaa na kuishia, kwa faida ya kampuni hiyo? kama nitarudia tena basi kichwa sio changu.
 
Back
Top Bottom