Serikali wekeni mikakati kabisa kuzuia kupanda bei kwa vitu (mshahara 180,000) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali wekeni mikakati kabisa kuzuia kupanda bei kwa vitu (mshahara 180,000)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UTAJUA, May 9, 2012.

 1. U

  UTAJUA Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuishahuri Serikali iweke mikakati mapema kwa Wafanyabiashara wenye Tamaa na Wasiokuwa na Huruma kuhusu Upandishwaji wa Bei wa Bidhaa na hata Kodi za Nyumba kisa Mshahara umepanda.
   
 2. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio SERIKALI hii....bei kupanda ni Kama kifo na binadamu....lazima.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwani mishahara imepanda?
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Duh bado una imani na hii serikali ya wezi....wao hawajui madhara ya bei ya bidhaa kupanda maana wanajua kesho watakwapua hela sehemu kwa hiyo haiwahusu
   
 5. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Unajua tunaishi maisha ya uongo sana! Eti imepandisha kima cha chini hadi 180,000 hebu tuone tu kwa uchini bajeti ya mtanzania
  *chumba kimoja cha kupanga kwa mwezi kimara at 30,000
  *nauli kuja mjini na kurudi per day 800 mara mwezi 24,000
  *umeme kwa mwezi 30,000
  *maji ya kununua per day 500 per month 15,000
  *hakuna chai, chakula mchana chips kavu 1,000 kwa mwezi 30,000
  *chakula usiku wali kwa mama muuza 1,500 kwa mwezi 45,000

  jumla kwa mwezi 175,000, hii ni bajeti ya mtu mmoja tu ambaye ana sehem ya kulala, nauli ya kuja job na hela ya kula, usihesabu gharama ya extended family wala serving, huyu mtu hatakiwi kuumwa wala asitembelewe na wageni, asipokupigia sim usishangae bajeti yake haitoshi. Halafu tunategemea maendeleo na rushwa kuisha, THUBUTUUU! Waanze wabunge kujilipa mshahara wa 180,000 bila posho wone kawa inawezekana.
   
Loading...