Serikali, Waziri wa Uchukuzi, Wabunge na Wananchi. Mnaliona hili la TAZARA?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
TANZANIA ZAMBIA RAILWAY. hali yake inasikitisha sana. Nenda pale ofisi za Tazara na nenda kaangalie Train zenyewe zilivyo kwa sasa.

Nenda kaangalie vituo vya Tazara huko njiani. Inasikitisha sana.huu ulikuwa mmoja ya miradi mizuri ya usafirishaji Africa kwa njia ya Reli. Ambao tulipaswa anza kujidai nao huu halafu ndo tukaendelea na SGR.

Hali yake kwa sasa ni tete...haina mwonekano mzuri na kiukweli inasikitisha sana. Tazara imekuwa kama ni mtoto aliyekosa wazazi, hakuna anayeiangalia.

Nasikia hata kuna watu wameweka mle ndani visima vya kuhifadhia mafuta yao. Na wengine wamemega eneo na kuweka bahari ya nchi kavu.

Mh. Rais ungepata muda ukatembelea Tazara. Hii Reli inasaidia sana wakazi wa Mkoa wa Pwani, Morogoro, Iringa, Mbeya na Mkoa wa Songwe. Hawa ni Watanzania wenzetu.

Lakini pia inasaidia watanzania wa pande zote ambao wanaweza kwenda Zambia au Mikoa hiyo tajwa kijamii au kiuchumi.

Mabehewa mengi yamechakaa, utaratibu wa zamani kuwa na mabehewa safi na ya kisasa haupo tena. Ratiba haifuatwi ipasavyo.

Haya mambo anayetuhujumi si Beberu ni sisi mbuzi jike wenyewe. Tunapaswa kuamua kutatua matatizo ya reli hiyo kwa kushirikiana na wenzetu Zambia. Ni vyema hata kukawekwa utaratibu wa kila mtu kusimamia kipande chake mwenyewe.

Yaani sisi tunasimamia upande wa Tanzania na wao wanasimamia upande wa Zambia. Maana pengine hii Joint Operation ndiyo imekuwa chanzo cha matatizo kwa reli yetu.

Serikali kadri mnavyokazia SGR ndivyo mkazie pia muendelezo wa matumizi ya TAZARA. Last time nilipanda Tazara kwenda Zambia ili niweze furahia mazingira ya Tanzania. Wakati wa kurudi nliamua kutumia Ndege. Sikuwa na hamu tena. Tazara hii si sawa na ya miaka ile ya 90 nasafiri safiri.
 
Utaambiwa umetumwa na mabeberu. Wakati kiuhalisia hiyo ndio hali halisi...
 
TAZARA inatia huruma sana. Tulikuwa tunapanda sana enzi zetu shule zikifunga.

Wale mliosoma Iyunga, Meta, Sangu, Rungwe, Loleza, Mbalizi, Pandahili n.k mtakuwa mnakumbuka shule zikifunga jinsi TAZARA Mbeya ilivyokuwa inapendeza kwa wanafunzi mbalimbali.

Treni tulikuwa tunaliita gogo!
 
Kuna pesa ilitolewa na wachina kuboresha hii reli lakini kuna jamaa mmoja akapeleka kwenye matumizi mengine na kuacha matajiri wenzake waendelea kuharibu barabara zetu..
 
Adui yetu ni sisi wenyewe kwa kweli.

Kuna pesa ilitolewa na wachina kuboresha hii reli lakini kuna jamaa mmoja akapeleka kwenye matumizi mengine na kuacha matajiri wenzake waendelea kuharibu barabara zetu..
 
Back
Top Bottom