Serikali (Waziri Bashungwa) tafadhali toeni tamko lenu la kimamlaka kuhusu ''Uhuni'' unaendelea kufanywa na klabu ya Yanga

Waulizeni Serikali tafadhali waliouhairisha na siyo TFF ya Rais Bora kuwahi kutokea Wallace Karia au kuanza Kuilaumu Timu ' iliyobarikiwa ' na Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club sawa?
Ikifika hiyo tarehe 3 msipoiona Timu ya Wananchi na Mabingwa wa Kihistoria na Timu pekee iliyochukua Kombe nje ya Tanzania nyinyi wenyewe ndio mtaenda Tifuatifua kuulizia kulikoni.
 
Sasa ni Mwezi unakatika kila ukiamka tu ni lazima ukumbane na Makundi mbalimbali ndani ya Klabu ya Yanga wakisema kuwa hawatocheza Mechi yao na Simba SC iliyopangwa Kufanyika tarehe 3 July, 2021.

Kila hawa Wapuuzi na Wahuni (Yanga SC) kupitia Makundi yao Kuanzia Msemaji wao Mshamba ( Mbwiga ) Bumbuli, Baraza la Wazee na Viongozi wa Matawi wakihojiwa Sababu ya Uamuzi wao huu wanachosema ni kuwa wanataka TFF iwaeleze ni kwanini iliahirisha Mchezo ule ambao Kimsingi ' uliahirishwa ' na Serikali na Ushahidi wa Tangazo husika kila Mdau wa Michezo aliliona na Kulisoma.

Kinachonishangaza zaidi GENTAMYCINE juu ya ' Uhuni ' huu wa Yanga SC ni kuona Serikali ( asa kupitia Wizara husika) ambayo pia inaongozwa na Waziri mwana Yanga SC ' Kindakindaki ' Bashungwa akinyamaza na akiwanyamazia hawa ' Wahuni ' hali inayotufanya Wadadisi na Wachambuzi wa Masuala (Issues) tuanze Kuhisi kuwa huenda hata huyu Waziri nae ni sehemu ya huu ' Mkakati ' wa Kipumbavu (Kipopoma) unaofanywa na Yanga SC.

Waziri wa Michezo Bashungwa na Serikali yako mnaweza mkadhani kuwa ' Uhuni ' huu unaofanywa na Yanga SC hauna ' Madhara ' ila kwa akina GENTAMYCINE tuliobarikiwa ' Maono ' tumeanza Kuona dalili za ' Hatari ' Kubwa hasa katika Soka la Tanzania na Ligi Kuu yetu ila ' Hatari ' kubwa naiona inaweza kwenda kutokea pale Uwanjani ( hasa pale tu Timu moja ) ikifungwa huku ' Mashabiki ' wake wakiwa wameaminishwa Ushindi au kukatishwa Tamaa ya kuwepo kwa Mchezo huo.

Katika hili naiomba Serikali ya Tanzania (hasa kupitia Waziri Bashungwa ) kuwa upesi sana liingilieni Kati, mlitolee Ufafanuzi, mkiri kuwa nyie kama Mamlaka Kuu ya Serikali ndiyo mliamua ' Kuihairisha ' Mechi ile na siyo TFF kama ambayo inatupiwa Lawama na Yanga SC ( na wana Yanga wengi) kuwa wao (TFF) ndiyo ' waliiahirisha ' wakati ' walioihairisha ' kwa sababu wazijuazo Wao ni Serikali hivyo TFF ' Kulaumiwa ' ni Kuonewa tu na Watu fulani (Wapumbavu ) kutafuta sababu kuwa ' Wakifungwa ' basi ' msababishi ' ni TFF kisha waanzishe ' Fujo ' ambayo huenda ' ikaigharimu ' Soka la Tanzania ambalo kwa sasa linakuwa vizuri kwa Matokeo mazuri ya Klabu Bingwa, pendwa na ' iliyobarikiwa ' na Mwenyezi Mungu ya Simba Sports Club.

Tafadhali Serikali, Wizara husika na Waziri mwenye Dhamama tokeni huko ' mlikojificha ' na mlitolee hili ' Sakata ' Tamko lenu la mwisho lenye Mamlaka ili liishe na lieweke kwani kwa Kulinyamazia hivi ni Kutesa tu ' Saikolojia ' za Wananchi ( hasa Wapenda Soka nchini ) na hata wale wasiopenda ila huwa wanafuatilia tu.
Serekali iiguse Yanga, inuke!!
 
Match ilishachezwa tarehe 8 kwa Simba kutoingiza timu uwanjani
Sasa kama ilishachezwa, kuna haja gani ya kutoa matamko? Yaani mechi imeshapita halafu afisa habari na wazee wa utopolo wanapita kwenye media kwamba hatutapeleka timu, sasa kwa nini uzungumzie kutopeleka timu wakati ulishacheza hiyo mechi? Akili zenu aliondka nazo Luc Eymael
 
Nyie ndo wale wanapelekeshwa kama kuku aliekatwa mkia; TFF wameshika makali huku Yanga au Simba wameshika mpini kubali au kataa. Hakuna kanuni iliyofuatwa wala inayowapa TFF kibali cha kusogeza mechi ya Simba na Yanga adi saa moja..na pia hakuna kanuni kanuni iliyowapa TFF kibali cha kusogeza mechi kutoka hiyo saa moja usiku adi tarehe 3 julai.
Kama timu zote zisipojitokeza hiyo tarehe 3 julai bado TFF watawajibika kuisogeza mechi mbele bila sababu yoyote.

Hitimisho la mechi kuchezwa hiyo tarehe 3 ni pale ambapo viongozi wa TFF na Serikali kuwajibishwa au kujiwajibisha kwa kutokufuata sheria zilizowekwa kama ambavyo wanataka au wanawajibisha timu/mwamuzi/au mdau yeyote wa mpira pindi ambapo hafuati taratibu.
Kijiti wamekalia wao TFF/Serikali wakichomoe kwanza. La sivyo mnakwenda kuibiwa tena mia mia zenu za kiingilio hiyo 3 julai.
Sasa kama ilishachezwa, kuna haja gani ya kutoa matamko? Yaani mechi imeshapita halafu afisa habari na wazee wa utopolo wanapita kwenye media kwamba hatutapeleka timu, sasa kwa nini uzungumzie kutopeleka timu wakati ulishacheza hiyo mechi? Akili zenu aliondka nazo Luc Eymael
 
Kwani lazima mcheze na Yango ndo mridhike, si iteni timu nyingine mcheze nayo, waachen Yanga na mambo yao

TFF yenu ndo inavuruga soka la TZ, angalia mizengwe tu ya uchaguzi ndo utaelewa TFF ndo wavurugaji wa kila ktu. sasa mnatafuta kuhamisha lawama kwa Yanga.

Toeni kwanza maamuzi zile kesi 7 za Yanga mlizokumbatia ndo mechi itachezwa, vinginevyo tafuteni wa kucheza naye
 
Kwani lazima mcheze na Yango ndo mridhike, si iteni timu nyingine mcheze nayo, waachen Yanga na mambo yao

TFF yenu ndo inavuruga soka la TZ, angalia mizengwe tu ya uchaguzi ndo utaelewa TFF ndo wavurugaji wa kila ktu. sasa mnatafuta kuhamisha lawama kwa Yanga.

Toeni kwanza maamuzi zile kesi 7 za Yanga mlizokumbatia ndo mechi itachezwa, vinginevyo tafuteni wa kucheza naye
Ubingwa bila kuipiga utopolo 4G haunogi.
 
Sasa hata wakipewa points watakuwa mabingwa? Yanga jitafakarini,timu yenu imeyumba na si ya kishindani tena ipo ipo tu.Na hii ni janja ya kuogopa kucheza na simba ambayo ikiamua kisema ngoja leo tupiiiige hawa ni mtachezea kichapo balaa
 
Back
Top Bottom