Serikali: Watumishi wa Umma kuanza kupandishwa vyeo kuanzia Mei Mosi, 2019

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Mkuchika amewaagiza maofisa na waajiri kote nchini kuwapandisha vyeo watumishi stahiki kwa wakati.

Mkuchika ametoa kauli hiyo bungeni leo Alhamisi Aprili 25 wakati akitoa kauli bungeni kuhusu upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma.

Amesema upandishwaji vyeo kwa watumishi waliokasimiwa katika Ikama na bajeti ya mishahara ya mwaka 2015/16 uliahirishwa Mei 2016 kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi hewa na mishahara hewa na vyeti feki kwa watumishi wa umma

Amesema awamu ya kwanza ya uhakiki ilianza Novemba 01,2017 ambayo ilihusisha uidhinishaji wa taarifa za watumishi 59,967 ambao taarifa zao za kupandishwa vyeo zilikuwapo katika mfumo wa taarifa za mishahara.

“Awamu ya pili ilianza Aprili Mosi mwaka jana ikihusisha watumishi zaidi ya 53,553 ambao walipandishwa vyeo lakini taarifa zao hazikuwa zimeingizwa kwenye mfumo wakati wa zuio tajwa na uidhinishwaji wa taarifa za watumishi 113,520 kwenye makundi hayo mawili kupitia mfumo wa HCMIS umekamilika,” amesema.

Mkuchika amesema baada ya upandishwaji vyeo watumishi wa umma 113,520 , Serikali imewaelekeza waajiri kuendelea na upandishwaji vyeo kwa watumishi 193,166 waliokasimiwa katika Ikama na bajeti ya mishahara kwa mwaka 2017/18 kuanzia Mei Mosi mwaka huu.

Ameelekeza kipaumbele cha kwanza kitolewe kwa utendaji mzuri ambao wanatarajia kustaafu hivi karibuni ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo kabla ya kustaafu

Hata hivyo, ameonya maofisa na waajiri watakaotekeleza kazi hiyo kinyume cha maelekezo yaliyotolewa na Serikali watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
 
Jamani tupate maelekezo kidogo Kwa mfano Mimi niliyeajiriwa mwezi may 2014 na na 2015 nkathibitudhwa kazini . nikawa na sifa ya kupandishwa cheo 2017/18. Lakini kutokana na Yale matatizo ya vyeti hawakutupandisha. Sasa 2018 January nkabahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma masters na December 2019 ntakuwa narudu kuendelea na kazi . Sasa je kutokana na sheria ya utumishi MTU akiwa shuleni hapandishwi mshahara. Sasa nilitaka kujua Mimi itakuwaje watanipandisha au wataniacha kwasababu sifa nilishakuwa nayo kabla ya kuja kusoma. Kuna kuna mtaalam wa utumishi au anayejua mambo haya anisaidie .
 
Back
Top Bottom