#COVID19 Serikali: Watu zaidi ya laki 5 wamepata chanjo ya COVID-19, mikoa iliyofanya vizuri ni Katavi, Lindi na Mtwara!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,882
141,813
Msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesema hadi sasa watanzania zaidi ya laki tano wamepata chanjo ya covid 19 ambayo ni 51% ya chanjo zilizopokelewa.

Mikoa iliyofanya vizuri ni Katavi, Lindi na Mtwara, amesema!

 
Chanjo ni hiari

Wasiochanjwa na waliochanjwa wote wana haki

Mungu ibariki Tanzania
 

Tunaomba takwimu ya Watanzania waliopiga nyungu tangu kuasisiwa kwake...
 
Wanalazimisha wajawazito clinic kuchanjwa vinginevyo hawatahudumiwa ili kusogeza data siyo?
Halafu maeneo yaliyofanya vizuri ni Yale yako nyuma kwa kila kitu,yaani Lindi haifai hata kuwa wilaya.
 
Mwendazake alieleweka Sana, msibani majuzi kiongozi kapewa wasaa Salam , Chanjo ya uviko muhimu, umati ukalipuka "hatutaki"
 
Lindi na Mtwara maambukizi ya Corona yapo chini sana sijajua kwa nini wanakimbilia kiasi hicho na Wasiwasi watakuwa wegeni kwenye Mkoa wala siyo wenyeji

Na kingine Dozi walizopewa kwenye hiyo mikoa ni chache. Tukumbuke kwamba Dozi cha Chanjo zimetolewa kila mkoa kwa idadi kulingana na uwingi wa watu..
Kuna mikoa wamepata dozi 15,000, 20,000, 10,000
 
Msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesema hadi sasa watanzania zaidi ya laki tano wamepata chanjo ya covid 19 ambayo ni 51% ya chanjo zilizopokelewa.

Mikoa iliyofanya vizuri ni Katavi, Lindi na Mtwara, amesema!
Mikoa yenyewe sasa!!!???! Afu watoe na takwimu za waatu walio chanjwa afu wakafa.
 
Back
Top Bottom