Serikali, wanasiasa na jeshi la polisi wanapotosha juu ya swala lilo mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, wanasiasa na jeshi la polisi wanapotosha juu ya swala lilo mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JUST, Jul 19, 2012.

 1. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33


  KWA MUJIBU WA PENAL CODE CAP 16 KIFUNGU KIFUATACHO NDICHO KINACHOTUMIWA VIBAJA. NINAOMBA WAKUELEWA HII LUGHA WASOME NA IKIWEZEKANA TAFASIRI YAKE ILI UKWELI UJIDHIHIRI.


  " 114
  .—(1) Any person who—

  ...........................................................................................................
  ..........................................................................................................

  (d) while a judicial proceeding is pending, publishes, prints
  or makes use of any speech or writing, misrepresenting
  such proceeding, or capable of prejudicing any person in
  favour of or against any parties to such proceeding, or
  calculated to lower the authority of any person before
  whom such proceeding is being had or taken; or

  (e) publishes a report of the evidence taken in any judicial
  proceeding which has been directed to be held in private;

  .................................................................................................."


  NAWAKILISHA
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Ngoja waje wataalam wa sheria tupate ufafanuzi vizuri
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Ndo hapo chacha! Silencing noisy people
   
 4. N

  Ndet Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazee wa ''kwa mujibu wa kifungu no.....'' tusaidieni ufafanuzi wa hicho kifungu
   
 5. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  bhululu hata wewe ukisoma vizuri utaelewa tuu
   
 6. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  ndet nadhani watakuja na kama kuna sheria nyingine watuambie maana watanzania tunaambiwa tu sheria inakataza je ni sheria ipi hiyo? mbona huwa hawaitaji?
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]
  Wadau: Pia someni makala hii iliyotoka ktk gazeti la RAI la leo.
  [/FONT]

  Upotoshaji wa kutozungumzia suala liliopo mahakamani

  * Sasa lengo ni kuziba midomo ya wananchi

  NA HILAL K. SUED

  Napenda kukiri mapema kabisa kwamba mimi si mtaalamu aliyeboea katika masuala ya sheria hususan zile zinazohusu uendeshaji wa kesi mahakamani. Lakini kipo kipengele katika sheria husika kinachokataza kulizungumzia kupitia vyombo vya habari suala la kesi ambayo iko mahakamani.

  Madhumuni ya kipengele hiki ni kujaribu kutoyumbisha mahakama katika maamuzi yake ili haki ipatikane. Lakini sasa hivi inaonekana kumeibuka tabia, au tuseme utamaduni wa kukitumia kipengele hiki vibaya, kama njia moja ya kimakusudi yenye lengo la kuwaziba wananchi midomo ili wasitoe maoni yao katika masuala mbali mbali, hususan masuala ambayo huibuka nchini na kuwa gumzo kubwa na na muonekano hasi kwa watawala, kwa maana ya serikali.

  Sakata la kutekwa na kupigwa vibaya kwa Dk Steven Ulimboka kumeibua mjadala mkubwa sana katika jamii na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii na si kazi kubwa sana kwa mfuatiliaji yoyote kuona kwamba sakata hilo limeikalia kooni serikali kwa kuonyesha ndiye mtuhumiwa mkuu.

  Sasa hivi sakata hilo linatakiwa lisizungumzwe katika jamii kupitia vyombo vya habari kwa sababu tu kuna mtu mmoja kafikishwa mahakamani kujibu shitaka la utekaji wa Dk Ulimboka. Hivyo wananchi na vyombo vya habari tayari vimezibwa midomo na hivyo kuipa amani serklai.

  Mimi nadhani tumefika mahala ambapo suala la kipengele hiki cha sheria lipatiwe maelezo, au tuseme tamko la tafsiri rasmi kutoka Idara ya Mahakama (Judiciary) kwani mhimili huo ndiyo unaoweza kutoa tafsiri kwa ufasaha na usahihi.

  Isitoshe, ni mahakama pekee ndiyo inayoweza kutoa amri ya kukamatwa yeyote yule ambayo anakiuka kipengele hiki na kufikishwa mbele ya mahakama.

  Kwa ufahamu wangu ni kwamba kile kinachokatazwa kuzungumzwa kupitia vyombo vya habari ni mwenendo wa kesi husika kwa kutoa habari zinazokuwa na upendeleo wa wazi wazi kwa upande mmoja – habari ambazo zinaweza kutoa ushawishi kwa mahakimu katika maaamuzi yanayotarajiwa kufikiwa.

  Bila shaka hili liko wazi kwa wengi tu ingawa limekuwa linakiukwa na baadhi ya vyombo vya habari, hususan magazeti na watu wengine. Nitatoa mfano.

  Katika baadhi ya kesi zilizokuwa zikiendelea za kupinga uchaguzi wa Ubunge tulikuwa tunasoma vichwa vya habari vilivyokuwa vina lengo la kuyumbisha mahakama. Hivi ni kama vile “Makongoro Mahanga hoi mahakamani” au ‘Wakili wa Mnyika amsambaratisha Hawa Nghumbi” na kadhalika na kadhalika.

  Kinachotakiwa kuripotiwa ni yale tu yanayosemwa mahakamani na siyo mwandishi wa habari kuweka hisia (opinion) yake, kama jinsi mifano hiyo inavyoonyesha.

  Lakini hakuna kosa kuzizungumzia kesi zilizo mahakamani kwa namna ya kuzitaja tu au kwa namna nyingine isiyo ya kuweka hisia za yule anayezizungumza. Aidha si kosa kulizungumzia suala ambalo halihusiani moja kwa moja (directly) na kesi iliyo mahakamani ingawa kwa ujumla linatokana na suala hilo.

  Mfano: Wiki mbili zilizopita Spika wa Bunge Anne Makinda aliwakataza Wabunge kulizungumzia suala la kutekwa na kupigwa vibaya kwa Dk Ulimboka na watu wasiojulikana kwa sababu eti kesi iko mahakamani. Hii haikuwa kweli, kwa sababu kesi iliyokuwa mahakamani wakati ule ni ile kati ya serikali na Chama cha Madaktari (MAT). Kulikuwa hakuna kesi mahakamani ya kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka.

  Hali kadhalika si kosa pia kuzungumzia suala ambalo liko mahakamani lakini halitaripotiwa katika vyombo vya habari. Sina hakika iwapo ipo katika Kanuni za Bunge kwa Spika kuruhusu suala liliopo mahakamani kuzungumzwa ndani ya Bunge bila ya kuwapo waandishi wa kutoka vyombo vya habari. Yumkini hili lawezekana hasa katika kamati za Bunge.

  Kwa mfano suala la mgomo wa madaktari ambalo Spika Makinda pia alikataza Wabunge kulizungumzia Bungeni lingeweza kuzungumzwa kwa njia hii ili kukidhi matakwa ya Wabunge hao.

  Hata hivyo suala kubwa la kujiuliza hapa ni jee, kipengele cha sheria kinachokataza kuzungumzia kupitia vyombo vya habari suala liliopo mahakamani kinazingatiwa?

  Kama nilivyosema hapo mbele, ni mahakama pekee ndiyo inayoweza kuisimamia suala hili punde tu itakapoona mwenendo wa kesi na maamuzi ya mahakama yanaingiliwa na ripoti za vyombo vya habari.

  Isitoshe kipengele hicho hakitoi ‘msamaha’ (exception) kwa mtu yoyote ndani ya jamii kwani athari yake katika kutafuta haki huwa ni ile ile bila kujali wadhifa wa ‘mkiukaji.’

  Na iwapo ‘mkiukaji’ huyo ni mkuu wa nchi, basi athari katika mwenendo wa kesi huwa ni mkubwa zaidi. Haki inatakiwa isiogope wadhifa wa mtu na hiki ni kitu cha msingi kabisa katika kuisaka haki.

  Nitatoa mfano: Katika hotuba yake kwa taifa mwisho wa mwezi Juni mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, pamoja na mambo mengine alizungumzia kwa kirefu mgomo huo huo wa madaktari wakati kesi baina ya serikali yake na MAT tayari ilikuwa mahakamani. Ikumbukwe siku chache tu nyuma Spika Anne Makinda alikataza kabisa suala hilo kuzungumzwa Bungeni.

  Katika hotuba yake, Kikwete alitumia muda mrefu kutetea upande wa serikali katika mgogoro wa mgomo huo ambao pia ulikuwa unasikilizwa na mahakama. Tafsiri inayopatikana hapa, na ni vigumu kuipinga kwa hoja, ni kwamba Kikwete alikuwa anajaribu kuueleza umma kwa kuonyesha kwamba madaktari ndiyo wa kulaumiwa. Kwa maneno mengine alikuwa anajaribu kuiyumbisha mahakama.

  Kusema kweli hotuba yake iliorodhesha mambo mengi – hasa yale makubaliano yaliyofikiwa, pamoja na yale ambayo hayakufikiwa baina ya pande mbili katika mgogoro huo ambao ulianzia mapema mwaka huu. Haya yote umma ulikuwa hauyajui kwani vikao baina ya pande hizo vilikuwa vya siri.

  Kikwete alienda zaidi ya hapo – siku chahce baada ya hotuba yake serikali yake ilitangaza kuwafukuza madaktari waliogoma na kuwanyang’anya liseni. Wachunguzi wa mambo waliona kwamba hatua hii ni uingiliaji wa moja kwa moja katika kesi ambayo serikali yake ilipeleka mahakamani.

  Kwa kiasi kikubwa hatua ya mkuu wa nchi haikuwa tofauti sana ki-malengo na alivyofanya wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010 pale alipokwenda kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi ambao walikuwa wanagombea Ubunge. Kuna wawili walikuwa na kesi mahakamani.

  Aidha kuna suala la kesi ya viongozi wa Chadema iliyotokana na maandamano ya wafuasi wa chama hicho kule Arusha kupinga mchakato wa kumchagua Meya wa Halmashauri ya Arusha.

  Mwaka jana hili suala lilitinga Bungeni na katika kujibu swali la Mbunge mmoja wa Chadema lililohusu ni nani hasa wa kulaumiwa baina ya polisi na viongozi wa Chadema kwa vifo vya wafuasi watatu wa chama hicho, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema bila kusita kwamba wa kulaumiwa ni viongozi wa Chadema. Wataalamu wa sheria wanaweza wakasema iwapo au la kauli hii inaweza kuathiri maamuzi ya kesi.

  Hata hivyo mara kadha baadhi ya mahakimu na majaji wamekuwa wakisema kwamba wao huwa hawayumbishwi na yanayosemwa nje ya mahakama kuhusu mienendo ya kesi wanazozisikiliza. Inawezekana hii ikawa ni kweli hasa kutokana na kwamba hakuna kesi yoyote inayokumbukwa vyema iliyowahi kufunguliwa dhidi ya mtu au chombo cha habari kilichokiuka kipengele cha sheria hii.

  Lakini pia inawezekana kwamba ukiukwaji wa kipengele cha sheria hii umekuwa mkubwa mno kiasi kwamba mahakimu na majaji wanashindwa pa kuanzia hasa pale miongoni mwa watu wenye wadhifa mkubwa katika jamii nao ni wahusika.
   
 8. m

  mushwabure Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Someni hii article kwa ufafanuzi on this issue.
   

  Attached Files:

 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mhh!!! kazi ipo,swala lipo mahakamani!!!!
   
Loading...