Serikali: Wanaosambaza picha za Rais Samia akiwa kwenye vivutio mbalimbali waache mara moja

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa picha za Rais Samia Suluhu Hassan zinazosambazwa mitandaoni zikimwonesha akiwa kwenye vivutio mbalimbali vya utalii, sio rasmi na hazina kibali cha serikali. Wizara imewaonya wote wanaohusika na kuwataka waache mara moja.


Si wawe wawazi tu - kuwa yuko kwenye kutalii na genge limeshika hatamu?
 
Hii ndio definition ya Dictatorship....

Wangesema tu kwamba hizo sio Rasmi sio kuanza kupigana mikwara mbuzi; huenda intention ya hao watu ilikuwa ni kutangaza Taifa na sio kumdhalilisha yoyote...,
 
Watu wameanza kuzikosoa ndio shida.Mi naona wanawasaidia wazirekebishe na si kuzuia watu kusambaza hizo picha wakati wao ndio walizitoa
Mbona hawazungumzii Ile wa Mnz akisimikwa Uchifu?? Katika historia ya Tanz haijawahi kuwa na Chifu mwanamke. Huku kwetu Masaini haiwezekani mwanamke akakabidhiwa Ile rungu nyeusi ya Malagwanani.
 
Mbona hawazungumzii Ile wa Mnz akisimikwa Uchifu?? Katika historia ya Tanz haijawahi kuwa na Chifu mwanamke. Huku kwetu Masaini haiwezekani mwanamke akakabidhiwa Ile rungu nyeusi ya Malagwanani.
Wamasai wenyewe wa siku hizi wanashinda saluni wakisuka dada zetu tu,nao Ni Kama wanawake tu siku hizi
 
Kwani muhusika mkuu “Hangaya” anasemaje kuhusiana na hili suala. Tuanzie hapo kwanza? 😅😅
 
Wanaochukua hilo tukio na kutengeneza movie ni Royal tour

Ni Sawa na filamu zote zinazotengenezwa wakiwa wana shoot huwezi wewe na kikamera chako koko eti upige na kusambaza bila ridhaa yao

Una uelewa mdogo mno

Kiwango chako cha kufikiri ni cha kuvukia barabara, kuoga na kupiga mswaki.

Umetoa mfano wa filamu. Unataka kusema hawa wanaozuiwa wametengeneza filamu?? Kulikuwa na maelekezo kuwa watu wasitumie picha zao kupiga picha za Rais??

Nia ni maudhui. Je hawa wanaosambaza hizi picha walizonipa bila kuruhusiwa, wanatengeneza filamu inayofanana na Royal Tour ili tuseme sasa maudhui ya filamu halisi yaliyo na copyright yamevunjwa?? Mnapenda kupitisha mambo yenu mitandao ya jamii lakini hamtaki kutambua haki ndogondogo za watumiaji. Kwani kwa kusambaza picha hizo Rais amedhalilishwa, amesingiziwa? Tena picha zenyewe mnato wakati inayotengenezwa ni documentary. Pathetic!!

Ujinga wa nchi hii unakuwa amplified na watu kama wewe. Kujifanya watu wa kamatazo from left, right and center!!
 
IMG_1979.jpg


Wanasema hawa waliotengeneza na kusambaza picha za Mhe. Rais eti hii sio page inayoendeshwa na Wizara ya Utalii? hawa @tzbranding si ndio wana brand ma ROYAL TOUR na Mambo ya Utalii wamewakana leo
 
Bila picha zenyewe kuwepo huu uzi ni fake, umbea na uzushi. Tuzione hizo picha ambazo serikali inasema zisisambazwe.
 
View attachment 1929857

Wanasema hawa waliotengeneza na kusambaza picha za Mhe. Rais eti hii sio page inayoendeshwa na Wizara ya Utalii? hawa @tzbranding si ndio wana brand ma ROYAL TOUR na Mambo ya Utalii wamewakana leo
Kama hiyo page iliyowekwa hizo picha fake inaendeshwa na wizara basi hiyo tayari ni failure. Mfano iweje watumie photoshop kwa kubandika picha hiyo hiyo moja ya rais kwenye maeneo matatu tofauti?
 
Back
Top Bottom