Serikali: Wananchi kuweni makini kabla ya kununua magari Japan

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kufuatia malalamiko ya Watanzania kudhulumiwa wanapojaribu kununua magari mtandaoni, kutotumiwa kwa wakati na kutumiwa magari yasiyo na sifa, Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umewataka wafanye uchunguzi kabla ya kutuma fedha

Umesema ni vigumu kwa fedha ambazo zimeshatumwa kurejeshwa kutokana na Sheria za nchini humo kwani Mamlaka huanzisha shauri dhidi ya mtu/kampuni iliyokiuka mkataba na sio ankara za malipo ambazo wengi huwa nazo

Aidha, Watanzania wanaoagiza magari wametakiwa kutembelea tovuti zaidi ya moja wanapotaka kufanya hivyo ili kufahamu bei za wastani za magari

1601107224292.png
 
Afrika kuna kampun za magari ila bado tunahangsika na gari za mjapani.SA ,Ghzmana na Nigeria kuna kampuni za kuunda magari tens mapya.
 
Kufuatia malalamiko ya Watanzania kudhulumiwa wanapojaribu kununua magari mtandaoni, kutotumiwa kwa wakati na kutumiwa magari yasiyo na sifa, Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umewataka wafanye uchunguzi kabla ya kutuma fedha...
Too little too late
 
Tuhamie South Africa tuunge uchumi wa bara letu. By the way magari ya south Africa ambayo ni under licence yana uimara zaidi kwa sababu wanaunda kwa kuzingatia mazingira ya Africa
 
Hata Rwanda kuna Kampuni ya kuunda magari ya Volkswagen sema hawajajiadvertise sana
 
Kufuatia malalamiko ya Watanzania kudhulumiwa wanapojaribu kununua magari mtandaoni, kutotumiwa kwa wakati na kutumiwa magari yasiyo na sifa, Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umewataka wafanye uchunguzi kabla ya kutuma fedha

Umesema ni vigumu kwa fedha ambazo zimeshatumwa kurejeshwa kutokana na Sheria za nchini humo kwani Mamlaka huanzisha shauri dhidi ya mtu/kampuni iliyokiuka mkataba na sio ankara za malipo ambazo wengi huwa nazo

Aidha, Watanzania wanaoagiza magari wametakiwa kutembelea tovuti zaidi ya moja wanapotaka kufanya hivyo ili kufahamu bei za wastani za magari

View attachment 1581223
Nimeagiza gari toka mwezi tano lakini mpka sahii naelezwa melly haijafika tz, dalili zakupigwa ndio hizi xaxa
 
Back
Top Bottom