Jpm akifufuka leo atahisi alikufa miaka 100 ilopita..mana hii U turn inayopigwa na wapambe zake hawezi amini.

Siasa za bongo bila unafiki huwezi ziishi.

#MaendeleoHayanaChama
Meza zinapinduliwa kibabe mnooo, huo ndio ubaya wa kuwa dikteta uchwara, watu wanakusikilizia tu, ukichomoka tu wanakubadilikia, wengi unaohisi wanakusapoti hawakusapoti, ukweli ni kwamba wanakuwa wanakuogopa tu.
 
Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amesema Wanafunzi wa Shule za Msingi/Sekondari watakaokatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro, mimba na changamoto za kifamilia watapewa nafasi ya kurejea Shuleni katika mfumo rasmi “leo leo natoa waraka zege halilali"

Millard Ayo
Ona wanavyoinajisi nchi. Kwa hiyo tunahalalisha wasichana kuweza kupata mimba shule. Hizi ni pressure za maliberali wa kizungu. Muda si mrefu utaona zile ngo zilizokua zinafunza watoto ushoga kuruhusiwa zirudi. Hata huko ulaya ni marufuku mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule ya msingi na sekondari. Sasa sisi tunafanya uamuzi utakaozidisha tatizo hilo.
R. I. P. Magufuli
 
Na walioshiriki kutoa 'mbegu' wataruhusiwa kulea mimba hizo na kiumbe kitakachopatikana bila kutishiwa mvua 30?
Sheria inasema kumchakaza "Minor" ni sawa na ubakaji, na ubakaji hukumu yake ni miaka 30. But hakuna sheria inayosema mtoto wa kike akipata mimba asirudi shule baada ya kumaliza mambo ya uzazi
 
Jpm akifufuka leo atahisi alikufa miaka 100 ilopita..mana hii U turn inayopigwa na wapambe zake hawezi amini.

Siasa za bongo bila unafiki huwezi ziishi.

#MaendeleoHayanaChama
Hebu tuache ushabiki wa kinafki. Je zuio lile lilikuwa halali? Tusimsakame tu Waziri tujiulize wewe ukiwa na binti yako akabakwa akafukuzwa shule unalionaje wewe tuache unafki hili ndio tatizo la Watanzania. Kwani Mwendazake alikuwa saint? no alikuwa binadamu alifanya makosa Mungu atamsamehe huko aliko.
 
Watanzania kuna kitu hakiko sawa vichwani mwetu.
Na kitu hicho ni ugonjwa wa kupenda kuabudu viongozi " au kitaalamu " leadersiosis"

Hatuwa challenge maamuzi Yao, hatuprotest juu ya chochote wanachoamua hata kama Kiko kinyume na sheria. Iwe kwenye vyama na hasa ccm , bungeni na karibu kabisa hata mahakamani

Leaders' worshipping country nani atatukomboa na mentality h iii
 
Ona wanavyoinajisi nchi. Kwa hiyo tunahalalisha wasichana kuweza kupata mimba shule. Hizi ni pressure za maliberali wa kizungu. Muda si mrefu utaona zile ngo zilizokua zinafunza watoto ushoga kuruhusiwa zirudi.
R. I. P. Magufuli
Wewe endelea kulialia na R.I.P., uamuzi umeshapita tayari!! Unafiki wa awamu iliyopita haupo tena!! Hiyo mijamaa yako unayoiabudu ni mibingwa ya kutembea na vitoto!! Ni basi tu kuna vitu vingine havisemeki hadharani......
 
Watakuwa kwenye mfumo wa elimu ya watu wazima na shule zao zimeshaandaliwa na walimu wanaajiliwa Sasa ila naona wametumia kauli hiyo Ili wasijione wametengwa ila shule watakazosoma ni elimu ya watu wazima watakuwa wanaelekezwa wakifika shule.
 
Viongozi hawa mnaowasifia kucha kutwa kuwa wana maono wakati ni fuata upepo...uje wa shetani au wa Mungu wamo tu. Ajabu prof mzima juzi kasema hili wakati wa JPM na hilohilo kalisema the opposite wakati wa SSH. Mmenikumbusha prof mwingine Kabudi (muungaji katiba mpya wakati wa Kikwete na huyohuyo mpingaji wakati wa JPM na SSH). Kabudi = Polepole=Bashiru! Akatokea Dr Gwajima wa JPM wa tofauti na Gwajima wa SSH juu ya Covid. Nakumbuka Dr Mwakyembe wa serikali 3 kwenye andiko lake la PhD na yule wa serikali 2 wakati wa Kikwete. Hao ni mifano halisi ya nchi yetu kwamba hatuna viongozi tuna wasaka tonge na wafukuza upepo. Wapi kina Waitara na Dr Mollel waliookoka toka CHADEMA to CCM in exchange for cash & political favours kwa maana ya vyeo. Kina speaker Ndugai wa bandari ya bagamoyo wakati wa JPM opposite na wakati wa SSH. Wapo wa priority ya umeme wa maji wakati wa JPM na opposite ya wakati wa Kikwete na SSH wanaotaka gas. Tumwombe Mungu aikoe Tanzania tupate credible leaders otherwise hatuendi popote ndugu zangu, tutalipishwa mikopo mpaka vitukuu. Na la kuogofya zaidi hawa ndio viongozi misikitiki na makanisani wanaonyenyekewa na kupewa priority. Hawa ndio waliojaza watoto wao vitengo vyote nyeti kwamba wawepo na tawala zao unabated. Unless muujiza uje, kama Taifa tutaendelea na mdumange huu. Msiwaamini hawa watu hata siku moja. Tungoje uzao mwingine labda.
 
Sawa tu kwa vile wameamua iwe hivo! Hata huo utaratibu wa nje ya mfumo usio rasmi ulikuwa haueleweki mpaka sasa! Ila angalizo ni umakini wa malezi uzingatiwe maana shule zinaweza kujaa watoto wa mama na kupelekea wasichana wetu kuona mimba ni issue ya kawaida!
Hii sheria ya miaka 30 inapunguza speed ya mafisi, maana ukidakwa lolote linaweza kukutokea
 
Back
Top Bottom