Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,792
- 1,834
Kama Nyerere alianzisha elimu ya watu wazima na ikawezekana, iweje leo uwe mjadala kama msichana akipata mimba arudi aun asirudi shule?Tungekuwa tunaongelea sana neno la kumzuia na kumlinda mtoto mjamzito kupata mimba akiwa shule ingesaidia sana kuliko kuendelea na mtoto mjamzito kuendelea au kutoendelea na shule.....kujadili hivi ni kukubaliana na tatizo..
Tutapambane zaidi na mbinu za kumlinda mtoto wa kike awe salama na ikiwezekana na wa kiume awe salama pia...
Ikigundulika binti kaingiliwa na mtu mzima hata bila kupewa mimba basi mhusika atiwe mbaroni akatumikie 30yrs....ikigundulika mchezo huu wanafanya wenyewe kwa wenyewe watoto walio shule basi wazazi waitwe watoto wahamishwe shule tofauti tofauti na adhabu kali, ikiwa pamoja na wazazi wote kuilipa faini serikali..Ulinzi huu uendane sambamba na ulinzi wa maadili ya jamii nzima...
Juu ya kuwalinda wasichana na mahusiano, hilo lipo tayari. Hata kisheria juu ya hukumu kwa atayepatikana kuwachezea hawa watoto. Lakini tatizo bado lipo, ndio maana ni muhimu kujadili juu ya hatma ya huyu mhusika msichana aliyepata mimba licha ya kuwepo sheria ngumu kwa mwanaume aliyehusika na hayo.