Serikali: Wakuu wa Mikoa na wilaya waache kutoa matamko kuhusu Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
f373026eaf073732faa8508ad034caf4

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa amewaonya baadhi ya viongozi wakiwemo Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwa kutoa matamko na takwimu kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa covid-19 nchini.

Majaliwa amesema hayo jana Jumatatu, Aprili 6, 2020 wakati akihutubia bungeni jijini Dodoma; “Kuhusu homa kali ya mapafu ya virusi vya Corona, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbali mbali na kama alivyosema Waziri wa Fedha, tume imeshaundwa na Serikali itatoa muelekeo kutokana na athari zinazoendelea kujitokeza.

“Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa kila mmoja anatamka atakavyo, nilishasema atakayetoa taarifa za ugonjwa ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na kama itabidi nitatoa mimi mwenyewe na kama italazimika sana atatoa Makamu wa Rais au Mheshimiwa Rais mwenyewe. Utaratibu huu utasaidia kuleta taarifa za uhakika, hii hali ya Wakuu wa mikoa na Wilaya kutoa matamko kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge hapa, haiko sawa.

“Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa nazo zinaratibiwa kutoa huduma ya upimaji sambamba na maeneo ya mipakani. Shughuli hizo za upimaji zinafanyika kwa usimamizi wa Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa lengo la kuthibitisha ubora wa vipimo,”
alisema Majaliwa.
 
Wangejifunza kwa yanayojiri ktk gonjwa hili la korona wangejijua kuwa wao mbali ya kujimwambafai ila ni wadogo kuliko pilton, naangalia apa CNN Gordon brown wa engalnd akipelekwa ICU nadhan kiherehere cha utu tubosi twa nchi ni muda tu Mungu akiamua kuwanyoosha watajua wao si lolote wala chochote.
Ila jamaa wanamuogopa sana. Hakuna mtu wa serikalini anayeweza kusema moja kwa moja kwamba anamlenga yeye!!

Aisee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa mikoa yule alishawaambia wasijione wanavyeo kuzidi yeye anawazidi vingi sana. M aile kauli alilengwa PM na spika nakumbuka
Hahaha mimi siwezi kumlaumu Paulo ila namsifu sana kwa ujasiri wake anaweza kutetemesha mtu yeyote ambaye hajui cheo chake kina nguvu gani. Japo wote ni watoto wa baba mmoja.
 
Back
Top Bottom