Serikali, Wahubiri hawa wana tofauti gani na waganga wa tiba za asili?

Yesu akawaambia wanafunzi wake´Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.Wakabishana wao kwa wao wakisema ni kwa sababu hatukuchukua mikate.
Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mikate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
 
Subiri tuone mwakani kama haohao kama siyo watakao panga foleni kwa waganga wakitaka wawe washindi kwenye chaguzi!
Wenye watoto walemavu wa ngozi TAFADHALI anzeni kuwaficha watoto.
Mwaka wa kafara unakuja.

 
Ni kweri wafuasi wa kibwtere walkuwa na imani, lakini mkuu hebu tuangalie vitabu vitakatifu vinasemaje kabla ya kuhukumu tu bila sababu. Wale wafuasi wa Kibwetere walikuwa wajinga kwani hawakuisoma biblia na kumiamini, Biblia inasema hakuna ajuaye siku wala saa ya siku ya mwisho (Mathayo 24:36), kama wangesoma haya maandiko wasingekubalikuchomwa moto. Kuhusu manabii, imeandikwa kuwa, usiamini unabii kama umetoka kwa Mungu mpaka pale utakapotimia (Jeremiah 28:9). Mengine unaweza kwenda kwenye vitabu hivi(Mathayo 7:15; 24:11 na Marck 13:22). Hiyo miujiza isikutishe ila simama na neno!

Hata hawa wafuasi wa hawa manabii "fake" licha ya wengine kuwa wasomi bado wamekuwa wajinga kupitiliza.

Imani pasipo kutafakari ni hatari sana.
 
Mkuu Salary slip, Unabii na injiri ni kwa wale wanaoamini, hawa ndio huguswa moja kwa moja na injiri hiyo na unabii huo. Kwa wale wasioamini wewe subiri hukumu tu. Hayo waachie wenyewe kwani huamini.
Injiri= INJILI
 
Bila shaka mdau anamzungumzia 'nabii' huyu hapa pichani.
Amelipia kipindi StarTV maalumu kwa ajili ya kuonyesha 'maajabu' yake.
DSCN4875.JPG


DSCN3045.JPG



Check pass yake kama alishaenda Nigeria. Si nasikia ndiyo kuna makao makuu ya Ibirisi?
 
Makao makuu ya Ibilisi ni Makha na sio Nigeria. Mahali hata majini yanaenda hija kweli pana Mungu hapo?
 
Aliyeleta hii habari ni mawili; a.Mganga wakienyeji au mtoto wa mganga waliopigwa marufuku
b.Akisikia habari za Yesu zinamkera sababu anafurahia watu kuwa waovu.
Mbona hampigi kelele baa zikifunguliwa hadi mabarazani mwa nyumba zenu. Watu wanashangilia uovu tuu wanaobadili tabia za watu wanawakera nini?!!!

Sii bora hata hawa watumishi wa Mungu maana mafisadi wote wa eacrow hamna mlokole hata mmoja katajwa. Hamuoni waubiri wanavyozidi kuuomba ndio ufisadi unaibuka maana sasa taifa linapona?
Mtumishi mmoja akihubiri kwa makosa haimaanishi wote wanamakosa.q
 
ni kweri wafuasi wa kibwtere walkuwa na imani, lakini mkuu hebu tuangalie vitabu vitakatifu vinasemaje kabla ya kuhukumu tu bila sababu. Wale wafuasi wa kibwetere walikuwa wajinga kwani hawakuisoma biblia na kumiamini, biblia inasema hakuna ajuaye siku wala saa ya siku ya mwisho (mathayo 24:36), kama wangesoma haya maandiko wasingekubalikuchomwa moto. Kuhusu manabii, imeandikwa kuwa, usiamini unabii kama umetoka kwa mungu mpaka pale utakapotimia (jeremiah 28:9). Mengine unaweza kwenda kwenye vitabu hivi(mathayo 7:15; 24:11 na marck 13:22). Hiyo miujiza isikutishe ila simama na neno!

unafahamu kuwa kuna baadhi ya waumini hawajui kusoma?
 
Hata hao wahanga wa kienyeji wengine bado wanaendelea kujitangaza kwenye maredio na tv tena kwa kueleza wamethibiishwa na serikali! Kuna mmoja anadai ana dawa iliyopasishwa na serikali ya katibu Figo ndani ya siku sababu! Wizara ya Afya kimya...
 
Back
Top Bottom