Serikali, Wahubiri hawa wana tofauti gani na waganga wa tiba za asili?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,222
144,939
Hivi karibuni serikali iliwapiga marufuku waganga wa tiba za asili ikiwa ni pamoja na kung'oa matangazao yao mitaani kwa kile kilichoitwa ni kupotosha umma na kuhatarisha maisha ya watu.

Kama lengo ni kuondoa upotoshaji na kuepusha wananchi kutapeliwa.Je,serikali hii inaridhika na hiki kinachofanywa na hawa wanaojiita wahubiri/manabii kupitia vituo vya Television?

Ukiangalia maombezi ya hawa watu kwakweli unaweza kupigwa na mshangao mkubwa maana siku hizi wamegeuka kuwa manabii,madaktari,wnamazingaombwe n.k.

Leo nimemuona mmoja anaejiita "prophet"(jina nimelihifadhi), akijitangaza kumsaidi ng'ombe wa mmoja wa waumini wake kupata mimba kwa kumpa chupa yenye mafuta maalumu na tukio hilo kuonyeshwa kwenye tv.

Anyway,inawezekana huyu "prohet" anafanya haya kwa ni njema tu, lakini je, kesho na keshokutwa akiibuka mwingine nae tutamuamini?

Huo ni mfano mmoja tu.Kuna wengine watakwambia umelogwa,ndoa yako ina matatizo kwasababu ya mtu fulani n.k.

Wadau,nafahamu mambo haya ni ya kiimani lakni kweli hizi ndio imani tulizorithi au hii sasa ni transformation ya mambo ya kiimani kwa ajili ya kujipatia kipato na kuhadaa watu?

Serikali,je,kuna tofauti ya waganga wa jadi na baadhi ya hawa wahubiri/manabii wa siku hizi?
 
usijali hao wanaeneza neno la mungu. au hajaona wanatembea mpaka juu ya maji kama yule wa kule nnigeria? au hata wale wanaobatizwa kwenye maji kama wale waliopata uhai wa milele kule bukoba-ziwa viktoria?
Ni neno la mungu tu. hakua jingine.
 
Bila shaka mdau anamzungumzia 'nabii' huyu hapa pichani.
Amelipia kipindi StarTV maalumu kwa ajili ya kuonyesha 'maajabu' yake.
DSCN4875.JPG

DSCN3045.JPG

Hehehe yule jamaa tapeli Star Tv pale anaongea ujinga hadi unaogopa eti anamwambia mwanamke hupati mimba sababu umewekea ndizi katika sehemu yako ya siri kiasi kwamba huwezi kupata mimba.
Mwengine alimwambia kama matatizo yanayokupata ni kwa kuwa ulivaa kufuli ya mfanyakazi mwenzako Lol! Ujinga sana
 
Huyo Frank V. Mlawah, ni dhahiri anapotosha ukweli wa neno la Mungu, ni Nabii wa uwongo.
 
Hivi karibuni serikali iliwapiga marufuku waganga wa tiba za asili ikiwa ni pamoja na kung'oa matangazao yao mitaani kwa kile kilichoitwa ni kupotosha umma na kuhatarisha maisha ya watu.

Kama lengo ni kuondoa upotoshaji na kuepusha wananchi kutapeliwa.Je,serikali hii inaridhika na hiki kinachofanywa na hawa wanaojiita wahubiri/manabii kupitia vituo vya Television?

Ukiangalia maombezi ya hawa watu kwakweli unaweza kupigwa na mshangao mkubwa maana siku hizi wamegeuka kuwa manabii,madaktari,wnamazingaombwe n.k.

Leo nimemuona mmoja anaejiita "prophet"(jina nimelihifadhi), akijitangaza kumsaidi ng'ombe wa mmoja wa waumini wake kupata mimba kwa kumpa chupa yenye mafuta maalumu na tukio hilo kuonyeshwa kwenye tv.

Anyway,inawezekana huyu "prohet" anafanya haya kwa ni njema tu, lakini je, kesho na keshokutwa akiibuka mwingine nae tutamuamini?

Huo ni mfano mmoja tu.Kuna wengine watakwambia umelogwa,ndoa yako ina matatizo kwasababu ya mtu fulani n.k.

Wadau,nafahamu mambo haya ni ya kiimani lakni kweli hizi ndio imani tulizorithi au hii sasa ni transformation ya mambo ya kiimani kwa ajili ya kujipatia kipato na kuhadaa watu?

Serikali,je,kuna tofauti ya waganga wa jadi na baadhi ya hawa wahubiri/manabii wa siku hizi?

NENO LA MUNGU linapatikana kwa kusoma BIBLIA PEKEE, ukisubiri au ukitegemea nabii akusomee.... matokeo ndo haya... !!! Akiwa anahubiri au kuonyesha maajabu yake we soma BIBLIA yako, ukiona hayamo anayofanya na kuonyesha,... Endelea na mambo mengine achana na utegemezi katika mambo ya MUNGU...
 
umesema na langu
 
Mtawatambua kwa matendo yao kama ni watumishi wa Mungu au la !

Alama kubwa ya manabii wa uongo ni UTAPELI NA UZINZI NK.
 
Hehehe yule jamaa tapeli Star Tv pale anaongea ujinga hadi unaogopa eti anamwambia mwanamke hupati mimba sababu umewekea ndizi katika sehemu yako ya siri kiasi kwamba huwezi kupata mimba.
Mwengine alimwambia kama matatizo yanayokupata ni kwa kuwa ulivaa kufuli ya mfanyakazi mwenzako Lol! Ujinga sana
Huyu mhubiri kwakweli ananishangaza sana.Alafu anajiita nabii!Maandiko naona yana timia kuhusu mwisho wa dunia.
 
Mpendwa napenda ujue kuwa ck za mwisho manabii wengi watatokea huku wakifanya miujiza mingi ajabu.ni wapunga pepo hao.
 
Aliyetwmbea juu ya maji kule naija mbona alizama na akafa? si utapeli huo?
 
Back
Top Bottom