Serikali: Wahanga wa ajali wanastahili fidia, kuna uelewa mdogo wa masuala ya bima

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza amesema wanaopata ajali au madhara katika Chombo cha Moto ambacho Fidia yake husimamiwa na Sheria ya Bima wanapaswa kulipwa.

Ameeleza hayo baada ya Mbunge Rita Kabati kusemi abiria wengi wanaopata Ajali wamekuwa wakisumbuliwa na wamiliki wa Bima tofauti na hali ilivyo kwa Vyombo vya Moto.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto kwa upande wa Wananchi akitaja baadhi kuwa ni kukosa ufahamu wa namna bora ya uandishi wa kuomba fidia na uelewa mdogo wa masuala ya bima.
 
Hata hivyo amesema bado kuna changamoto kwa upande wa Wananchi akitaja baadhi kuwa ni kukosa ufahamu wa namna bora ya uandishi wa kuomba fidia na uelewa mdogo wa masuala ya bima.
nani alaumiwe, kwanini serikali haitoi elimu kwa umma juu ya masuala ya Bima kama inavyotoa elimu ya maradhi mbalimbali kama UKIMWI, TB nk
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza amesema wanaopata ajali au madhara katika Chombo cha Moto ambacho Fidia yake husimamiwa na Sheria ya Bima wanapaswa kulipwa.

Ameeleza hayo baada ya Mbunge Rita Kabati kusemi abiria wengi wanaopata Ajali wamekuwa wakisumbuliwa na wamiliki wa Bima tofauti na hali ilivyo kwa Vyombo vya Moto.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto kwa upande wa Wananchi akitaja baadhi kuwa ni kukosa ufahamu wa namna bora ya uandishi wa kuomba fidia na uelewa mdogo wa masuala ya bima.
Hawa ni matapeli maana wao ndiyo wasimamizi alafu wanalalamika nini?
 
Aina ya ushahidi uliokiwa unatakiwa kupelekwa na abiria ndio ilikuwa shida sababu unakatiwa ticket wanaandika majina wanavyosikia, mkata ticket unamwambia unaitwa Michael, au Rachel yeye anaandika Maiko, Recho sasa hapo ndio proof gani ya jina kwamba ndio wewe maana ukitoa kitambulisho unakuta jina jingine.

Pia ticket abiria wengi hawajui kuzitunza mpaka mwisho wa safari ili kuwa na ushahidi pamoja haya yote bado unaweza kumdai mwenye gari maana list ya majina naamini anayo kwenye chart ya seats. Pia lazima awe na list kwa ajili ya kumbukumbu na masuala ya kodi.

Kiujumla ni kukosa uelewa na shida inakuja mawakili tumekatazwa kuwa ambulance chasers ingekuwa haipo hiyo sheria kila penye ajali ungekutana na mawakili wanatoa msaada wa kisheria kuhusu fisia. Wenzetu wakisikia ajali vichwa vinauma maana wanajua fidia italipwa kubwa sisi huku mwenye gari anaulizia kama gari imepona ndio anaendelea na abiria

Sheria ni mbovu sana bado tuna mwendo mrefu mno, makampuni ya bima yanapata faida za kumwaga tu nchini sababu tunakata bima Ila hatudai fidia na wameweka utaratibu mgumu mpaka unakata tamaa.
 
Elimu itolewe kwa raia namna ya kudai fidia... Pia kuwepo na njia rahisi za kutambua wahanga wa ajari kisheria...
 
Back
Top Bottom