Serikali, waelekezeni wanaotafuta elimu ya India na China kwa watoto wasio na sifa

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,703
4,697
Kuna wimbi la kupeleka vijana kusoma digrii India na China baada ya form 4 na 6 kwa ufaulu hafifu! Hili ni wimbi jipya lililoanzia Dar. Tukio hili la vyeti feki, liwe fundisho kubwa kabisa kwa wazazi tulio na ’nyodo’ Tumekuwa wataalamu wa elimu ktk familia kuliko hata walioko wizarani. Tunawatafutia watoto wetu shortcuts za elimu ya India na China bila kuangalia siku zijazo itakuwaje.

Kijana anamaliza form 4 au form 6 kwa ufaulu hafifu, mzazi anampeleka kusoma digrii India na China kwa kisingizio cha eti wengine wameweza, bila kujali aina ya elimu inayotolewa india na china kwa wageni. Tunawaponza vijana wetu kwa mazoea ya shórtcuts ambazo huenda wazazi pia walipitia.

Baada ya vyeti feki, tusiwaponze watoto wetu.
 
una hoja ya msingi sana na wengine wanaboreshewa cheti baada ya kulamba 4, au zero na baada ya muda unasikia ni mkurugenz taasis fulani hapa nchini
 
Kijana anamaliza form 4 au form 6 kwa ufaulu hafifu, mzazi anampeleka kusoma digrii India na China kwa kisingizio cha eti wengine wameweza, bila kujali aina ya elimu inayotolewa india na china kwa wageni.
Hapo penye nyekundu: Hilo la ufaulu hafifu tunaweza kukesha hapa tuna bishana. Kila chuo na nchi wana miongozo yao ya udahili. Baada ya serikali kubadilisha gia angani mwaka wa jana kuna vijana ambao huko nyuma wangeweza kuingia vyuo lakini mwaka wa jana ikashindikana-sasa mtu kama huyo akipata chuo cha nje kuna tatizo gani? Issue hapa ni kuwa kwa wale wenye uwezo kwao watasonga mbele hadi degree kwa wale wenye uwezo hafifu (wa pesa) ndio ndoto inaingia shimoni inabidi waangalie njia mbadala. Na aliyekwenda akirudi na degree yake kuna wa kumkataa?
Nakubaliana na wewe kuhusu quality ya elimu ya kwamba wazazi wapeleke watoto wao kwenye vyuo ambavyo quality ya elimu ni nzuri. Na kwa sasa kuna mashirika 2-3 hapa Tanzania ambayo yamebobea kwenye hili-wanajua vyuo vya China na India vinavyotoa elimu nzuri na mazingira ya huko. Hivyo ni vizuri kupitia kwa hawa ambao watakuhakikishia mzazi kuhusu quality na gharama ambazo zinahusika. Mwenye ufaulu hafifu kama atapata chuo kizuri sioni tatizo kama serikali inamawazo mengine basi watoe sera na miongozo kuhusu hili jambo.
 
Hili nina ushahidi nalo, baada ya mama ndalichako kuja na chujio kuwa form six ni lazima uwe na angalau two, kuna watu wameenda nje ya nchi na three na four zao kwenda kusoma degree ...
Mkuu naona hapa unatuingiza chaka. Pitia tena vigezo vilivyotolewa na TCU, ili ufikiriwe udahili baada ya F6 unatakiwa uwe na point 4 kwenye masomo husika mawili. Hivyo kuna wenye div 3 ambao wanavigezo hivyo.
Kwenda nje ya nchi kama umepata chuo kizuri sioni tatizo na ndio maana wakirudi vyeti vyao inabidi vihakikiwe na TCU kama wanataka ajira kwa mfano serikalini.
 
F
Fafanua zaidi una maana elimu ya iNDIA na China iko chini kuliko ya kwetu? au Unalinganisha na nchi gani?
Tukubali kwamba wengi wanakwenda kusoma nje kwa matarajio ya kurudi nchini au kwingine kupata kazi. Hakuna anayetegemea kupata kazi India au China. Ndo maana kuna pendekezo, waongozwe na serikali. Vijana hawa wataponzeka na wengine ndo hao waliochakachua vyeti na kwa kuogopa screening ya TCU, wanaingia India na China. Huko ni biashara. Baadhi ya vyuo ni vya kiwango cha chini sana! sasa hivi kila cheti cha nje lazima kithibitishwe na TCU.

Hakika kama mfumo huu wa utawala hautavurugwa, wazazi watawaponza vijana. anayeshindwa arudie au apitie mfumo mbadala badala ya kumwaga pesa kwenye vyuo vya ajabu tuu.
 
Kuna wimbi la kupeleka vijana kusoma digrii India na China baada ya form 4 na 6 kwa ufaulu hafifu! Hili ni wimbi jipya lililoanzia Dar. Tukio hili la vyeti feki, liwe fundisho kubwa kabisa kwa wazazi tulio na ’nyodo’ Tumekuwa wataalamu wa elimu ktk familia kuliko hata walioko wizarani. Tunawatafutia watoto wetu shortcuts za elimu ya India na China bila kuangalia siku zijazo itakuwaje.

Kijana anamaliza form 4 au form 6 kwa ufaulu hafifu, mzazi anampeleka kusoma digrii India na China kwa kisingizio cha eti wengine wameweza, bila kujali aina ya elimu inayotolewa india na china kwa wageni. Tunawaponza vijana wetu kwa mazoea ya shórtcuts ambazo huenda wazazi pia walipitia.

Baada ya vyeti feki, tusiwaponze watoto wetu.
Tofauti cheti feki na ufaulu hafifu
 
wasi wasi upo wapi wakati mtu yoyote atakaefanya kazi taasisi yoyote serikalini ni lazima cheti chake kifanyie verification akiwa amesoma nje ya nchi.
maana yake ni kuwa ukisoma nje ya nchi ni lazima upeleke cheti chako TCU wakakihakiki kama ni kweli ulisoma chuo na kama hicho chuo kinajulikana na kama hicho kina hadhi ya kutosha.
 
Mkuu uko sahihi, kwa hili pia nimeshuhudia mwenyewe, na kwa nchi yetu wanafunzi wengi wa namna hiyo niliowashuhudia mimi wanatoka Tanzania Visiwani. Pia Malaysia nayo ni nchi wanakimbilia watu wengi wenye ufaulu hafifu.

Kwa namna nyingine pia Wizara ya Elimu imehusika kupeleka wanafunzi nchi hizo ulizotaja kusoma digrii (master) ambazo hawana sifa za kusoma. Niliwahi kushuhudia mwalimu wa Biology na mwingine wa Chemistry wameenda kusoma masters za Engineering kupitia wizara ya Elimu ili hali walihitajika watu wenye background ya engineering.
 
By the way mleta maada rudi kwanza fanya research ya kutosha ikisha njoo utuandikiePost ya maana kidogo.
Samahani sana kwangu mimi hii post naitafsiri kuwa kama kidogo una wivu fulani hivi. Na vile vile hujui huko Kwa wahindi na wa china wanatoa Elimu vipi.
Kwahiyo futa hii post ukafanye research ikisha njoo uandike tena
 
Mkuu uko sahihi, kwa hili pia nimeshuhudia mwenyewe, na kwa nchi yetu wanafunzi wengi wa namna hiyo niliowashuhudia mimi wanatoka Tanzania Visiwani. Pia Malaysia nayo ni nchi wanakimbilia watu wengi wenye ufaulu hafifu.

Kwa namna nyingine pia Wizara ya Elimu imehusika kupeleka wanafunzi nchi hizo ulizotaja kusoma digrii (master) ambazo hawana sifa za kusoma. Niliwahi kushuhudia mwalimu wa Biology na mwingine wa Chemistry wameenda kusoma masters za Engineering kupitia wizara ya Elimu ili hali walihitajika watu wenye background ya engineering.
Hata UK wanakwenda kusoma tena vyuo kama Warwick University na vyenginevyo huku form 6 wana "0"
vyuo vya nje sio kama vya tanzania ukifeli na maisha yako basi, wenzetu wana options tofauti.
ukienda UK, US, India China, Japan, Korea au huko Malaysia hata kama una ufaulu hafifu bado unaweza kusoma kwasbabu kuna options.
kabla ya kuanza degree unafanya Pre-University. na hio Pre university inategemea na course gani unataka. Kwahiyo msikurupuke tu na kulalamikia wenzenu wanapotafuta sehemu nyenginezo ambapo options zipo.
ikisha boss ukiwa na Degree ya chemistry unaweza kusoma engineering mfano tu kama chemical engineering au any engineering ambayo imo katika area ya chemistry.
hata yule mwenye degree ya biology anaweza kusoma master ya bio engineering au anything related with biology.
 
Kuna wimbi la kupeleka vijana kusoma digrii India na China baada ya form 4 na 6 kwa ufaulu hafifu! Hili ni wimbi jipya lililoanzia Dar. Tukio hili la vyeti feki, liwe fundisho kubwa kabisa kwa wazazi tulio na ’nyodo’ Tumekuwa wataalamu wa elimu ktk familia kuliko hata walioko wizarani. Tunawatafutia watoto wetu shortcuts za elimu ya India na China bila kuangalia siku zijazo itakuwaje.

Kijana anamaliza form 4 au form 6 kwa ufaulu hafifu, mzazi anampeleka kusoma digrii India na China kwa kisingizio cha eti wengine wameweza, bila kujali aina ya elimu inayotolewa india na china kwa wageni. Tunawaponza vijana wetu kwa mazoea ya shórtcuts ambazo huenda wazazi pia walipitia.

Baada ya vyeti feki, tusiwaponze watoto wetu.
Kwani wakienda India, China, USA au UK wanaenda soma PCM au PCB? Hujui kuwa elimu ya chuo kikuu almost it has nothing to do with hizo combination zenu za firm six?
 
Hata UK wanakwenda kusoma tena vyuo kama Warwick University na vyenginevyo huku form 6 wana "0"
vyuo vya nje sio kama vya tanzania ukifeli na maisha yako basi, wenzetu wana options tofauti.
ukienda UK, US, India China, Japan, Korea au huko Malaysia hata kama una ufaulu hafifu bado unaweza kusoma kwasbabu kuna options.
kabla ya kuanza degree unafanya Pre-University. na hio Pre university inategemea na course gani unataka. Kwahiyo msikurupuke tu na kulalamikia wenzenu wanapotafuta sehemu nyenginezo ambapo options zipo.
ikisha boss ukiwa na Degree ya chemistry unaweza kusoma engineering mfano tu kama chemical engineering au any engineering ambayo imo katika area ya chemistry.
hata yule mwenye degree ya biology anaweza kusoma master ya bio engineering au anything related with biology.
Biology inaendana na Petroleum Engineering (Reservoir Engineering)?
 
Hili nina ushahidi nalo, baada ya mama ndalichako kuja na chujio kuwa form six ni lazima uwe na angalau two, kuna watu wameenda nje ya nchi na three na four zao kwenda kusoma degree ...

Wapi alisema angalau uwe na two? TCU wanataka D mbili.
 
Hili ni la kweli kabisa,mtoto kashindwa kupata credit za kumpeleka form five halafu wazazi wake wanampeleka India akasome Degree kwa miaka minne. Mwaka mmoja pre entry,miaka mitatu anasoma degree.
 
Hili nina ushahidi nalo, baada ya mama ndalichako kuja na chujio kuwa form six ni lazima uwe na angalau two, kuna watu wameenda nje ya nchi na three na four zao kwenda kusoma degree ...
Wewe muongo bwana. Nani alikwambia division three si qualification ya kwenda chuo kikuu. Ninyi vijana acheni kupotosha mambo aaaah, hadi mnakera. Kama hauna taarifa kamili usiandike hapa.
 
Back
Top Bottom