Serikali wacha kuchezea pesa zetu za pensheni

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Juzi nilimsikia kiongozi mmoja akiongelea swala la hali mbaya iliokuwa nayo Televisheni ya Taifa (TBC) na kusema kwamba inahitaji kiasi cha shilingi bilioni zipatazo 18 ili iweze kuweka mambo yake sawa, kiongozi huyo alidai kwamba wapo kwenye mazungumzo na mashirika ya pensheni waweze kukopa pesa kwa ajili ya kuinasua TBC.

Hii si mara ya kwanza kwa serikali kutolea macho pesa zetu za mafao ya uzeeni. Tukumbuke kwamba PSPF wanaidai pesa nyingi serikali kutokana na mafao ambayo PSPF iliwalipa watumishiwa serikali ambao hawakuwahi kuchangia kwenye mfuko huo. Pia kuna pesa ambazo mfuko mmoja wa pensheni (Kati ya NSSF na PPF) wanaidai bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) ambayo hadi sasa ina hali tete kutokana na wanafunzi waliosomeshwa kutoanza kulipa mikopo yao. Pia kuna majengo ya Mabibo hostel, Daraja la kigamboni linakuja, Chuo kikuu cha UDOM nk ambazo pesa zinatoka kwenye michango yetu ya mafao ya uzeeni.

Nimeingiwa na hofu sana na halii pengine na wenzangu wanaochangia kama mimi ni wakati muafaka kuanza kuitolea macho serikali iache mara moja kuchezea pesa zetu kwakuwa sisi wafanyakazi especially ndugu zangu babyboomers tulio kwenye 30's and 20's ambao tutastaafu kwa mkupuo kipindi kikifika.Ikiwa sisi tunakatwa kodi ambayo ni kubwa kwenye mishahara sasa iweje tena wakachukue na savings zetu za uzeeni?

Serikali acha mara moja hii tabia!
 
Back
Top Bottom