Serikali: Vigogo waligawiwa viwanja Gezaulole kwasababu wana uwezo wa kujenga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali: Vigogo waligawiwa viwanja Gezaulole kwasababu wana uwezo wa kujenga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Aug 7, 2012.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Serikali imesema Bungeni leo kwamba mojawapo ya vigezo vilivyotumika kuwagawia vigogo viwanja vya eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni ni pamoja na uwezo wa waombaji kuendeleza eneo husika.

  Waziri mhusika amesema kwamba Manispaa ya Temeke ilipokea maombi 16,000 lakini viwanja vilivyokuwepo ni 1,800 tu.

  Ameendelea kusema kwamba vigogo nao ni wananchi na wana haki ya kumilikishwa ardhi
   
 2. d

  decruca JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  rubish!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wamepewa tu hakuna lolote!!
   
 4. m

  manucho JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ok, kama suala ndiyo hilo wangepewa tu hakuna haja ya kutangaza na form zingekuwa sawa na idadi ya viwanja, ya nini wanatapeli watu wanunue form wakati idadi ya viwanja ni vichache.

  Utapeli tu, serikali tapeli iliyoshindwa kazi inakufa
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo vigogo peke yao ndio wenye uwezo wa kuendeleza Gezaulole?
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndo maana yake. Mkisikia viwanja vipya vinatangazwa wala msisogeze pua, ni kwa wenye uwezo tu, yaani watumishi wa serikali
   
 7. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sasa kwa nini waliuzia walala hoi form? ndio wizi kwa masikini
   
 8. m

  mob JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  ina maana sie tunatakiwa kwenda mwabepande,kimara ,tabat liwiti,msakauzi lakini kwenye vilivyopimwa ni vyao sio.ok polepole tutafika
   
 9. m

  markj JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kama ndo ivyo! basi watuamishe hii nchi! wabaki wao waijenge kama sisi hatuna uwezo wakujenga! kwanza hata ivyo viwanja wamegaiana tu! hakuna aliyenunua hapo! sasa kama wanauwezo mbona wanapenda vya bure! wasilete zao! mbona MABWEPANDE hawagaiani wanagaina sehemu zingine, yani hawana hata aibu hawa jamaa, badala yakuwapa walalahoi angalau hata kuwapoza na madudu yao wanayo tufanyia! sasa siwangegawa viwanja wakasema hivi ni kwa ajili ya walimu na mdr tu! ndo waombe! afu wangegawa eneo lengine kwaajili ya watu wote! MASKI WAO,UPANGA WAO,OYSTABAY WAO,SIJUI AREA D WAO!KISASA WAO!RASKAZONE WAO,KICHANGANI WAO! BADO NA HUKU TENA WANATAKA WAO! ila nadhani mwisho wa siku JEHANAMU PIA ITAKUWA WAO.
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono uwapa viwanja wenye uwezo, kwa sababu haimake sense kumpa kiwanja mtu ambaye hawezi kujenga katika eneo ambalo limedhamiriwa kufanywa mji, kama ndio hivyo wangewaachia tu walewale traditional owners. tatizo ni pale inapoaminika kuwa mwenye uwezo ni kigogo tu! kwamba uwezo wa mtu unajulikana kutoka na sirname yake!!! Kama wako serious wangeomba kuonyesha uthiitisho wa uwezo wa kujenga , sio kugawa viwanja according to sirname na kusema hao ndio wenye uwezo!!!
  Wamekusanya almost sh. milion 500 kimagumashi kwa kugawa form 16000 kwa sh. 30,000 wakati kuna viwanya less than 2000.
   
 11. e

  elly1978 Senior Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii nchi ni yakuichoma moto, ingekuwa ni mtu, dawa ni kung'oa meno yote na kucha bila ganzi, pambafu
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,535
  Likes Received: 81,957
  Trophy Points: 280
  Sera mpya ya magamba...Viwanja vya ujenzi kutolewa kwa wale wenye uwezo wa kujenga tu (mafisadi) na siyo walalahoi (makapuku)...Unajuaje huyu ana uwezo wa kujenga na yule hana wakati walichowakilisha ni form tu ambayo haionyeshi vipato vyao!?

   
 13. Small Boy

  Small Boy Senior Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtanzania mimi ni lini na mimi nitapewa ardhi katika nchi yangu?
  Kwanza hao vigogo ndio waliochangia mimi kuwa maskini, na ndio wenye uwezo wa kujenga. mimi uwezo nitapata lini?
  2015 CCM Must go.......
   
 14. S

  Shoboga Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Haya mambo yananijengea roho ya ubabe na uhasama... niliomba kiwanja wamelamba 30,000/= yangu ... kinaniuma sana... kwa jina langu tu walijua mimi ni mlala hoi sitaweza kujenga... before I change my name I will see that something happens!!
   
 15. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tulipigania ardhi isiwe mojawapo ya items za EAC, tukaungana na viongozi wetu kupaza sauti na kutia msimamo, tukaonekana wazalendo. Kumbe tulikuwa tunatumika kuwahakikishia viongozi wetu uhuru na uwezo wa kupora ardhi yetu kama viongozi wa Kenya walivyopora ardhi ya umma miaka ya nyuma. Hatimaye kuhusu ardhi, Tanzania haitaweza kujitofautisha na Kenya
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,080
  Likes Received: 7,306
  Trophy Points: 280
  Serikali inarudisha maendeleo ya nchi nyuma bila kujijua.

  Kumpa Kiwanja mtu ambae ana majumba Chung nzima ni kutoitendea haki eneo husika.
  Wengi wa vigogo hawa wananunua hivi viwanja kama kuwekeza tu kwa ajili ya watoto wao hapo baadae kwani wao tayari washajitosheleza.
  Ndio kusema kua mpaka kiwanja hicho kije kujengwa basi hesabu kuanzia miaka 10-20 ijayo. Kwamba kwa sasa kitabaki Pori tu, hivyo huduma muhimu sahau kabisa.

  Aina ya pili ya wanunuzi vigogo ni wale reseller. Hawa wanajipa moyo kua ardhi ni asset ambayo ina appreciate in value so watakuja kuuza miaka ijayo kwa bei kubwa.
  Wengi wao hawa wapo Ardhi na hata Manispaa kwenyewe.
  Kundi hili pia linajumuisha Wanasiasa mbalimbali.

  Pita Mtoni Kijichi, Kibada, Gezaulole, Mwanagati, nk. Miaka na Miaka Nyumba ni chache lakini kila kiwanja kina mtu.
  Huduma muhimu ziko mbali kwani wa kuhudumiwa ni wachache.

  Sheria ya kunyang'anya kwa ambae hajajenga haifanyi kazi. Mwanagati watu wana viwanja karibu mwaka wa kumi sasa.

  Kibada nyumba ni za kuhesabu, labda quality ya hizo nyumba ndio inalibeba eneo.

  Imefika wakati sasa serikali iangalie hizi sababu nazo. Bora kumpa maskini ambae hana kiwanja akajenga chap, kuliko Tajiri ambae anaenda kujilimbukizia tu kwa ajili ya miaka ijayo.
   
 17. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kuna mwenye list ya hayo majina 1800 a'post' humu?
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo walioomba wot hohehahe hawana uwezo wa kujenga?
  kila mara wanachukua wao washajenga? mbona viwanja kibao vipo wazi huko kigamboni?
  halafu majibu ya dharau namna hiyo maana yake nini? au wamejisahau eeeh? dawa yao kuwaondoa magamba 2015 ndo watakuwa na adabu
   
 19. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kumbe nimejua janja ya hii serikali mnawapora walalahoi ardhi yao kwa kisingizio cha kupima,halafu
  mnapeana viwanja wenyewe na kuwanyima walalahoi waliokuwa wanaishi hapo,sasa waende wapi?
  Kwa mtindo huu nawasapoti wananchi wa Kinyerezi kuiburuza manispaa ya Ilala mahakamani na
  kuzuia miradi yao ya kitapeli,Wanakinyerezi kama kuna mmoja wenu humu waambie na wenzio
  kazeni buti mpaka kieleweke.
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nimewahi omba na sijawahi pata
   
Loading...