Serikali: Usipende kuahidi vitu unavyojua fika hutavifanya

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,581
11,658
Usipende kuahidi vitu unavyojua fika hutavifanya. Kama unajua huna nia ya kutekeleza unachoahidi jifunze kuwa jasiri na kusema hapana mapema. Wakati mwingine kupunguza matarajio na watu kwako ni busara kwa sababu inakupa fursa ya kuzidi matarajio hayo.

Usiwe mwepesi kusema mambo mengi matamu kusikika wakati unajua lengo ni kuwafurahisha watu kwa kuwaambia unachohisi wanakitarajia kwako.

Huna sababu yoyote (na kwa kweli hulazimiki) kupandisha matumaini ya mtu hali ukijua utaishia kumkatisha tamaa baadae kwa lugha rafiki. Jiamini na kuwa mkweli mapema.

Ukweli ni kwamba wakati mwingine watu wanataka kusikia hapana kwako. Iseme mapema. Unaposema ndiyo wanayojua hujaifikiria vizuri na hutaitekeleza wanajua wewe ni mtu usiyeaminika.

*********
Kwa upande mwingine, ni vizuri kuwaamini watu lakini usiamini watu kupita kiasi. Usipoamini watu kuna vingi hutavifanya. Lakini ukiamini sana ahadi unazosikia utakatishwa tamaa baadae.

Amini watu ukijua wengi husema wasichomaanisha. Jifunze kusikiliza katikati ya ahadi. Mtu anaposema, 'ninakutegemea sana,' 'ninataka tufanye hii kazi pamoja,' 'bila wewe hii kazi haitakwenda', wakati mwingine anafikiri ndicho unachotaka kukisikia kwa wakati huo. Usitarajie vingi sana kwa watu wepesi kuahidi.

mr mkiki
 
Nitajitolewa mwili wangu iwe sadaka katika kupigania wanyonge , nitahakikisha hakuna mtoto wa masikini anayekosa mkopo .
 
Kuanzia kesho hakuna kusafirisha magwangala nje ya nchi!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom