Serikali turekebisiheni Sheria ya Usajili wa Blogs vijana tujiajiri

Wakati vijana tunajitahidi kupambana na umasikini serikali nayo inazidi kupambana vijana tusitoke kwenye umasikini,

Mimi ninataka kufungua blog ya kuwa natangaza mambo mengi ya urembo utanashati nk lakini nashangaa kumiliki blogu na kuisajili hapa nchini ni gharama kubwa mpk kufikia milioni moja.

Hii yote ni juhudi ya serikali kuhakikisha vijana tunakufa maskini, naomba serikali ituonee huruma basi tufanyieeni sisi ambao ndio tunaanza kumiliki blogi hata iwe ada elfu thelasini kwa mwaka.

Au basi kama ishu ni kukontroo maudhui basi usajili uwe bure, tafadhali tunawaomba ivi hali ni mvaya vijana tunataka kujikomboa lakini sera za serikali zinaturudisha kwenye umasikini na utegemezi

Tusaidieni jamani vijana tutakimbilia wapi sasa😥
Nyie c ndiyo mnaosaidia kufanikisha wizi wa kura?

Mi-5 tena!
 
Back
Top Bottom