SERIKALI TUPIENI JICHO MWEKEZAJI WA KIBENA TEA ESTATE

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
14,648
2,000
Wapendwa sana wana JF,Shalom....!!!!,Bila kupoteza muda niende kwenye mada moja kwa moja.Ipo hivi Mwezi huu Nilikuwa Kibena-Njombe kumsalimia ndugu yangu anayefanya kazi ktk Kampuni ya chai ya Kibena iliyopo mkoani Njombe (Kampuni hii kwa sasa Inamilikiwa na Mwekezaji kutoka nchini Kenya ajulikanaye km DL Group limited,ambaye anamiliki pia mashamba ya chai ya Luponde na Ikanga ).Huyu ndugu yangu yupo section ya Kiwanda (Factory).
Kilichonisibu hadi kuja hapa ni kutokana na hali ngumu anayopitia ndugu yangu hapo kazini,na baadaye nikaamua kufanya Uchunguzi kwa Wafanyakazi wengine, kwasababu Ndugu yangu huyo anaishi ndani ya Eneo la Kampuni hivyo ikawa rahisi kuona Nini kinafanyika.Katika maelezo niliyoyapata kutoka kwa ndugu yangu huyo na wafanyakazi wengine,nimeelezwa matatizo yafuatayo;

1.Ucheleweshwaji wa mishahara kwa Wafanyakazi; Unaambiwa mishahara inachelewa Sana kutoka,huu mwezi wa Oktoba ndio wanapokea Mshahara wa mwezi wa tisa.Halafu hakuna tarehe maalumu ya kupokea mishahara hiyo.Wafanyakazi ukiwatazama tu usoni unaona kabisa ni watu wasio na furaha.
2.Michango ya wafanyakazi kwaajili ya pension kutopelekwa NSSF.Ili Hali wao wanakatwa kwenye mishahara yao, Viongozi wao wa vyama vya Wafanyakazi wakijaribu kufuatilia wanaishia kupewa vitisho na Mwekezaji, Matharani yupo aliyeandikiwa barua ya kusimamishwa kazi kwasababu ya kufuatilia jambo hili.
3.Huduma duni shambani kwenye zao la chai; Unaambiwa huyu mwekezaji tangu aweke mbolea mwaka 2018, wakati anapokea Kampuni hii toka Kampuni iliyokuwepo ya Rift valley, hajawahi weka mbolea tena,hali hii imesababisha kushuka kwa uzalishaji wa chai kwa kiwango cha kutisha Sana.Kutokana na kushuka kwa uzalishaji kumesababisha wafanyakazi kufanya kazi hata zile zisizo ktk mikataba yao, Matharani mdada mmoja nilikuta analalamika kuwa aliajiriwa kwa kazi ya kiwandani lkn ajabu anaambiwa aende kupakia magogo ya Kuni.
4.Uvunaji wa miti bila kuipanda;Huyu Mkenya ana kasi kubwa Sana ya kuvuna miti na kisha kupasua mbao pasipo kuipanda mingine.Kutokana na matatizo hayo na mengine mengi, Wafanyakazi hao wamekuwa wakidai haki zao bila mafanikio,Jamaa waliniambia kuwa waliwahi kugoma lkn bila mafanikio,nilipowauliza je Uongozi wa Mkoa,na Wilaya Wana taarifa hizo??,Jamaa waliniambia kuwa walishawapelekea taarifa kuhusu kadhia hii lkn wapo kimya,inasemekana kuwa huyu mwekezaji anatoa Sana mlungula kuwatuliza viongozi hao ili wasimfuatilie.

Binafsi nikajiuliza hivi Bodi ya Chai Tanzania, inafanya kazi gani?. Kimsingi Bodi ya chai Tanzania ndio chombo chenye dhamana ya kusimamia uzalishaji wa chai na biashara nzima ya chai,na Kampuni lazima ipeleke Ripoti ya uzalishaji kwenye bodi hii, sasa km uzalishaji umeshuka,wao wamechukua hatua gani kunusuru hali hii?.Pia ishu ya maslahi ya Wafanyakazi mamlaka husika zimechukua hatua gani?.Zao la chai hutumia nishati ya kuni ktk ukaushaji wake,sasa ikiwa Mwekezaji huyu ataendelea kuteketeza miti bila kupanda halafu aje aondoke akiacha miti ikiwa imeisha tutafanyaje?.

USHAURI WANGU:
Naiomba Serikali ifanye hima kuchunguza tuhuma hizi dhidi ya mwekezaji huyu.Nilivyomsoma huyu jamaa ni kwamba yeye hataki kuongeza gharama zozote kwaajili ya uendelezaji wa zao la chai Bali ni kuvuna pesa tu kutoka kwenye zao la chai, yaani Anataka kuvuna pesa nyingi kwa uwekezaji kiduchu,ndio kusema anabana Sana matumizi kiasi kwamba hata miundo mbinu inayoharibika wala haitengenezi.Ile Kibena tea Estate iliyokuwa ikisifika kwa ubora imepotea ubora kabisa, Kwani inasemekana kuna mwaka iliwahi kupewa tuzo kidunia.Sasa basi Serikali ifanye Hivi;
a.Ifanye Uchunguzi wa kimya kimya,hata kwa kutumia kitengo chake Cha TISS.
b.Iunde Tume ya kuchunguza malalamiko ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho na kuhakikisha kuwa wanapewa stahiki zao.
c.Ufanyike utaratibu wa kuwaita/kuwaalika wawekezaji wengine kutoka mataifa mbalimbali na washindanishwe
View attachment 1983497
Sehemu ya shamba la chai Kibena -Njombe.
 

Attachments

  • IMG_20210908_125510_344.jpg
    File size
    116 KB
    Views
    0

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom