Serikali tuonee huruma, mwajiri wetu wa zamani hakupeleka mafao yetu kwa mujibu wa Sheria

Mongasa

Member
Jul 3, 2019
68
125
Natanguliza zangu nyingi shukrani kwako Mh Rais kwa mengi unayofanya kwa ajili ya Wananchi wako, pamoja na hayo kuna mambo mengi aidha watendaji wako hawakuambii au wao ni sehemu ya uozo huo.

Yapata miaka zaidi ya miwili tunahangaikia kufuatilia pesa za michango yetu ya hifadhi ya jamii ambayo kimsingi ni kuwa mwajiri wetu wa zamani New Habari 2006 Ltd hajawahi kupeleka, tumefuata taratibu mbalimbali lakini inaonekana hili suala ni gumu sana.

Kwa mamlaka yako tunaomba umwamrishe mmiliki wa Kampuni tajwa bwana Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Naibu Waziri wa Kilimo wafuate Sheria na kupeleka michango ya wafanyakazi.

Nikutakie kazi njema iliyotukuka na kumbuka kutupia jicho hapo NSSF
 
Mongasa

Member
Jul 3, 2019
68
125
Nakushauri onana na waziri mwenye dhamana atakusaidia

Asante kwa ushauri lakini kwa Waziri tulishafika hakuna kinachofanyika nguvu ya Waziri imekua ndogo kwa hao wakubwa, tunaumia zaidi kuona mmiliki anaweza kutoa msaada hadi Bilioni moja lakini pesa ya michango yetu hana nayo muda, kwakua Rais hao watu anawamudu atuombee wapeleke michango ya Wafanyakazi ndo takwa la kisheria
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,233
2,000

TOMNOTKAT

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
827
1,000
Asante kwa ushauri lakini kwa Waziri tulishafika hakuna kinachofanyika nguvu ya Waziri imekua ndogo kwa hao wakubwa, tunaumia zaidi kuona mmiliki anaweza kutoa msaada hadi Bilioni moja lakini pesa ya michango yetu hana nayo muda, kwakua Rais hao watu anawamudu atuombee wapeleke michango ya Wafanyakazi ndo takwa la kisheria
Mnadai shs ngapi jumla? Ikibidi Tuwasaidie pakuzinyofolea?
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,277
2,000
Sasa ile misaada yake wakati wa COVID-19 angeenda kuwalipa watu stahiki zao.
Upande mwingine kuna kitu hakipo sawa aidha kwenu au kwa serikali sababu mwajiri hasipopeleka michango ya mifuko ya jamii ya watumishi wake hilo ni kosa kisheria na inabidi apelekwe kwa Pilato, iweje suala hili lishughulikiwe kama hiyari ya muajiri?

Huo mfuko wenu ni wazembe na nyie pia wazembe sababu mlikuwa hamuendi kufuatilia salio la michango yenu kama inapelekwa sawasawa.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,656
2,000
Natanguliza zangu nyingi shukrani kwako Mh Rais kwa mengi unayofanya kwa ajili ya Wananchi wako, pamoja na hayo kuna mambo mengi aidha watendaji wako hawakuambii au wao ni sehemu ya uozo huo.

Yapata miaka zaidi ya miwili tunahangaikia kufuatilia pesa za michango yetu ya hifadhi ya jamii ambayo kimsingi ni kuwa mwajiri wetu wa zamani New Habari 2006 Ltd hajawahi kupeleka, tumefuata taratibu mbalimbali lakini inaonekana hili suala ni gumu sana.

Kwa mamlaka yako tunaomba umwamrishe mmiliki wa Kampuni tajwa bwana Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Naibu Waziri wa Kilimo wafuate Sheria na kupeleka michango ya wafanyakazi.

Nikutakie kazi njema iliyotukuka na kumbuka kutupia jicho hapo NSSF
Tukuone kwanza jinsi ulivyovaa, cap unayo? Shati unalo? Hata kama halitafanana na la Polepole angalau ranging ziwe, kupauka si hoja.
 
Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,436
2,000
Natanguliza zangu nyingi shukrani kwako Mh Rais kwa mengi unayofanya kwa ajili ya Wananchi wako, pamoja na hayo kuna mambo mengi aidha watendaji wako hawakuambii au wao ni sehemu ya uozo huo.

Yapata miaka zaidi ya miwili tunahangaikia kufuatilia pesa za michango yetu ya hifadhi ya jamii ambayo kimsingi ni kuwa mwajiri wetu wa zamani New Habari 2006 Ltd hajawahi kupeleka, tumefuata taratibu mbalimbali lakini inaonekana hili suala ni gumu sana.

Kwa mamlaka yako tunaomba umwamrishe mmiliki wa Kampuni tajwa bwana Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Naibu Waziri wa Kilimo wafuate Sheria na kupeleka michango ya wafanyakazi.

Nikutakie kazi njema iliyotukuka na kumbuka kutupia jicho hapo NSSF
Tuko busy na Lissu kwanza mpaka tuhakikishe hagombei. Shauri yenu na Bwege wenu.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,834
2,000
Nendeni mahakamani washitakini mwajili na nssf kwenye marekebisho ya mwisho ya sheria za mafao nssf ndio anawajibika kama mwajili hakupeleka mafao na ssra kabla haijavunjwa
 
wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,144
2,000
Rostam huyu huyu..... Kweli CCM kichaka Cha wahalifu..

Hapo mwajiri anatakiwa ashitakiwe na shirika la hifadhi ya jamii... Huu Ni wizi... Kuiba mafao ya wafanyakazi na kuibia serikali makato yaliyopaswa kuhifadhiwa...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom