Serikali tunaomba ufafanuzi bei elekezi ya Sukari imebadilika?

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734
Wakuu!

Kupitia taarifa ya habari ITV saa 2 nimeona na kusikia kutokea Mwanza juu ya zile tani 500 zilizopelekwa huko kutokea kiwanda cha kagera ili kuokoa uhaba wa sukari katika jiji hilo, cha kusikitisha imetangazwa kuwa wananchi walinunua mfuko wa Kg 50 kwa bei elekezi ya Tshs. 98,000/= kwa mfuko hii ikimaanisha wamenunua bei ya jumla kg 1 kwa tshs.1,960/=.

Nimeweka andiko hili ili tupate ufafanuzi kwani bei elekezi ya lejaleja kwa mlaji Serikali ilitamka kuwa ni Tshs. 1,800/= sasa hii bei elekezi ya Kg 1 kwa Tshs. 1,960/= kwa muuzaji wa jumla imetokea wapi?
 
Mm bado sijaelewa kitu hivi mkuu hakufanya utafiti wabei ya sukari au alitaka kujidhalilisha
 
Hata hivyo wamekurupuka umeme ukashuka bei ,
Bei ya umeme imeshuka kwa wasiojua kuutumia umeme lakini kwa wale wanaojua kuutumia umeme bei iko palepale, maana ukinunua umeme wa Tsh. 40,000/= unapata unity 112.3 wakikata na kodi yao. hapo awali nilikuwa nikinunua umeme wa 40,000/- bila kodi na service charge nilikuwa napata 146.3 units sasa hivi 149.3 units, yaani kuongeza unit 3 ndio nijitoe akili kusifia?
 
Mwanzo nilikua na kaakiba ka sukari nilinunua zamani kilo elfu 2, siku zote watu wanapiga kelele humu nikajua ni porojo tu, jana nimeishiwa kwenda dukani kilo 4000 kila duka naloingia, ikabidi nimpigie simu mkuu wa wilaya akaahidi leo wanaenda kuwakamata wafanyabiashara wanaouza zaidi ya sh. 2000 kwa kilo, nasubili jioni nitaenda kucheki tena. Ila nimegundua sio sukari peke yake hadi nyanya sa hivi sado sh 12,000 kutoka sh. 3,000 last month, yani nyanya 3 unapata kwa buku.
 
Bei ya umeme imeshuka kwa wasiojua kuutumia umeme lakini kwa wale wanaojua kuutumia umeme bei iko palepale, maana ukinunua umeme wa Tsh. 40,000/= unapata unity 112.3 wakikata na kodi yao. hapo awali nilikuwa nikinunua umeme wa 40,000/- bila kodi na service charge nilikuwa napata 146.3 units sasa hivi 149.3 units, yaani kuongeza unit 3 ndio nijitoe akili kusifia?
Hata kama ingekuwa unit moja lazima usifie..kumbuka mkono usio na shukrani hukausha Neema zote..

Angalia Mbowe ameshindwa kuwajengea hata ofisi tu. Miaka 20 CHADEMA bado ina ofisi chafu kuliko zote duniani.
 
Hata kama ingekuwa unit moja lazima usifie..kumbuka mkono usio na shukrani hukausha Neema zote..

Angalia Mbowe ameshindwa kuwajengea hata ofisi tu. Miaka 20 chadema bado ina ofisi chafu kuliko zote duniani.
Sasa Mbowe na CHADEMA inaingiaje hapa? ni vema akili zako zikawa hai ndugu kuliko kufikiri kwa kutumia akili za wengine.
 
Utamu unachanganya Watu wengi.
 
Attachments

  • image.png
    98.1 KB · Views: 33
Z
Unazionaje ofisi za chadema pale ufipa??
Zinakuhusuje kwa mfano. Wewe siyo mwanachadema na wala hujaombwa mchango wa ofisi kimbelembele cha nini? Nimekuambia tena nafasi za uteuzi zimesitishwa kwa sasa kwasababu ya ukosefu wa pesa. Na hata akiteua baadae jina lako halitakuwepo kwani hujui kama hujui kuongoza.
Watu wanajadili issue ya sukari wewe unaleta habari za majengo chakavu ya watu ilihali wewe hata kibanda cha nyasi huna. Si aibu hii rais wa malofa!
 
Back
Top Bottom