Serikali tunaomba mtufungulie ile barabara ya Feri kuelekea Ocean Road Hospital

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,397
3,491
Wasaalam wanabodi,

Miaka ya nyuma ile barabara tulikuwa tunaitumia vizuri tu.

Akaja mtu na mawazo yake ya kujiimarishia ulinzi akaamua kuifunga bila taarifa zozote.

Sasa kwa kuwa ni awamu ya sita, tunaomba serikali yetu tukufu chini ya Rais Samia mtufungulie ili tuweze kurahisisha mizunguko yetu kama zamani.

Ahsante sana!!
 
Kuna siku nilikatiza kule enzi za Jiwe, tulirushwa kichura chura kutoka hapa hapa mwanzo feri mpaka huku hospitali ya ocean road.
wale mbwa sitawasahau.
Sie tuliimbishwa nyimbo ya taifa sema jamaa ni mtu wa kigoma alivyotaka kunipigisha sasa push up akajiroga akaniuliza wewe mtu wa wapi nikwambia kigoma akaniuliza tena sehemu gani basi skufanya kosa nikamwambia ni mjukuu wa fulani,mzee ambae ni mwanga mkubwa kigoma

Kilichofata niliambiwa ondoka haraka huruhusiwi kupita maeneo haya nilitoka speed 260
 
Welcome to police state, white house pale USA unatembelea bila shida,Union Building pale PTA unatembelea viunga vyake bila bughudha,awamu ya kwanza mbele ya ikulu yetu ilikua sehemu Safi na salama kupunga hewa, mara walipoingia wapangaji wapya pale kila kitu kikabadilika!,pamoja na ulinzi wote ule..kilichotokea kimetokea!,karibuni huku lingusenguse hatuna high walls wala electric fences
 
Wasaalam wanabodi,

Miaka ya nyuma ile barabara tulikuwa tunaitumia vizuri tu.

Akaja mtu na mawazo yake ya kujiimarishia ulinzi akaamua kuifunga bila taarifa zozote.

Sasa kwa kuwa ni awamu ya sita, tunaomba serikali yetu tukufu chini ya Rais Samia mtufungulie ili tuweze kurahisisha mizunguko yetu kama zamani.

Ahsante sana!!
By the way Ikulu rasmi ya nchi ni Dodoma.
 
Kuna siku nilikatiza kule enzi za Jiwe, tulirushwa kichura chura kutoka hapa hapa mwanzo feri mpaka huku hospitali ya ocean road.
wale mbwa sitawasahau.
Tulisha sema ikulu ya dar iondolewe ilo eneo inazuia ukuaji wa mji hata kujenga gorofa refu wanazuia kwa sababu za kipumbavu za ikulu kuonekana kwa juu
 
NAUNGA MKONO HOJA ! MTU UNASHUKQ KUTOKA KWENYW PANTON NA UNAELEKEA OCEAN ROAD, ZAMANI TULIKUWQ TUNAKATIZA CHAP ; KUJA JIWE NA VIJANA WAKE BALAA. BODABODA 2000 NA SEHEMU UNAIONA. LOL; MAMA @SAMIASULUH UKIPITA JF LIFANYIE KAZI
 
Miye kuna siku ile aliyekuja mfalme wa Moroco nahisi, nilienda kule nyuma nina strees kinama, kuna mtu alinifuata kwa upole na kunambia huruhusiwi kupita huku. Nikamshukuru huyo nikasepa zangu.
 
Uoga tu eti hata picha huruhusiwi, wakati White House watu wanaingia
 
Wasaalam wanabodi,

Miaka ya nyuma ile barabara tulikuwa tunaitumia vizuri tu.

Akaja mtu na mawazo yake ya kujiimarishia ulinzi akaamua kuifunga bila taarifa zozote.

Sasa kwa kuwa ni awamu ya sita, tunaomba serikali yetu tukufu chini ya Rais Samia mtufungulie ili tuweze kurahisisha mizunguko yetu kama zamani.

Ahsante sana!!
Halafu sasa hivi Rais yuko Dodoma.
 
Wakati ikulu za wenzetu ni sehemu ya kutalii na kuwavutia wageni, kwetu ikulu ni strictly prohibited, nenda Kremlin uone watu wakiingia huku na kule kuona historia ya warusi, red square yote mtu unapita na kujipigia picha unavyotaka
 
Miaka iliyopita tulikuwa tunawapokea marais kupitia geti la baharini. Hakukuwa na mbwembwe kama hizi za sasa.

Marais walikuwa ni watu wa kujishusha wanaoingilika tofauti na hawa wanaolindwa mpaka na helikopta juu.
 
Uoga tu eti hata picha huruhusiwi, wakati White House watu wanaingia
Hivi whitehouse unaijua au una ambiwa? Yaani nyinyi vipi! Unalinganisha Tanzania na USA? Unafikiri Whitehouse hailindwi hata kidogo! Ghrama zinazotumika kulinda Whitehouse ni budget ya miaka mingi ya Tanzania. Kuna lindwa na satellite na vifaa vingi advanced! Unaweza ukakuta unapoingia au kupita karibu unachunguzwa hadi ndani ya utumbo wako bila kujielewa! Sasa hayo ndiyo Unalinganisha na kwetu, technology wanayo tumia ni aibu ukijua wanachokufanyia!
 
Tz hamna technology ya kulinda White House?
 
Back
Top Bottom