Serikali tumieni mfano wa shule ya Kisimiri kuleta mabadiliko katika ufaulu

Ni kweli kisimiri inachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu kwa advance...lakini kwa mazingira yale na ufaulu wao wapongezwee tu...masuala ya uchache sidhani...nimesoma pale mazingira ya kisimiri ni magumu sana...ila huyo Kisongo anajitahidi mnooo
Hakuna shule yenye mazingira mazuri kwa upande wa serikali labda kibaha. Unaijua tabora boys? Kiufupi hakuna shule yenye miundo mbinu mizuri kwa upande wa special school. Uzuri wa hizi shule ni kuwa wanafunzi wanajituma na wanajua wamekifata nini.
 
Kama hayo maneno kaongea huyo mwalimu basi amekurupuka au atakua ameongea ili kutaka sifa. Kisimir ni mojawapo ya shule znazochkua wanafunzi wenye division one na mwisho ni point 14 kwa upande wa a level
Ni lini imechaguliwa kuwa shule maalam? Naomba uje na tangazo la serikali.
 
Kisongo ni headmaster mzuri sana...ambaye anashirikiana sana na wanafunzii na matunda yameonekanaa Hongeraa my headmaster...nakumbuka useme wake wa Win with honor and Lose with honor...MUNGU KWANZA KUSOMA SANA!
Hapa sasa serekali wanapaswa kufanya mambo kama haya kama motisha ili shule nyingi za serekali zijitaidi na walimu kuacha uzembe.1.walimu washule hiyo husika kupandishiwa Mara moja mishahara.mbili nyumba na mabweni na madarasa kuongezwa .tatu kutoa Gari mpya kwa shule husika.nakuambia nakumbia Ndalichako Mh na Mama yangu kipenzi mwakani utaniambia matunda utakayopata mama yangu jembe,
 
Azania wamefeli,na vivulana vidogo dogo ambavyo havijakauka shombo ya maziwa.

Sababu kuu ya AZANIA kufeli.

1:-Wanafunzi kujihisi wao ni "watoto wa mjini" ilhali kichwani kumejaa pepcorn.

2:--kuzungukwa na vibinti vibichi vya Jangwani Sec na Zanaki,Shaaban Robert na Tambaza,uzoefu unaonyesha mvulana mmoja wa Azania ana Wasichana/Mzizi mwenziye kila shule tajwa.

3:-Kuendekeza starehe na kila mmoja kujiita diamond platinumz,kutaka kuwa msanii badala ya kusoma,wanataka maisha mteremko.
4-Lishe duni hasa Chips za mafuta ya transformer na maji ya kandoro ,hela yao inayobaki i apokwenda nitakwambia.

5:-Smart Phone/Simu..,Hawa wote wanazo simu za ku slaidi,Wanaweka bundle ,wana download picha za ngono na kutumia a na wazinzi wenzao wa Zanaki etc,wanachat sana watsupp kwenye magroup yasiyo na maana.

6:--Team Kiba/Diamond:-Hawa watoto wa Azania ndio walioanzisha team Diamond/Kiba,mda wote wanashinda insta kufuatilia yakiyojiri na kubishana nani yupo juu kati ya wasanii hao wawili mtu mzima jua unapochangia mjadala wa Diamond na Kiba una urge na watoto wa Azania .

7:-Kushinda kwenye ma -gheto ,hasa maeneo ya Jangwani na Magomeni wakati wazazi wao wapo makazini,huko gheto ndipo wanapopiga 'mitungo' madada zetu wa Jangwani,Zanaki na Shaaban Robert.

8-VILEVI-pombe za Pakiti,Tambuu,Kuberi,Miringi,na Gomba ambazo zinashushwa na Tahmeed pale magomeni,Hawa watoto wanatumia hivyo vyote wakiamini hivyo vilevi vinaongeza nguvu ili wapige madem wengi zaidi of which sina uhakika.

9-BASH--Hawa watoto kila weekend wao ni Bash,hili neno najua ukimwita yule mtoto wa Kisimiri ama Tabora Boys atafikiri ni neno la Chemisty topic ambayo hakusoma lakini kwa Azania ni talk of the day!Wao ni kula bata na tour zisizoisha!

10:--Vitendo vya ngono kwenye hii shule kipindi cha mahafali ni wazi kabisa,mtoto anakunjiwa nyuma ya mlango,chooni,etc.

11:--Waalimu wengi hapa Azania ni ******,am sorry to say so but namsaidia JPM.
Hawa ni wake za wakubwa ambapo waume zao wanapopata nafasi za kuteuliwa ama kuchaguliwa waje Dar basi hakuna namna mume anataka kuja na mkewe,na inatafutwa shule iliyopo jirani,wanajazana hapo Na kupiga soga tu,


Bwana Yesu asifiwe sana!

Jumapili njema,

My take:-

RC Makonda,nakusihi,wajibisha afisa elimu wa kanda ,Mwalimu mkuu,DeD vunja bodi ya Shule.
Amesheni waalimu waliopo hapo.
Umenena sana ila hapa umekosea.ded mgeni.Afisa elimu na mkuu washule hawana kosa kama unakiri walimu ni wake Wa vigogo sasa watawakemeaje wakati wake za wakubwa.sema hivi kwa dar es salamu yote serekali itenge mikoa kama lindi.mtwara.ruvuma.kigoma.simiyu.songwe.nk watumishi wote hasa walimu na Manesi madoctor waamishwe kwa kupangiwa hiyo mikoa asiyetaka aache kazi ili wakajifunze wenzao wanafanyaje kazi katika mazingira magumu.
 
Kisimiri n kama mzumbe wanachukua wanafunzi wenye vipaji kwa iyo no wonder special mwanafunzi sio shule

Mbona mwalimu mkuu anasema hawajawahi kupokea division one ! Wao wanapokea three na chache two
 
Mkubwa kasema dawati likivunjwa, mwalimu atakatwa mshahara.

Acha walimu walinde madawati kisha mengine yatafuata baadae.
 
Mbona mwalimu mkuu anasema hawajawahi kupokea division one ! Wao wanapokea three na chache two
Huyo mwalimu ni muongo na nazani inabd atuombe msamaha kwa kutudanganya. Nazani ameongea hayo maneno akitaka watu wamuonee wivu. Trust me kisimiri ni special na nafahamu kuwa ni special toka mwaka 2009.kuna washkaj zangu walikua na ufaulu mzur tu one ya 11,12 na wa mwisho alikua na 14. Na walichuguliwa hapo.
 
Mkuu jaji mfawidhi umeongea ukweli mtupu kuhusu Azania na shule za town center jijini Dar.
Hata hivyo,mbona sisi tulisoma shule hizo,ujana tumeufanya na masomo tulifaulu?
Mimi nilisoma Tambaza ya akina Puza na mziki wake kuna watu wanaujua humu.
Haya mapenzi ya "Azajangwa" hayajaanza leo.
Mimi nadhani hakuna uwajibikaji wa kielimu darasani kwa hao watoto.
Kama walimu wataingia kufundisha darasani frequently,mwanafunzi akapewa majaribio kila weekend au every after two weeks,wasiofanya majaribio hayo wakafuatiliwa ikiwa ni pamoja na kuita wazazi wao,wanaofeli pia wakafuatiliwa,mtu akaambiwa chini ya wastani huu kwa idadi ya majaribio kadhaa ukifeli basi tafuta shule nyingine ya kwenda au rudia darasa,wakiwa groomed hivyo,huna haja ya kukimbizana nao gheto wala wapi,watatulia wenyewe na kusoma.
Hivyo usimamizi wa hiyo shule kitaaluma kwa sasa ni mbovu.Ndio sababu kuu.
Wakibanwa darasani,hayo mengine yatapotea yenyewe bila kutumia nguvu na hata kama watabaki baadhi wanayafanya,hawatayafanya kwa kiwango cha kuwaathiri kielimu hivyo,maana muda hawatokuwa nao.
Watoto wa siku hizi wa Azania muda wote wako tuition,mtu unajiuliza,darasani hawakai?kwanini?huu uhuru wanatoa wapi?
Nampa Makonda ushauri,ahakikishe anaweka mfumo wa kufuatilia attendance ya walimu na wanafunzi darasani kwenye hizo shule za jijini,kuwe na mfumo wa kufuatilia majaribio kama hiyo shule ya Mwl Kisongo,nawahakikishieni hamtasumbuka na hawa watoto wa mjini,watatulia tulii.
Na mengineyo yataibuka,mtasikia walimu wanaanza kulalamikia uhaba wa test tube maabara,hapo mtajua sasa watoto wanafundishwa.
 
Back
Top Bottom