NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,462
- 17,291
Maji yakimwagika hayazoleki!
Katiba iliyopo mliiona ni mbovu wenyewe mkaanzisha mchakato wa katiba mpya wenyewe!Wala sio Mbowe wala Lisu wala Upinzani nchini!
Kuendelea kutumia jeshi la polisi kuzuia hiki mlichokianzisha wenyewe ni kujiua wenyewe kisiasa na kupoteza uhalali wa serikali yenu wenyewe!kwani upinzani haukuanzisha huu mchakato bali ninyi! Upinzani unaisaidia serikali kutimiza azma ya wananchi kupata katiba mpya itakayosaidia mchakato wa kupata serikali zijazo nchini.
Ili kujifichia aibu fanyeni yafuatayo:-
1. Anzisheni makongamano endelevu ya mapungufu ya katiba iliyopo ili ku spin makongamano ya katiba mpya ya upinzani yanayoendelea ili kuonyesha mna nia ya dhati ya mabadiliko na mkisema katiba iliyopo wananchi hawaijui tena fanyeni hivyo kwa miaka mitano hadi 2025!
2. Anzisheni somo la Katiba kuanzia shule za msingi hadi sekondari na vyuo mkitaka katiba ieleweke kwa wote!!hii ni ku buy time hadi wakati wa uchaguzi ujao.
3. Muanzishe Baraza la mpito la uchaguzi la maridhiano kwa ajili ya uchaguzi ujao huku mkisisitiza muda wa kupitisha katiba mpya hautoshi!!Baraza lihusishe wenyeviti wa siasa woote nchini. Huku mkisisitiza demokrasia itatamalaki na kurejesha asilimia 40 ya wabunge wa upinzani katika uchaguzi ujao 2025.
3. Mwisho kabisa !!Uchaguzi ujao Katiba mpya iwe ndio ajenda na ilani ya chama tawala ili mpate dola tena!mkisha shika dola mtaanza mchakato wa katiba mpya kuipitisha na mapendekezo yake.
Mkifanya hayo mtapona kwa kipindi hiki cha presha hizi za upinzani! Kuliko kutumia Jeshi la Polisi na kuchafua taswira ya nchi yetu kimataifa.
Ni mimi mtia nia wa Urais 2040 kunapo majaaliwa ya Baba Mwenyezi!!!