Serikali, Tume ya Uchaguzi wavutana


Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,865
Likes
738
Points
280
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,865 738 280
 
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

“Haijawahi kutokea hata siku moja kwamba tume imeagizwa na kiongozi yeyote wa juu kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea,”
Dar es Salaam.
Wakati Serikali ikisema Daftari la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kwa ajili ya kura za maoni ya Katiba Mpya, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haina mpango huo kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Badala yake Nec imesema inajiandaa kuboresha daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuingiza wale wote waliotimiza miaka 18 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema jana kwamba itakuwa vigumu kuliboresha daftari hilo kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2014 kwa sababu muda uliobaki ni mfupi na hakuna fedha za kufanya hivyo.
“Muda uliobaki kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni ni mfupi, itakuwa vigumu kwa tume kuliboresha daftari la wapigakura nchi nzima ila tunajiandaa kuliboresha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Jaji Lubuva.Alisema nchi ni kubwa kijiografia kiasi kwamba unahitajika muda mrefu kwa ajili ya kuliboresha daftari hilo na kwa vile zoezi la upigaji kura za maoni litafanyika mwanzoni mwa 2014, tume itakuwa imechelewa kufanya hivyo.
Kauli ya Serikali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alipoulizwa jana mjini Dodoma kuhusu tamko la Jaji Lubuva, alisema msimamo uliotolewa na Waziri Mkuu wiki iliyopita ndio msimamo wa Serikali.
“Serikali tunajiandaa, na wao (NEC) wanajua fedha za mwanzo tumeshapeleka na mchakato umeanza. Wameshakagua mashine zitakazotumika….process (mchakato) hii yote inalenga kura ya maoni,” alisema Lukuvi.
Hata hivyo, Lukuvi alisema inawezekana kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba Katiba Mpya itapatikana Aprili 26, mwaka huu ndiyo inayowachanganya, wanaona muda uliopo ni mfupi lakini hilo ni la Serikali na siyo tume.
Desemba 5, mwaka huu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alivihakikishia vyama vya siasa na Watanzania kwamba Daftari la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kabla ya upigaji kura ya maoni juu ya Katiba Mpya. Hali kadhalika Pinda alisema Serikali itatumia daftari hilo la Nec katika upigaji kura ya maoni ya katiba kwa pande zote za Muungano.
Pinda alitoa kauli hiyo wakati akihitimisha hotuba yake ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 ambapo suala la daftari la wapiga kura lilibua mvutano mkali. Wabunge wa Tanzania Bara walitaka daftari la wapiga kura liboreshwe kwanza, huku wale wa Zanzibar wakitaka wasio na vitambulisho vya ukaazi waruhusiwe kupiga kura kwa kutumia daftari la Nec.Pinda alitoa kauli hiyo wakati akihitimisha hotuba yake ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 ambapo suala la daftari la wapiga kura lilibua mvutano mkali. Wabunge wa Tanzania Bara walitaka daftari la wapiga kura liboreshwe kwanza, huku wale wa Zanzibar wakitaka wasio na vitambulisho vya ukaazi waruhusiwe kupiga kura kwa kutumia daftari la Nec.
“Haijawahi kutokea hata siku moja kwamba tume imeagizwa na kiongozi yeyote wa juu kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea,” alisema.
Alisema tume inafanya kazi zake kwa uhuru lakini kama wananchi wanataka mabadiliko yoyote kwenye Katiba Mpya kuhusu namna ya kupata tume, hilo ni suala la msingi. “Tume iko huru, ila wananchi wanaweza kuamua namna ya kupata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo wanapenda iwe, sisi hatuna kipingamizi,” alisema Jaji Lubuva.
Kauli za wanasiasa
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema kauli ya Nec inaashiria kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilidanganya Bunge na Watanzania wakati wa mjadala wa Muswada wa Kura ya Maoni kuwa daftari litaboreshwa kabla ya upigaji wa kura za maoni. Alisema kauli hiyo inaashiria kwamba wananchi waliopoteza kadi, waliokosa fursa wakati wa uboreshaji mwaka 2010 na waliofikisha umri wa kupiga kura watakoseshwa haki ya kupiga kura kuamua hatima ya nchi yao.
Mnyika alisema Nec imeamua kung’ang’ania daftari lenye kasoro ambalo limekuwa likilalamikiwa tangu mwaka 2010 kwamba linahitaji kuhakikiwa.
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alipotafutwa jana kuzungumzia hilo, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu, kama ilivyokuwa kwa James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

Chanzo Mwananchi
 
 
 
 
 
 
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Messages
3,393
Likes
251
Points
160
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2013
3,393 251 160
sijaona mvutano ulipo ni jambo ambalo lipo wazi kabisa huku ikiwekwa bayana kuwa daftari litaboreshwa kosa liko wapi.
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Messages
3,393
Likes
251
Points
160
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2013
3,393 251 160
tatizo la wandishi wetu hasa hawa wandishi njaa watu wakiwa na mtazamo tofauti wa namna ya kumaliza jambo fulani inakuwa wanavutana kitu ambacho ni kituko kweli.
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
56,884
Likes
52,166
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
56,884 52,166 280
daftari liboreshwe sasa , muda mfupi maana yake nini ? Tunakimbilia nini ?
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
21,535
Likes
16,269
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
21,535 16,269 280
tatizo la wandishi wetu hasa hawa wandishi njaa watu wakiwa na mtazamo tofauti wa namna ya kumaliza jambo fulani inakuwa wanavutana kitu ambacho ni kituko kweli.
Anza kuandika wewe ili tuone tofauti.
 

Forum statistics

Threads 1,263,613
Members 485,990
Posts 30,158,007