Serikali/TRA yazitaka Benki kutopandisha viwango vya tozo/ VAT katika miamala yake

Itafika mda hii nchi mpaka hela unayompa mtoto kwenda kununulia chakula shuleni serikali itaikata kodi. Mpaka hela ya house-girl ya matumizi serikali itataka chake. Mpaka hela ya mkewe kula bata serikali itataka chake. Lakini ukiwa unafanya kazi serikali haipo kukusaidia ukiwa unatoka jasho.

hizo benki tayari zinalipa kodi kwenye mapato wanayopata sasa tena juu ya hio kodi serikali inaongeza nyingine ya ujanja na inategemea kusiwe na muongezeko wa bei. Yani serikali mission yao mwaka huu ni kuuwa sekta binafsi na kuongeza gharama ya maisha TZ.
 
Ila nakumbuka lengo la Serikali ilikua kwamba kinacho kusanywa na bank kama service charge ndicho kilipiwe kodi na bank zenyewe na sio mwananchi kulipishwa liba juu ya service charge kama mabenki yanavyotaka iwe

Ivi watu hamuelewi benki ni biashara na kama biashara yoyote ile kodi ni mojawapo za gharama. Kodi ikiongezeka inamaanisha gharama ya kufanya biashara imeongezeka na ili hiyo biashara ipate faida inahitaji kuongeza bei, gharama na ada za wateja au kutoa huduma ya low quality ili kusawazisha hela wanayotumia kuendesha biashara.
 
Sijaelewa haya maelekezo ya TRA! Ninaamini Tanzania Bankers Association (TBA) watakaa chini na serikali ili kuliweka hilo vizuri.Sioni namna gani utazibebesha benki mzigo huo na hivyo kuwapunguzia mapato yao.Naamini Benki siyo NGOs hivyo wanapaswa kupata faida au kurejesha gharama zao za utoaji huduma kupitia transaction charges!

Hii ni issue ya kibiashara na kwa benki kucharge 18% kama VAT juu ya viwango vya tozo wanazotoa nafikiri ni sahihi na ndivyo inavyostahili kuwa na hapa simaanishi kwamba jambo hili halitakuwa mzigo kwa mtumiaji wa huduma za kibenki! Naamini with time tutazoea na tutasonga mbele!
 
Ila nakumbuka lengo la Serikali ilikua kwamba kinacho kusanywa na bank kama service charge ndicho kilipiwe kodi na bank zenyewe na sio mwananchi kulipishwa liba juu ya service charge kama mabenki yanavyotaka iwe

Lazima uelewe sababu za Benki kukucharge service charge na pia uelewe namna VAT inavyopaswa kuchajiwa! Mambo mengine nafikiri ni ya kitaaluma zaidi kuliko siasa.

Ni vizuri TRA watoe ushauri wa kitaaluma kwa serikali kuhusiana na suala hili ili kuondoa mkanganyiko usio na tija.Bado nafikiri lengo la serikali kuanzisha kodi hii ni jema na kwa kweli litaiongezea serikali mapato.

Wananchi lazima tukubali kwamba kuna vipato vyetu vingi havikatwi kodi na ni jukumu la serikali kutambua vyanzo vyote vya mapato na kuvitoza kodi na kwa namna hii tu ndipo nchi itaondokana na utegemezi na kuweza kutoa huduma muhimu kwa wananchi wake
 
Tra tra.....sasa wao wapate wapi faida...mbona sarakasi. Kwani mabenki ni NGO
 
Sasa ndugu yangu unadai wewe ni mwanasheria halafu unaji contradict. VAT act iko very clear kwamba ni goods and services gani zina attract VAT..na zipi ni exempted. Bank transaction fees hazikuwa kwenye list ya services zinazo attract VAT...sasa ulitaka mabenki yakusanye VAT kwenye transaction fees kwa nguvu ya sheria ipi? Serikali iliona hilo na hata waziri alikiri kwamba kuna huo upungufu kwenye hotuba yake ya bajeti na ndio maana ikafanya marekebisho kwenye VAT act. Inamaana sasa VAT kwenye transaction fees ndio imekua introduced..and since its a consumption tax..it must be passed on to the consumer.

Mwanasheria uchwara. Anatia aibu.

Anasema mabenki yalikua yanakwepa kodi. Yatakwepaje kodi iliyokuwa exempted?

Hii nchi nimegundua ina tatizo kubwa sana la elimu. Kama "mwanasheria" anaongea hivyo mtu wa kawaida mtaani si hatari zaidi.
 
Tunaomba hii is we tetesi na isiishie kwenye mabenki tu ifike hadi kwenye mitandao ya simu

Mitandao ya simu ni wakwepaji wakubwa wa kodi kwa hiyo hiyo VAT ya 18% walipe wao kutoka kwenye hizi commission wanazokata kutoka kwenye miamala.
 
Safi,kumbe vyanzo vya kodi viko vingi sana,sasa serikali iwapunguzie mzigo wa kodi wafanyakazi.
 
Lakini pesa yenyewe iliyoongezeka ni sh 150 sioni kama itaongeza ugumu wowote wa maisha.

Mkuu hakuna pesa ndogo. Nenda benki kaweke milioni moja, ipungue sh. 150 uwaambie wakuwekee milioni moja kwa kuwa sh. 150 haina maana. Au nenda supermarket ununue kitu ikasoro sh. 150 uone kama watakupa.

Kwa utafiti wangu niliofanya, nimegundua kuwa matajiri wakubwa hawadharau pesa yo yote! Sisi walala hoi ndiyo tuna tabia ua kudharau pesa ndogo na matokeo yake tunabaki watu wa kawaida tu!
 
Knowledge has always been free from parties. The earlier interpretation was based on incremental tax concept but given TRAs explanation it is even more clear that previous banks' charges constitute the incremental tax base. The problem with fellow Tanzanians is lack of proactive thinking but to blame instead of inquisition.

Daaah...you are a typical Mdanganyika!!! But it is your choice to be mentally slaved...so just stop bluffing, it doesn't help you clear the wrong projection that you already confidently did....without a blink !!!! Empty excuses...very sad!!!!
 
Knowledge has always been free from parties. The earlier interpretation was based on incremental tax concept but given TRAs explanation it is even more clear that previous banks' charges constitute the incremental tax base. The problem with fellow Tanzanians is lack of proactive thinking but to blame instead of inquisition.

Tatizo la Watanzania wengine mlisoma kwa kukariri masomo na mmeendelea hivyo hata maishani. Sasa hizo bank charges ambazo zamani zilikuwa hazilipiwi VAT na sasa serikali imeamua zilipiwe VAT si zinalipwa na walaji/customers/consumers? Open up your thinking ability potential!

Interesting.....you do not even know your exact argument. Seemingly confused !! Brainwashed....!!!
 
Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha http://www.https://jamii.app/JFUserGuide/2016/07/ufafanuzi-wa-tra-kuhusu-ongezeko-la.html
 
Nadhani TRA wakisimamia huo udau walioleta juu ya makato yao itakuwa jambo la heri sana, hio kodi walimwe Benki ndani ya faida wanayoipata kupitia makato ya miamala na iwe kama sehemu ya gharama zao za uendeshaji, sio kuipiga teke kwa mteja mwenye account utakuwa uonevu sana jamani!
Ikiwa hivyo kama usemavyo, ggarama zitapanda tena ktk jina la upandaji wa gharama za uendeshaji na si VAT tena.
 
Back
Top Bottom