Serikali, tofautisheni HERBALISTS na MEDICAL DOCTORS

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,894
nimewaza sana, nimeona serikali inatakiwa kutunga sheria kabisa inayotenganisha watoa dawa za mitishamba na waganga waliosomea vyuo vikuu. fikiria:

1. Mtu analala usingizi anaota ndoto kuwa mti fulani ni dawa, anaamka anaweka kibanda kwamba babu yake kamuotesha ndoto na kumrithisha uganda, na yeye anaitwa MGANGA sawasawa tu na medical doctor wa muhimbili.

2. mtu anaibuka tu anakwamba babu yake au baba yake alimrithisha uganga, hajaenda hata shule, na yeye anajiita mganga.

3. mtu amefeli shule, kafika form four kapata zero, au kafika form six kapata zero, pengine hata masomo ya sayansi alikuwa hasomi. anaenda china anasoma certificate ya mitishamba kwa mwaka mmoja, anarudi hapa anajiita yeye ni doctor.

4. mtu hajui hata mwili wa mwanadamu ukoje, hajasoma hata vitabu, kiingereza hajui ambacho ndicho vitabu vingi anavijua, hajui side effects ya baadhi ya mimea kwenye mwili wa mwanadamu, lakini kwasababu ana imani yeye ni mganga ana weka kibao na yeye ni doctor, na anajifanya kutibi watu.

5. mtu anaibuka leo, anashika mti au tunda moja tu, anakwambia tunda hili linatibu magonjwa 100, hajawahi kufanya tafiti, hajawahi kuugua na kujifanyia experiment yeye mwenyewe, wamesaga malimao ya unga rundo, machunga, majani ya matunda na takataka kibao wanalisha watu rundo, anajiita yeye mganga.

6. mtu ameona duniani heshima ya mwanamke ni kuzaa mtoto, akatangaza kuwa anatibu watu wasiozaa, kwasababu wanawake ndio wahanga, wako tayari kufanya lolote, ili kufanikiwa anahonga wanawake kadhaa, anawapa hela ili awachukue picha awahoji waseme walikuja kwake kutibiwa wakapona kumbe hamna kitu, asilimia 90 % ya waliotibiwa kwake wameliwa malaki kadhaa na hawajapona, tuwafanye nini hawa?

7. mtu hajui hata kujibu swali la kitabibu, ukimwuliza hata sehemu fulani ya mwili wa mwanadamu haijui...anajiita mganga.

8. mtu amekuwa msomi wa kitabu cha dini (kuran kwa waislam, au kwa wakristo kuna hawa wasabato kama kina ndodi na mashahidi wa yehova kama yule chizi aliyekodi kipindi tbc juzi). anaibuka leo anasema anatibu kwa kutumia vitabu vya dini, na anajiita mganga. umesoma wapi wewe hadi uitwe mganga?

hivi hawa mbona wanatofautiana na wanatumia jina moja? kwanini serikali isitunge sheria na itofautishe kabisa haya majina kwasababu yanachanganya wananchi, kwanini serikali isiweke sheria kabisa kwamba hawa watu MARUFUKU KUJIITA WAGANGA/DOCTORS wajiite HERBALISTS AU TRADITIONAL HEALER. hii itasaidi mwananchi ajue kuwa huyu ninayeenda kwake leo ni doctor au mtu wa mitishamba tu asiyejua mwili wa mwanadamu, na ni sawa tu na mtu aamue kwenda kwa mganga wa kuaguaa anayetibu kwa imani au wanaoenda kwa medical doctors.

jambo ambalo mnatakiwa kujua ni kwamba, hawa traditional healers wengi, wanatibu kwa IMANI. mtu hajui hata mwili wa mwanadamu lakini anatibu kwa imani tu, spiritually, unatibu kiroho ndio maana wanakuwa wanawasiliana na mashetani, sijui wanaita mababu etc.
 
Serikali dhaifu sana hii! Haithamini maisha ya watu wake kabisa! Hadi afya za watz tena wapiga kura zimefanywa huria, kila mganga anatibu kama anavyojisikia! Na tatizo kubwa la watz ni ujinga uliokithiri na viongozi magoigoi wasiojua wanachosimamia! Kila kitu tz ni rubbish kabisa! Elimu, afya, mazingira, n.k!!

Naunga mkonyo hoja.......! Ulimi hauna mdomo........!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
hahaha, mtu anaamka asubuhi anasema amerithishwa, ameoteshwa ndoto, amesoma kitabu cha dini ..hahahaha. jamani jamani, nawaonea huruma watanzania. hili ni bom kubwa sana.ndio maana nchi zetu haziendelei, kwasababu hatuko serious kwenye mambo ya msingi. nenda ulaya wewe una certificate ujiite doctor utaona mziki wake.
 
ni kitu cha ajabu sana kwakweli. asubuhi nimeangalia kipindi cha morning trumpet cha azam two, walimwalika pia mganga, pamoja na msajili wa hao waganga, hakika yake hawa waganga wa kienyeji ni bomb kubwa sana, hawajui hata wanachotibu.wanatoa tu maungaunga ya madawa hata wasiyoyajua. hata ukimwuliza humo kwenye dawa kuna nini hajui, atakachokwambia tu ni kwamba mimi najua hiyo ni dawa, na inaponya basi.
 
Back
Top Bottom