Serikali toeni ushirikiano kwa wazee wajiajiri

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,037
9,952
Wakati wa kikao cha JPM na wafanyabiashara, wazee walilalamika kunyanyaswa na serikali. Lilikuwa Jambo la huzuni sana.

Kwenye kikao cha JPM na wachimba madini, napo wazee walilalamika kulaliwa na serikali hadi wengine kufilisika.

Juzi kwenye kikao cha JPM na madaktari limejirudia tena. Mzee aliyeanzisha chuo kwa lengo jema naye kanyanyaswa hadi kufunga chuo chake.

Kule Kibaha mzee Upendo Express anahangaika kupata vibali vya kufungua kiwanda cha kutengeneza mabasi, hamna support yeyote kutoka serikalini.

Lakini kwenye mahafali ya vyuo na shule, serikali haohao wanawahimiza vijana wajiajiri.

Sasa wenye mitaji ujuzi na uzoefu wanapigwa mizengwe wakati huohuo tunahimiza wasio na mitaji wala uzoefu wajiajiri. Hivi tuko makini kiasi gani?

Kwanini tusitoe support kwa hawa wazee wajiajiri waajiri na wengine na wawaachie vijana ofisi za umma.

Serikali haiwezi kuajiri watu wote na hakuna serikali ilishawahi kuajiri watu wote. Hawa wazee wana mitaji na ujuzi; wanahitaji kuungwa mkono tu, hawahitaji kuwezeshwa na mtu au kujiunga kwenye vikundi wakopeshwe fedha.

Na hela ya kula wanayo. Mkiwapuuza wao wataishi vizuri na familia zao ila nyie ndiyo mutahangaika na wakosa ajira.
 
Back
Top Bottom