beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika na katika kipindi kinachoishia Aprili 2019, Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Tsh. 2,300.9 ikilinganishwa na Tsh. 2,270.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2018.
Utulivu katika mwenendo wa thamani ya shilingi umetokana na utekelezaji wa sera ya fedha, usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi ya Serikali, matumizi ya gesi asilia badala ya mafuta na kuzalisha umeme.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.
“Sababu nyingine ni baadhi ya viwanda kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikuwa zikiagizwa kwa wingi kutoka nje ikiwemo vigae na marumaru,” amesema Dkt. Mpango.