Serikali tazameni upya huduma zitolewazo kupitia e-Government kwa taasisi nyingi za Umma

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
352
1,000
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye serikali mtandao kwa kuweka e-Services kwenye taasisi mbalimbali ila zipo changamoto zinazokwamisha malengo ya mradi huu;

1. Top management wa Idara za serikali hawajui maana ya serikali mtandao na awajawahi kufundishwa au kuelimishwa kuwaondoa kwenye mfumo wa zamani kwenda kwenye mfumo mpya.

2. Watendaji wa chini hawaelewi kabisa tafsi ya serikali mtandao. Mfumo unakuelekeza namna yakujaza ombi la huduma na nyaraka za kuattach lakini ukifika kwa afisa anakuelekeza vitu ambavyo havipo kwenye website na Wala havijaandikwa kwenye sheria yoyote. Anajiamulia tu kukurudisha bila kujali muda wala uharaka wa huduma unayotaka.

3. Huduma nyingi zilizokuwa zinatoka zikiambatana na ujumbe wa sms kwa mteja kwa Sasa hazitoki hivyo. Mfano ukiwa nje ukaomba visa hupati ujumbe wowote kwa email hivyo nivigumu kujua Kama ombi limepokelewa. Ukienda kwenye huduma Kama maji na masuala mengine ya huduma za kijamii upati uthibitisho au notification on time.

5. Wateja wengi wanalazimika kufanya huduma manually bila kujua wanafanya huduma mannually, nenda TRA, Uhamiaji, Polisi (lost report), hospitali nk uangalie muda unaotumia kupata huduma kulinganisha na muda wa zamani. Tulitegemea e- services iondoe mahusiano ya rushwa kwa kupunguza kukutana kwa mtoa huduma na mpewa huduma ila Sasa hivi ni Kama unalazimika lazima uwe karibu na ofisa wa serikali ndipo upewe huduma.

Kwa kuwa kitengo hiki kimepata wizara mpya naamini Jambo la Kwanza nikusimamia watumishi wa Umma wapate elimu kuhusu e- services na kuweka utaratibu wa notification kwa kila service hata Kama wananchi watalipia kuliko hii kukesha ofisi za umma ukijibizana na watendaji ambao wakati mwingine kwa kauli zao hata hii mifumo ya serikali awaiamini. Mtumishi anakujibu mbona wengine tukiwaelekeza wanafanya wewe ujuaji tu, mbona wengine wanaatach document zinakubali wewe unashindwaje? Kama ulikuwa na haraka si ungeanza mwaka uliopita?

We need to reform mindset za watumishi tupunguze muda na kurahisisha huduma.
 

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
706
1,000
Watu wetu kwenye mambo ya IT ni bure kabisa na lugha ya Kiingereza imekuwa ni changamoto kubwa sana kwao! Mfano mimi toka mwezi wa nne mwaka huu nina update taarifa BRELA ,kazi niliyokuwa nachukuwa siku moja sasa imekuwa ni mwaka mzima!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom