Serikali: Tayari tumetoa Tsh. Bilioni 15.49 kwa ajili ya CoronaVirus na tumesamehe kodi kwa baadhi ya vifaa vya kujikinga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Waziri wa Fedha, Philip Mpango amesema Serikali iliunda timu ya Kitaalamu inayochambua jambo hili kiumakini, na kipaumbele cha Serikali ni kukinga watohuduma za afya na Wananchi

Amesema kwa makadirio ya awali katika kipindi cha Machi hadi Septemba mwaka huu zinahitajika Tsh. Bilioni 382.5 kwa ajili ya kukabiliana na #COVID19 na hadi sasa Hazina imetoa Tsh. Bilioni 15.49 pamoja na nusu Bilioni zilizoenda Zanzibar

Ameeleza kuwa Serikali inaangaliza zaidi upatikanaji wa vifaa vya kujikinga (PPE), kuwakinga watoa huduma za afya, dawa, vifaa tiba, kuongeza vitanda, ventilators (mashine za kupumulia), magari ya wagonjwa na kuimarisha kambi za wagonjwa

Aidha, amesema wametoa ridhaa ya kusamehewa kodi kwa vifaa takriban 15 vinavyotumika kujikinga na #CoronaVirus kama alivyoomba Waziri wa Afya na vifaa hivi vitasamehewa ushuru wa forodha na VAT

Pia amesema "Tumefanya kazi ya kuchambua mafungu mbalimbali ambayo matumizi yake yanaweza kuahirishwa ili kuelekeza fedha hizo kwenye matumizi ya dharura"

Kukabiliana na Corona ni kipaumbele cha juu kabisa cha dharura cha awamu ya 5, hakuna serikali makini inayoweza kupuuza nguvukazi, watu wake fa ndi maana tunalipa umuhimu mkubwa jambo hili
 
Pamoja na haya yote lakini bado kuna viumbe vitalalamika tu.
malalamiko ndo kipaumbele kikubwa kwa wabongo wengi.
 
Wewe umeumia kwenye hayo mandege tu? Nenda pale Amana ukajionee mwenyewe watz wenzako wanavoteseka.
Hivi kama kitu hujui acha kupoteza muda. Lini hospitali za serikali zilikuwa safi na Vifaa? Au corona imekuja na Vifaa. Mabadiliko ni process
 
Rais asimamishe ujenzi wa ma fly over na miradi mingine tupigane na adui Coronavirus anayemaliza watu wetu.
Je watu wakiisha hiyo miradi ataifaidi Nani?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom