Serikali tatu na dhamira yetu kuelekea Shirikisho la Afrika ya Mashariki

GKM

JF-Expert Member
Dec 5, 2012
738
324
Wasalaam,

Tangu kutolewa kwa Rasimu mpya ya katiba yetu kumekuwa na mijadala mbalimbali kutokana na maudhui yaliyomo katika rasimu hiyo. Binafsi nimekuwa nikitafakari mustakabali wa nchi yetu endapo kama rasimu hiyo itapita bila kufanyiwa marekebisho yoyote.

>Je endapo tunataka kuwa na serikali tatu (kwa mfumo wa shirikisho), je tunaweza kusema kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuelekea katika mfumo wa shirikisho la afrika mashariki?
>Kama tuna dhamira ya kuwa na EAF, je, kwa nini nchi zetu mbili zisiingie ktk shirikisho hilo zikiwa na mamlaka na uwakilishi unaojitegemea?
>Je, ni kweli kwamba serikali tatu ni option bora kuliko serikali moja? Au ni kukosekana kwa kiongozi mwenye ushawishi na 'ubavu' wa kulisimamia hilo?
>Je, kuna haja ya kuendelea na mradi wa vitambulisho vya taifa? Kama ipo, ni taifa lipi hilo?

Kwa sasa ni hayo tuu.

Karibuni kwa kuchangia.
 
Kuna dhamira ya dhati kweli kuunda EAF?
 
Kama mambo ya nje ni jambo la Muungano, Taifa hilo ni Tanzania!
Kwa hiyo EAF haiwezekani kwa sababu ya serikali 3 za Tanzania?
Na kwa hiyo unapendekeza serikali moja ya Tanzania au serikali moja ya EAF??
Onesha kuwezekana kwa serikali moja ya EAF kabla hujazishangaa hizo 3 za Tanzania...
Mwisho, jiulize kwa nini serikali moja haijawezekana kwa miaka 51 ya Muungano kabla hujashangaa serikali 3 kwenye Rasimu.....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom