Serikali tatu kwa jicho la tatu

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,178
1,195
Wakati tume ya mabadiliko ya katiba ikiwa imewasilisha rasimu ya pili ya katiba, na kupendekeza muundo wa serikali tatu (Serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, Serikali ya jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya jamhuri ya Tanganyika), jicho la tatu linahitajika kuona ni kwa jinsi gani serikali hizi zinaweza kufanya kazi pasipo migongano.

Kwa muundo uliopo sasa wa serikali mbili, Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar anaruhusiwa kuunda wizara azitakazo (maji, nishati, miundombinu n.k) na kuteua mawaziri na manaibu waziri. Na ukiangalia kazi zinazofanywa na mawaziri wa serikali kuu (ukiacha waziri mkuu) zimejikita zaidi bara. Hoja ni kwamba kukiwa na serikali ya Tanganyika yenye rais wake na mawaziri wake, kazi za mawaziri wa serikali kuu (ya jamhuri ya muungano) zitakuwa ni nini.

Kuhusu swala la uwakilishi wa wananchi, sasa kuna bunge kwa serikali kuu na baraza la wawakilishi kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Gharama za uendeshaji wake hazionekani kama ni mzigo sana kwani baraza la wawakilishi lina wajumbe wachache. Sasa kukiwa na lile la Tanganyika lenye wajumbe zaidi ya 200 (majimbo ya bara), gharama za uendeshaji zitakuwaje.

Rais wa nchi husika (mfano sasa yule wa serikali ya Zanzibar) ndiye mwenye watu (watu wanamuona kama ndiye aliye karibu nao zaidi). Sasa tukiwa na yule wa Tanganyika ataekuwa na ushawishi kwa watu wa bara, rais wa serikali kuu anakuwa na watu gani.

Tukija kwenye swala la uwakilishi kwa uwiano wa ki-nchi washiriki (yani Tanganyika na Zanzibar), kuwa mwenye dhamana akitoka bara basi naibu/makamu atoke zanzibar na kinyume chake, je inaleta mantiki ukichukulia tofauti kubwa ya idadi ya idadi ya watu kati ya nchi hizi mbili (zaidi ya milioni 35 kwa bara na pungufu ya milioni 5 kwa Zanzibar) na ukubwa wa maeneo ya nchi hizi mbili.

Nadhani hili swala linahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu zaidi ya kuliorodhesha kwenye katiba mpya
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
4,170
2,000
Usiogope kwa kuwa bado Katiba ya Tanganyika haijaandikwa! Nadhani italeta ufumbuzi wa mashaka yako! Ingelikuwa tayari imeandikwa tungelijadili! Kinachohitaji mjadala sasa ni Katiba ya Tanganyika!
 
Foum Jnr

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
272
170
hakuna haja ya wananchi kupigia kura rais wa muungano kwa mfumo huu, nafasi ya uraos wa muungano iwe ni heshima tu isio na maamuzi bali bunge la muungano ndio lenye nguvu. Rais wa muungano na wazanzibar wapishane kama rais na makamo wake kwa kupokezana kwa terms. mambo yenyewe ya muungano yakiwa matano, tunahitaji rais mwenye maamuzi ya nini? na kwa hili tutaondosha uwepo wa rais watatu na makamo na wengine, baraza la mawaziri wa muungano dogo lenye uwakilishi kwa kila pande kwa yaliomo ndani ya muungano likiongozwa na bunge la muungano..
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,841
2,000
Mleta uzi aduwilly anataka kutuaminisha kuwa Ma waziri wa Serikali ya muungano hawajui Job description zao hata wale ambao wizara zao zina cover mambo ya Muungano na ndo maana wamejikita zaidi Tanganyika.
Hii unaweza kuwa pia ni due to Jeuri ya Wa Zanzibar kutoitambua Serikali ya Muungano.
Tukiwa na Serikali tatu...Mawaziri wa Muungano watapewa majukumu yao ya kufanya.
Kama unataka kusema kuwa Ma waziri wa Muungano hawana cha kufanya then kimsingi unamaana kuwa hakuna haja ya Muungano...
 
Last edited by a moderator:

Kocho

Senior Member
Jun 5, 2013
120
0
miccm kichwa ngumu kweli huu mungano haulipi tena kutokana na wakati husika kam ni udugu hauwezi vunjika msiogope lichama lenu kufa mbona ni kawaida tu au mnaogopa kutiwa jela kwa maovu yenu c mlitenda nanyi mtatendewa ukitenda uovu utalipwa uovu hapa duniani akhera hisabu mc mlazimishe ngombe kunywa maji huu mungano umechuja waulizeni wananchi wanautaka hyo ndo salama vinginevo mnatengeneza bomu la ujirani kua uhasama
 
Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,142
2,000
Tusijenge HOJA YA WINGI WA WATU, SOMENI MAGNER CARTER YA 1964
Wakati tume ya mabadiliko ya katiba ikiwa imewasilisha rasimu ya pili ya katiba, na kupendekeza muundo wa serikali tatu (Serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania, Serikali ya jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya jamhuri ya Tanganyika), jicho la tatu linahitajika kuona ni kwa jinsi gani serikali hizi zinaweza kufanya kazi pasipo migongano.

Kwa muundo uliopo sasa wa serikali mbili, Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar anaruhusiwa kuunda wizara azitakazo (maji, nishati, miundombinu n.k) na kuteua mawaziri na manaibu waziri. Na ukiangalia kazi zinazofanywa na mawaziri wa serikali kuu (ukiacha waziri mkuu) zimejikita zaidi bara. Hoja ni kwamba kukiwa na serikali ya Tanganyika yenye rais wake na mawaziri wake, kazi za mawaziri wa serikali kuu (ya jamhuri ya muungano) zitakuwa ni nini.

Kuhusu swala la uwakilishi wa wananchi, sasa kuna bunge kwa serikali kuu na baraza la wawakilishi kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Gharama za uendeshaji wake hazionekani kama ni mzigo sana kwani baraza la wawakilishi lina wajumbe wachache. Sasa kukiwa na lile la Tanganyika lenye wajumbe zaidi ya 200 (majimbo ya bara), gharama za uendeshaji zitakuwaje.

Rais wa nchi husika (mfano sasa yule wa serikali ya Zanzibar) ndiye mwenye watu (watu wanamuona kama ndiye aliye karibu nao zaidi). Sasa tukiwa na yule wa Tanganyika ataekuwa na ushawishi kwa watu wa bara, rais wa serikali kuu anakuwa na watu gani.

Tukija kwenye swala la uwakilishi kwa uwiano wa ki-nchi washiriki (yani Tanganyika na Zanzibar), kuwa mwenye dhamana akitoka bara basi naibu/makamu atoke zanzibar na kinyume chake, je inaleta mantiki ukichukulia tofauti kubwa ya idadi ya idadi ya watu kati ya nchi hizi mbili (zaidi ya milioni 35 kwa bara na pungufu ya milioni 5 kwa Zanzibar) na ukubwa wa maeneo ya nchi hizi mbili.

Nadhani hili swala linahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu zaidi ya kuliorodhesha kwenye katiba mpya
 
Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,142
2,000
LAZIMA AWEPO AMIRI JESHI na ndivyo ilivyo is a bit ceremonial
hakuna haja ya wananchi kupigia kura rais wa muungano kwa mfumo huu, nafasi ya uraos wa muungano iwe ni heshima tu isio na maamuzi bali bunge la muungano ndio lenye nguvu. Rais wa muungano na wazanzibar wapishane kama rais na makamo wake kwa kupokezana kwa terms. mambo yenyewe ya muungano yakiwa matano, tunahitaji rais mwenye maamuzi ya nini? na kwa hili tutaondosha uwepo wa rais watatu na makamo na wengine, baraza la mawaziri wa muungano dogo lenye uwakilishi kwa kila pande kwa yaliomo ndani ya muungano likiongozwa na bunge la muungano..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom