Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!

Kwani kuna mtu hajui kuwa tunajenga reli? Wafanyabiashara wanakamuliwa, wafanyakazi na wakulima nao ni budi wakamuliwe.

Ni rahisi kupunguza kuliko kuongeza. Habari ya mshahara kuongezwa, sahau, sahau, sahau kabisa. Unachotakiwa ni kupiga kazi tu, haya mambo ya mishahara, achana nayo.

Katika kipindi hiki tunajenga Taifa, inabidi watu wapewe tu hela ya chakula na bima ya afya, basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Technically umekubaliana na mimi kwamba, ili kupunguza madhara ya inflation kwenye purchasing power lazima mshahara upande..

Sijui kwanini umempinga mwenzako?
Tatizo haukunielewa, Mimi nimekwambia kuwa umeangalia swala la mfumuko wa bei kwa context moja, Nakuelewesha tena sasa. Mfumuko wa bei unaweza kutazamwa kwa sababu au matokeo
Mfumuko wa bei kwa mtazamo wa sababu huwa kama ifuatavyo;

Mfumuko wa bei huelezeka kama kupanda kwa jumla kwa kiwango cha bei. Kwa maneno mengine, bei za bidhaa na huduma nyingine kama vile nyumba, mavazi, chakula, usafirishaji, na mafuta lazima ziwe zinaongezeka ili mfumuko wa bei utokee katika uchumi. Ikiwa bei za aina chache za bidhaa au huduma zinaongezeka, hatuwezi kusema ni mfumuko wa bei.

Zipi ni sababu kuu zinazopelekea kutokea mfumuko wa bei kwenye context hii? Wataalamu wa uchumi wanatoa sababu mbili ambazo hutofautisha kati ya aina mbili za mfumko wa bei: Demand-Pull na Cost-Push. Aina zote mbili za mfumuko wa bei husababisha kuongezeka kwa kiwango cha jumla cha bei ndani ya uchumi.

  1. Kwa upande wa Demand-Pull, Mfumuko wa Demand-Pull hutokea wakati mahitaji ya jumla ya bidhaa na huduma katika uchumi yanaongezeka haraka zaidi kuliko uwezo wa uzalishaji wa uchumi. Sababu moja inayoweza pelekea mfumuko huu ni benki kuu inapoamua kuongeza kwa haraka pesa kwenye mzunguko na kusababisha pesa kuwa nyingi kuliko bidhaa za kununua hivyo kusababisha viwango vya zamani vya mishahara visiweze kukimu bei mpya hivyo mishahara kupanda pia kunaweza kuwa ni njia kupunguza makali ya mfumuko wa Demand-Pull. Kwa namna moja au nyingine kuongezeka kwa mishahara pia kunaweza pia kuleta mfumuko wa bei ikiwa kutakuwa hakuna ongezeko la uzarishaji wa bidhaa, hii hutokea kwa kuwa watu huwa na kibuli cha manunuzi yani “Purchasing power” wakati hakuna bidhaa nyingi za kununua hivyo itabidi market forces ziingie kwenye Darwnism, yani survival the fittest ama mwenye pesa nyingi ndio atakae nunua bidhaa na mwishowe hutokea bei mpya iliyo sukumwa na kibuli cha manunuzi.
  2. Mfumuko wa Cost-Push, hutokea wakati bei za malighafi zinazo tumika kwenye mchakato wa uzalishaji zinaongezeka hivyo kufasababisha bei za bidhaa kupanda. Bidhaa zinapo kuwa na bei mpya maana yake mishahara ya dhamani haiwezi kumudu mahitaji mapya ya kimanunuzi sokoni. Kuongezeka kwa mishahara ya wafanyakazi waliopo kwenye mnyororo wa uzalishaji au kuongezeka kwa bei za malighafi na usafirishaji zinaweza kuwa ni sababu za aina hii ya mfumuko wa bei. Kupanda kwa bei ya bidhaa zinazotoka nje husababisha pia aina hii ya mfumuko wa bei.
Haijarishi mfumuko umeletwa na nini ila madhara yake yanatakiwa kupungzwa kwa serikali kusimamia na kuweka viwango vya mishahara kwa wafanyakazi na bei elekezi kwenye bidhaa muhimu.
Au benki kuu kutumia contractionary monetary policy ili kupambana na mfumko wa bei kwa kupunguza usambazaji wa pesa ndani ya uchumi na kupunguza bei za dhamana na hati fungani au kuongeza viwango vya riba.

Kwa mtazamo wa mtoa mada hapo juu inaweza pia akawa hana maana hizi za mfumuko unaotokana na sababu ama anahisi kuwa madhara ya mfumuko iliopo tunaweza kuyakabili kwa kuongeza mishahara, na hapa ndipo ambapo tunapokuja na Mfumuko wa bei kwa mtazamo wa Matokeo yake.

Mfuko wa bei kwa mtazamo wa matokeo, hapa mfumuko wa bei huelezeka kama kupungua kwa nguvu ya manunuzi ya sarafu fulani kulingana na muda. Makadirio ya kiwango ambacho nguvu ya manunuzi kwa sarafu hupungua kunaweza kuonyeshwa katika kuongezeka kwa wastani wa bei za bidhaa na huduma fulani zilizochaguliwa katika uchumi kwa kipindi fulani cha muda. Aina hii ya mfumuko inaenda sawa kabisa na price index kwa Walaji, wauzaji wa jumla na wazarishaji ambapo kutokana na sababu nyingi tofauti zikiwemo market forces, Price index huwa inapanda na marachache sana hupunguaga. Mfumuko tunapouangalia kwa mtazamo huu unakuwa na madhara ambayo tunaweza kuyapunguza kwa muda mfupi au kwa muda mrefu.
  1. Kwa muda mfupi tunaweza kupunguza madhara kwa kuongeza viwango vya mishahara ya wafanyakazi kwenye sekta zote, ambapo huwa kuna madhara yake pia ikiwemo kudorola kwa uchumi na kukosekana kwa ajira.
  2. Kwa muda mrefu serikali kupitia benki kuu inaweza kutumia contactionary monetary policy ili kupunguza uwepo wa sarafu za nchi kwenye uchumi na soko la kimataifa. Hapa huwa kuna madhara ya muda mfupi ambapo watu watashindwa kumudu bei za vitu lakini baada ya muda bei zitashuka ili ziweze kuwafuata watumiaji, ama wazarishaji wanaweza kuboresha ufanisi kwenye mnyorolo wa uzalishaji ili waweze kuendana na hali za kifedha za watumiaji
  3. Pia ili kucounter check market forces za demand na supply, Serikali inapaswa kuchukuwa hatua za ziada zitakazo endana na Contactionary monetary policy ya benki kwa kuweka bei elekezi, . Njia hii ni sahihi kwa kuwa mfumuko wa bei maranyingi hutokana na Uranguzi wa wafanyabiashara kwa kupandisha bei ya vitu iwapo hakuna gharama za uzalishaji zilizo ongezeka. kwenye masoko ya nchi za kibeberu mtu anaweza kupandisha bei ya bidhaa kwakuwa tu kuna watumiaji wengi wanaihitaji kuliko uwezo wake wa kuzalisha. Serikali ikiweka sheria kali na adhabu kuwataka wafanya biashara wafuate bei elekezi itawafanya hawa wafanyabiasha wenye vitendo vya kiovu vya kiranguzi kuwekeza kwenye kutanua Scale za plant zao iliwaweze kukimu mahitaji ya soko. Ambapao faida yake huwa ni ongezeko la ajira mpya wakati wafanyabiashara wanatanua scale za uzalishaji
Sina nia ya kumuunga mkono mtoa mada wala kukuunga mkono wewe ila najaribu kuonesha kuwa nyie wote wawili mnautazama mfumuko wa bie kwa upande mmoja. Hakuna nchi isiyokuwa na Tatizo la mfumuko wa bei ila huwa tunaamua kuliongeza kwa kufuata njia za muda mfupi ilikupunduza makari yake na matokeo yake ni mfumuko unaokuwa kila siku.
My take ni kuwa tusidharau kupandisha mishahara ya watumishi ila pia tupandishe kwa kuangalia inaweza kuwa na madhara gani kwenye uchumi, pia serikali itumie vizuri nafasi yake kudhibiti uranguzi, hii nchi ni ya kijamaa hivyo mfanyabiashara hawezi kujipangia bei ili ajipatia fedha nyingi kwa kuwarangua wanyonge. Kupanda kwa bei kunapaswa kuwa kuwe cost-driven na sio demand-driven.
Hata hivyo serikali pia inapaswa kuangalia sera zake za kodi, maana hizi kodi ndio sababu za kupanda kwa bei, Ukimzidishia kodi mfanya biashara na hujampa bei elekezi ujue umemzidishia bei mwananchi kwa kuwa mfanyabiashara nayeye atapandisha bei.
 
Fanyeni kazi mtaongezwa mishahara mpaka lini, mkishaongezwa mnabadilisha maisha mtataka magari mazuri mkapange masaki na Oysterbay. mkija upande wa pili nyie ndo washika kofia acheni kulia kulia fanyeni kazi
 
Mimi nikimuona mtumishi wa chini anaomba/ kupokea rushwa sitashangaa,maana hao ndio wahanga wakubwa ,posho hawana,motisha hawana,wanategemea mshahara tu wenye thamani ya miaka 10 iliyopita, wakati mahitaji mbali mbali yakiwa yamepanda mara dufu,
Hali ikiendelea hivi hata familia zao zitasambaratika,
Mlioshiba jaribuni kuwakumbuka wenye njaa
 
Hujawahi kumsikia mkuu wa kaya? Alisema kuwa kupanga ni kuchagua.

Yeye amechagua miundombinu kwanza. Mishahara baadaye, 2030, kwa watakaokuwa bado hai.
 
Hii awamu ni historia! Watumishi wataikumbuka kwa mateso na adha waliopata.

Hakuna cha flai ova wala treni umeme zitakazo kumbukwa,zaidi ya umaskini wa kupindukia,kuporomoka kwa uwekezaji na mitaji.
Wafanyakazi ombeni Serekali idhibiti Mfumuko wa bei kwanza, mengine yatajiseti yenyewe!!
 
Wafanyakazi ombeni Serekali idhibiti Mfumuko wa bei kwanza, mengine yatajiseti yenyewe!!
Huna unaloweza,miaka yote hiyo unadhibiti kitu gani!
Alafu unang'ang'ania goli,ngoja deportivo ikuwahishe wengine waendeleze.
 
Endelea kutafakari utapata majibu nini cha kufanya, lakini Kuongezewa mishahara kwa huduma inayotolewa bure ni ngumu hapa duniani because workers they don't provide any profit in terms of money.
Usikute na wewe ni Mshauri eti wa huyo mzee wako! Kweli Nchi imepatwa. Kama mawazo na mtazamo wako ndiyo huu!!! Ni jambo lisilo shangaa kumuona mzee wako akigeuka kituko kila siku kutokana na matamko yake! Kumbe amezungukwa na watu wenye upeo mdogo sanawa kufikiri.

Eti Walimu hawastahili kwa sababu hawaingizi chochote! Kwani hizo ada walizo kuwa wanawatoza wazazi kabla ya 2015 walizisitisha hao walimu, au yule mjuaji wako na chama chake, kwa lengo tu la kujitafutia umaarufu wa kisiasa?

By the way, mbona kuna walimu wanao fundisha Kidato cha Tano na Sita na ambako bado ada inaendelea kutozwa? Unasemaje juu ya hilo? Nao hawaingizi hela? Vipi kuhusu walimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu!!

Jitahidi basi kupunguza ujuaji usio na faida yoyote ile.
 
Hii awamu ni historia! Watumishi wataikumbuka kwa mateso na adha waliopata.

Hakuna cha flai ova wala treni umeme zitakazo kumbukwa,zaidi ya umaskini wa kupindukia,kuporomoka kwa uwekezaji na mitaji.
Mitano tena
 
Pitia uzi vizuri, hivi vitu viwili ni tofauti kabisa. Non related.. na nimetoa majibu kuhusu comment yako

Eti kwasababu watu hawana kazi ndo wengine wasiongezwe mshahara?
Najua n vtu Viwili tofauti... Ila ata ww mwenyew yatafakar km ww una uhakika wa mshahara kla mwez unalalamika je yule ambae ata chek number haijui mwaka wa 6 huu afanyeje. Yaan mtu ambae hana kaz atataman apate hcho chako kidogo maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom