Serikali simamieni msimamo huo huo mlioamua huko mpakani Kenya

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,258
1,541
Nashukuru mungu kuona serikali yangu kuamua kukata mzizi wa fitna baina yetu na majirani zetu juu ya Madereva wetu wa Tanzania.

Nimeona serikali umeamua kwenda mpaka mpakani mwa Kenya na Tanzania na kubaini baadhi ya madudu katika upimaji wa Corona.

Haiwezekani mtu anae shughulika na kupima Corona. Anapima mtu Zaidi ya mmoja kwa mkono ule ule bila kunawa kwa mikono. Wakati wataalam wa afya wanasema mtu hutakiwi kujishika usoni bila kunawa mikono lakini muuguzi wa afya ambae una muhudumia mtu hunawi mikono huu ni uzembe na ujinga Kama watakua hawafanyi makusudi

Pia wazo la serikali yetu la kutaka madereva wetu wapimwe Tanzania then wapewe sertificate waende nayo Kenya ilo wazo pia ni nzuri japo sidhani Kama watalikubali. Ila nafikiri big point ilitakiwa kila mtu anae agizo mzigo kutoka Tanzania aje apokelee mpakan watanzania wasiingie Kenya Wala wakenya wasiingie Tanzania kila mtu afie kwake

Je kwa njia hii tufanyeje?

Inatakiwa baada ya mzigo kutoka Tanzania kuwasili mpakan linakuja gar lingine kutoka Kenya na Madereva wote kutoka pande mbili wawe wanpimwa kila mmoja anakuja kwenye makutano na sertificate yake hapo wanaongezwa kila pande vijana wawili wa kusaidia na wao wanpimwa waje na sertificate zao bila ivyo Tanzania tutaendelea kuwa kichaka Cha baadh ya viongozi wa nchi jiran kujifichia kwenye takwim za Corona Mana kila siku tutaendelea kutangazwa watanzania

Serekal haya maneno yanayo vumishwa kwenye mitandao ya kwamba Tanzania ndio tunasambaza Corona si mazuri Tena serekal ichunguze huenda Kuna mchezo mchafu

Kama Zambia anawaaminisha watu eneo kubwa lililo athirika ni Kijiji Cha mpakan Tena anasema sababu kubwa ni watanzania. Tena kwa msisitizo anafunga mpaka wake hapo moja kwa moja tutaonekana sis ni popo tumebeba virus
Serekal ni vizury kua Makin

Angalia video ya jins watanzania wanavyo pimwa Corona mpakan

 
Wewe mzungu mzalendo mbona kiswanglish chako kigumu, andika kwa kiswahili ueleweke, au gari yako imezuiwa? Hatukutetei ng'o.
 
Kipindi hiki sijui majirani walilima chakula cha kutosha!

Nipo hapa nasubiri
 
Kwa maoni yangu Mkuu wa Wilaya hana uwezo wa kuwasiliana na nchi jirani. Anachoongea hapo ni porini na kuwafurahisha madereva wa malori waliochoka .

Hii ngoma ni uwanja wa Prof Kabudi sio kwenda kuchukua majani ya corona Madagascar
 
Back
Top Bottom