Serikali: Shule za msingi zina utitiri wa Mitihani isiyo na ubora. Wengine hufanyishwa Mitihani kila wiki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
SERIKALI imekiri kuwapo kwa utitiri wa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa shule za msingi za umma na binafsi na imesema mitihani mingi haina ubora kwa maendeleo ya kitaaluma ya watoto.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alisema hayo jana na kubainisha kuwa wizara inaangalia uwezekano kuisitisha mitihani hiyo kwa kuwa ni mingi bila sababu za msingi.

“Katika baadhi ya shule, wanafunzi wanawekewa kambi za kila wiki na kufanyishwa mitihani hata wiku za mwisho wa wiki,” alisema Dk Akwilapo wakati wa mkutano wa mwaka unaofanyika kwa siku mbili ulioandaliwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC).

Tume imeelezea wasiwasi kwamba kumekuwa na mitihani mingi ya kujitathimini isiyo na ubora. Dk Akwilapo alisema wizara inajua kuwapo kwa mitihani hiyo na kwa sasa inawashirikisha wataalam ndani na nje ya wizara hiyo ili waangalia kuangalia namna ya kuisitisha au kuboresha vipindi.

Alisema kwa mtazamo wake ni kwamba kuboreshwa kwa ufaulu wa masomo kati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni matokeo ya ubora wa ufundishaji na usimamizi wa elimu.

Aidha, Dk Akwilapo ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama njia za kufundishia wanafunzi wa shule za awali na msingi.

“Ninaihakikishia Tume kuwa wizara iko tayari kufanya kazi na tume ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kati ya wanafunzi nchini,” alisema Katibu Mkuu.

Tume inasimamia karibu taasisi 1,223 za mafunzo ya elimu inayojumuisha shule za awali 404, shule za msingi 268, shule za sekondari 373, shule za seminari 50, vyuo vikuu tisa vya ualimu, vituo 96 vya mafunzo ya ufundi, na taasisi 22 za elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume, Peter Maduki alisema shule chini ya Kanisa Katoliki imechukuwa mfumo wa mitihani ya majaribio inayopangwa kwa kusaidiwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Maduki alisema mitihani imepangwa katika kila kanda ikihusisha shule za msingi na sekondari.

“Kwa bahati mbaya, kumeibuka mlipuko wa mitihani ya majaribio katika kata na wilaya ambazo ubora wake unatia shaka,” alisema.

Maduki aliishauri serikali kupitia tena mitihani hiyo na kupunguza vipindi ili kutoa nafasi kwa mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujifunza.

Akizungumzia mkutano huo, Maduki alisema umeandaliwa kama mkakati wa kuwakutanisha wataalamu kutoka wizara za Elimu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizopewa jukumu la kusimamia sekta ya elimu.

Tume inatumai mkutano huo utatoa fursa ya kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kujadili njia bora za kutumia ICT katika ufundishaji na ujifunzaji.
 
Sijui tatizo ni nini?

Kuna wengi ambayo Hawaijui elimu ila wanapenda kuisemea Elimu.

Q& A is the most and popular teaching and learning quadrant.

Sasa mwanafunzi kasema miaka 6 huko ukiulizwa alichosoma hata every week shida nini?

Kwanza Std VII ilifaa kuwa Review Classroom sema ndio hivyo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mitihani acheni wafanye tu hakuna namna la sivyo wataambulia kucheza midako, rede na mipira siku za jumamosi au kushinda mitaani kujifunza kainama, kaokota kainika za Diamond.

Muda wa kushinda na waototo hatuna pesa zimebana kila kona caheniwashinde madarasani hasa hawa wa Day maana wenzao wa bweni wanalindwa
 
Sijui tatizo ni nini?
Kuna wengi ambayo Hawaijui elimu ila wanapenda kuisemea Elimu...
Tatizo linakuja pale wazazi wanawajibika kulipia kila mtihani wa majaribio unaofanyika, uwe wa kata, wilaya, hata wa darasa! na mwanafunzi ambaye hatoi malipo hayo, haruhusiwi kufanya, na badala yake huambulia viboko!

Mitihani hiyo imekuwa kichaka cha walimu kujiongezea vipato kinyemela, kwani habari kutoka katika baadhi ya shule zinasema aghlabu wanafunzi wenyewe ndio wanaosahihisha mitihani hiyo, kwa mtindo wa kubadilishana karatasi.
 
HII Mitihani ya kila j, mosi
shule za msingi na sekondary ni miradi ya walimu
Mwafunzi wa shule ya msingi mtihani 1 ni 500

Mwanafunzi wa secondary mtihani 1 1000

Darasa 1 lina wanafunzi 300× 500= 150,000
huo ni mtihani 1
Wanafunzi wanafanya mitihani 2 kila wiki sawa na shs 300,000
Ukitoa gharama za uchapishaji
Mitihani yenyewe ni cope & paste
Mwalimu anabakia na mkwanja wa maaana,,
Anawapoza wazee wa kamati ya wazazi pamoja na mwalimu mkuu wa shule kihaina
Mshahara kwake ni ziada tu na anakwenda kuuchukua siku atakayopenda kwenda kuuchukua bila hata presha yeyote
Mkwanja anao wa mitihani fake
 
Tatizo la public school ndio hili.

Sasa hivi mwalimu anaweza kuandika maswali 45 au 30 ubaoni kila wiki, kusahihisha madarasa yote na achana na notice na nyomi zile tulizofyatua huko majumbani kwetu.

Nadhani swala ni nyie wazazi kwenda shuleni kupiga gharama ya 'heavy duty photocopy machine' (12 Milion) jichangeni inunueni ya shule pesa kidogo sana iyo. Ili walimu wakiwa na majaribio yao na mazoezi wabakie na kazi ya kuprint tu.

Pia kumbukeni walimu hiyo ndio kazi yao sasa mnadhani walimu wakale wapi? Kama mnaona wanafaidi nendeni mkasome vyuo vya ualimu muwe walimu.

Huku private mnalipa mamilioni tena mnanyanyaswa vizuri na vitoto vyenu hamsemi kitu.
Shule za jumuiya bhana (public schools) zile ndio shule maana wazazi hawajui maana ya elimu na watoto wao halikadharika

Sasa mwalimu analo jukumu la kufundisha mwanafunzi na mzazi/mlezi wake. Wenye akili na wanaojitambua kidogo watoto wao wako huko private (St. kunani). Napendekeza serikali iongeze mara dufu mshahara ya walimu wa shule za Umma

Nawasilisha!!!!
 
Tatizo linakuja pale wazazi wanawajibika kulipia kila mtihani wa majaribio unaofanyika, uwe wa kata, wilaya, hata wa darasa! na mwanafunzi ambaye hatoi malipo hayo, haruhusiwi kufanya, na badala yake huambulia viboko!..
kama Shule ya msingi lugalo,wanafunzi wa darasa la saba mitihani kila ijumaa, na ni lazima kila mwanafunzi aende na elfu mbili ya mtihani, inafikia wakati mtoto asipokuwa na iyo ela wanamchapa ,yaan wapo bize kuwapa mitihan ili wapate ela kuliko kuwapa taaluma au kuwafundisha,, mtoto wa wifi yangu anasoma pale kila siku wanalalamika juu ya ilo, darasa la saba wapo wanafunzi #125, yaan kwaiyo efu mbili ukipiga hesabu ni ela nyingi,
 
HII Mitihani ya kila j, mosi
shule za msingi na sekondary ni miradi ya walimu
Mwafunzi wa shule ya msingi mtihani 1 ni 500

Mwanafunzi wa secondary mtihani 1 1000

Darasa 1 lina wanafunzi 300× 500= 150,000
huo ni mtihani 1
Wanafunzi wanafanya mitihani 2 kila wiki sawa na shs 300,000
Ukitoa gharama za uchapishaji
Mitihani yenyewe ni cope & paste
Mwalimu anabakia na mkwanja wa maaana,,
Anawapoza wazee wa kamati ya wazazi pamoja na mwalimu mkuu wa shule kihaina
Mshahara kwake ni ziada tu na anakwenda kuuchukua siku atakayopenda kwenda kuuchukua bila hata presha yeyote
Mkwanja anao wa mitihani fake
Wewe kweli Kanda Matope, hivi ulishawaona walimu wanalipwa OVERTIME, OR PERDIEM? wache bhana walimu wangu na wao wapate hata nauli na hela ya kulipia kodi, nasikitika sana kuona mtu yeyote akimyanyasa mwalimu, masikini ya mungu hawajuagi kuongea, wao kila kitu sawa, naumia ila bai tu waache wamenisaidia hapa nilipo. Ukitaka na wewe nenda kasomee ualimu upate hako unakokaita kamkwanja.
 
HII Mitihani ya kila j, mosi
shule za msingi na sekondary ni miradi ya walimu
Mwafunzi wa shule ya msingi mtihani 1 ni 500

Mwanafunzi wa secondary mtihani 1 1000

Darasa 1 lina wanafunzi 300× 500= 150,000
huo ni mtihani 1
Wanafunzi wanafanya mitihani 2 kila wiki sawa na shs 300,000
Ukitoa gharama za uchapishaji
Mitihani yenyewe ni cope & paste
Mwalimu anabakia na mkwanja wa maaana,,
Anawapoza wazee wa kamati ya wazazi pamoja na mwalimu mkuu wa shule kihaina
Mshahara kwake ni ziada tu na anakwenda kuuchukua siku atakayopenda kwenda kuuchukua bila hata presha yeyote
Mkwanja anao wa mitihani fake
Wewe ni bonge la muongo! Acha umbea... koma!!
 
Acha hizo, mtumikia hekaluni hula vya hekaluni.

Back to the topic. Mitihani hiyo no mizuri Sana. Mfano Hayati Mwl. Manoni aliyewahi kuwa Mwl. Mkuu wa shule za msingi Madenge,Mgulani ,na kurasini Dsm alikuwa anatumia hiyo approach na alikuwa anafaulisha Sana wanafunzi.
HII Mitihani ya kila j, mosi
shule za msingi na sekondary ni miradi ya walimu
Mwafunzi wa shule ya msingi mtihani 1 ni 500

Mwanafunzi wa secondary mtihani 1 1000

Darasa 1 lina wanafunzi 300× 500= 150,000
huo ni mtihani 1
Wanafunzi wanafanya mitihani 2 kila wiki sawa na shs 300,000
Ukitoa gharama za uchapishaji
Mitihani yenyewe ni cope & paste
Mwalimu anabakia na mkwanja wa maaana,,
Anawapoza wazee wa kamati ya wazazi pamoja na mwalimu mkuu wa shule kihaina
Mshahara kwake ni ziada tu na anakwenda kuuchukua siku atakayopenda kwenda kuuchukua bila hata presha yeyote
Mkwanja anao wa mitihani fake
 
kama Shule ya msingi lugalo,wanafunzi wa darasa la saba mitihani kila ijumaa, na ni lazima kila mwanafunzi aende na elfu mbili ya mtihani, inafikia wakati mtoto asipokuwa na iyo ela wanamchapa ,yaan wapo bize kuwapa mitihan ili wapate ela kuliko kuwapa taaluma au kuwafundisha,, mtoto wa wifi yangu anasoma pale kila siku wanalalamika juu ya ilo, darasa la saba wapo wanafunzi #125, yaan kwaiyo efu mbili ukipiga hesabu ni ela nyingi,
Acha wivu bwana,2000 kitu gani kwa week.

Mitihani ni Jambo la muhimu. Shule za msingi Kama Mgulani, kurasini na shule alizopitia Hayati MJ Manoni alikuwa anafaulisha Sana wanafunzi kutokana na hiyo mbinu.
 
SERIKALI imekiri kuwapo kwa utitiri wa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa shule za msingi za umma na binafsi na imesema mitihani mingi haina ubora kwa maendeleo ya kitaaluma ya watoto.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alisema hayo jana na kubainisha kuwa wizara inaangalia uwezekano kuisitisha mitihani hiyo kwa kuwa ni mingi bila sababu za msingi.

“Katika baadhi ya shule, wanafunzi wanawekewa kambi za kila wiki na kufanyishwa mitihani hata wiku za mwisho wa wiki,” alisema Dk Akwilapo wakati wa mkutano wa mwaka unaofanyika kwa siku mbili ulioandaliwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC).

Tume imeelezea wasiwasi kwamba kumekuwa na mitihani mingi ya kujitathimini isiyo na ubora. Dk Akwilapo alisema wizara inajua kuwapo kwa mitihani hiyo na kwa sasa inawashirikisha wataalam ndani na nje ya wizara hiyo ili waangalia kuangalia namna ya kuisitisha au kuboresha vipindi.

Alisema kwa mtazamo wake ni kwamba kuboreshwa kwa ufaulu wa masomo kati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni matokeo ya ubora wa ufundishaji na usimamizi wa elimu.

Aidha, Dk Akwilapo ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama njia za kufundishia wanafunzi wa shule za awali na msingi.

“Ninaihakikishia Tume kuwa wizara iko tayari kufanya kazi na tume ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kati ya wanafunzi nchini,” alisema Katibu Mkuu.

Tume inasimamia karibu taasisi 1,223 za mafunzo ya elimu inayojumuisha shule za awali 404, shule za msingi 268, shule za sekondari 373, shule za seminari 50, vyuo vikuu tisa vya ualimu, vituo 96 vya mafunzo ya ufundi, na taasisi 22 za elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume, Peter Maduki alisema shule chini ya Kanisa Katoliki imechukuwa mfumo wa mitihani ya majaribio inayopangwa kwa kusaidiwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Maduki alisema mitihani imepangwa katika kila kanda ikihusisha shule za msingi na sekondari.

“Kwa bahati mbaya, kumeibuka mlipuko wa mitihani ya majaribio katika kata na wilaya ambazo ubora wake unatia shaka,” alisema.

Maduki aliishauri serikali kupitia tena mitihani hiyo na kupunguza vipindi ili kutoa nafasi kwa mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujifunza.

Akizungumzia mkutano huo, Maduki alisema umeandaliwa kama mkakati wa kuwakutanisha wataalamu kutoka wizara za Elimu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizopewa jukumu la kusimamia sekta ya elimu.

Tume inatumai mkutano huo utatoa fursa ya kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kujadili njia bora za kutumia ICT katika ufundishaji na ujifunzaji.

Alafu hana cheo cha DK .yani hata aibu hana .kuandaa mwanafunzi na mitahani ni kumeweka sawa hata siku ya mwisho kufanya si kigeni kwake.
 
kabla ya kutoa maamuzi mngejaribu kutafakari kwanza lengo la hiyo mitihani nini. Msije mkaitoa mitihani mkasababisha bomu jingine.
Mtihani ni sawa na mechi ya mchezo wa mpira. Huwezi kumfunga mpinzani wako kama hufanyi mazoezi ya kucheza na timu mbalimbali michezo ya kirafiki. Na ndio maana hata timu yetu ya taifa stars inapokua na mechi huwa inaanza kujipima kwanza kwa kucheza na timu mbalimbali michezo ya kirafiki. Na kwa hao wanafunzi ni hivyo hivyo wanapofanya mitihani mbalimbali ya majaribio ndivyo wanajiweka vizuri zaidi kukabiliana na mitihani yao ya mwisho. Hivi hili swala msilichukulie kwa uharaka bali mkae chini kishamfanye evaluation ya kutosha ili mjiridhishe impact za hiyo mitihani kwenye ufaulu wa mwanafunzi ndipo mfanye maamuzi. Fanyeni utafiti tena wa kisayansi data zote mnazo kusanyenyi shule zote zinazofanyisha mitihani mingi wanafunzi wake kisha mlinganishe na ufauru wa hizo shule kila mwaka. Baada ya hapo tengenezeni model ya mlichokipata. Msiishie hapo tu kisha kusanyeni na shule zinazofanyisha mitihani michache kisha linganisheni ufauru wake kwa kila mwaka. Kisha tengenezeni model. Chukueni model ya shule zinazofanyisha mitihani mingi linganisheni na model ya shule zinazofanyisha mitihani michache kisha manyeni maamuzi kutokana hitimisho la utafiti mliofanya.
 
kila mchungaji atakula madhabahuni mwake, waacheni kidogo na walimu wapate viji senti hata vya mafuta ya taa, mishahara yao yenyewe ya mawazo halafu kidogo wananchopata mnataka pia muwabanie duh. Pia elimu yetu ya kibongo ndivyo ilivyo hata kipindi nasoma tulikua tunapiga ppr hadi kero sema necta inakuja maswali yaleyale, na finally tunafaulu
 
Lissu aliwaambia mfumo wetu wa elimu toka Primary hadi vyuo Vikuu ni wa kukaririshwa...sasa mmeanza kuelewa taratibu uzito wa hoja yake eee!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom