Serikali: Shule binafsi, marufuku kukaririsha darasa au kufukuza Mwanafunzi kwa kutofikia wastani wa shule

Tamko hili ni sahihi tuliunge mkono, elimu yetu inahitaji mabadiliko chanya ili tuenze kwenda mbele sambamba na dunia ya leo. Elimu yetu ni bado no ileile aloiacha mkoloni ambayo wao huko kwao waliisha achana nayo. Hii inaitwa Victorian education system, ilianzishwa na malkia Victoria, yenyewe Ina karirisha, inajenga matabaka (mwenye akili na mjinga), Ina nidhamu ya uoga, inatumia sana adhabu Kama nyenzo ya kufundishia, wale wanaofaulu Ina wapa kiburi na dharau, inaigawa jamii Kati ya wasomi wanaotaka kuabudiwa na wasiosoma wanaodharauliwa, elimu hii badala ya kuwa nyenzo ya kuiendeleza jamii inageuka kuwa kisu Cha kuikata jamii vipande vipande, walioianzisha walisha achana nayo, elimu yao Sasa ni inclusive wanasema 'no child shall be left behind' Sasa elimu ni haki ya kimsingi ya kila mtoto, watoto wote lazima wafike form 4
 
Naona wanaanza kutapatapa...mkitoka hapo mtasema shule binafsi ada isizid 60,000/= sababu akili zenu mnazijua wenyewe....
Hivi huko wizarani huwa wanaajiriwa watu wa akili hivi kabla ya kutoa tangazo kama hili huwa hawajadiliani kabisa...
 
Kwa upande mwingine mi naona Shule za binafsi wanajali quality. Shule za serikali wanajali quantity.Wanafunzi kwenye Shule za serikali wamelundikwa Kwa hiyo uwiano kati ya idadi ya wanafunzi na ubora wa huduma haupo .Shule zetu za private hawahitaji ku-deal na wanafunzi wengi ambao hawataweza kuwahudumia vizuri so inawabidi wa-base kwenye mchujo kitaaluma ,Na ukiangalia mitihani ya kitaifa idadi ya watahiniwa Shule binafsi ni 10 au 15 wakati zile za serikali ni 50 Na kuendelea .Ni rahisi kihudumia wachache kuliko kuhudumia wengi.Maoni yangu ,wastani wa serikali uko chini sana waupandishe kidogo! Kwa sekondari wanaoshindwa waende garage na kwingineko (I mean VETA inawahusu) ukiwachuja mtihani wa mwisho unakuwa na namba ya wahitimu wa form four Kwa jina lakini si kwa uhalisi.MTU anamaliza form four hata barua ya kimombo (ki-English) hawezi kuanduka hata maarifa ya msingi (ya kuvukia barabara just kidding!)hana haya kamaliza ili iweje. Serikali pandisheni wastani kidogo!!
 
Haya yote yanasababishwa na Serikali kutotimiza wajibu wake ipasavyo kulikopelekea shule za Serikali kushuka Kitaaluma hivyo kutoa nafasi kwa Shule za Binafsi kushika Soko matokeo yake ndo haya hujui ushike kipi uache kipi!

Wametuwekea shule za kata ili tuwe wapumbavu Daima.

Acha Trump atutukane Watawala wa Afrika wanashida nyingi
 
Hahaha kasahau kuwakumbusha HESALB sasa mikopo ni kwa kila mtoto HAKUNA madaraja. Na TCU ifutwe, MITIHANI iondolewe level zote watoto wote waende university of Dar as Salaam na MUHAS bila kujali ufahulu wao ili kila mtoto apate elimu sawa na anayoipenda. "No child left behind". Tanzania raha kweli kweli, elimu bila mitihani, kila mtoto afaulu level zote hiyo ndiyo elimu sawa kwa wote.
 
Hizo shule zipo kuvutia biashara zao kwa kufanya sifa ya kufaulisha wanafunzi wote kumbe njama watumiazo ni kubagua watoto wenye vipaji
Ni bora wangweka matangozo ya kutaka watoto wenyepaji pekee kuliko hizo njia watumiazo
kama una mtoto aliyepitia private hautakuja kutamka hayo unayotamka hata siku moja. ukweli siku zote upo wazi.
 
Mimi naona wameamua bora liende tu uwe hujui kusoma au kuandika ww twende tu hakuna wastani wa kukuzuia kuendelea hahahaaaa ..sisi tulio soma shule za wastani tunajua umuhim maana km ww dish linayumba unapigwa chini ili ufanye bidii ya kusoma sio bora liende
 
yan darasa wote wafaulu eti mwanao peke yake afeli utasema walim hawajafanya kaz yao?? nonsense kabsa
kuna wengne ni vichwa maji mwache arudie akichoka ataamua kua seriuz
Wastani wa serikali ndio unaozungumziwa. Ni 21 i think kwa form 2. Sasa mtoto labda ana avg ya 48 hajafikisha ya kwao ya 50 ndio amefeli? Nonsense na wewe pia.

Sent from my PHANTOM5 using JamiiForums mobile app
 
KWAHIYO KAMA MTOTO HANA NIDHAMU ASIREKEBISHWE KWA SABABU SERIKALI IMESEMA. KAMA UNAONA UGUMU/GHARAMA KWA MTOTO WAKO KURUDISHWA NYUMA ZIPO SHULE ZA SERIKALI TENA ZA BURE PELEKA HUKO. WEWE NI MMOJA WA WAZAZI WASIOJUA UMUHIMU WA ELIMU. NA KAMA HUNA MTOTO NI MMOJA WA WALE WA NDIO MZEE KWA KILA KITU
Uelewa huu duni uliupata wapi? Akirudia darasa anapata nidhamu? Mijitu kama wewe munafanya serikali iandike barua kama hizi. Angalia hata unavyoandika, jamani!
 
Back
Top Bottom