Serikali: Shule binafsi, marufuku kukaririsha darasa au kufukuza Mwanafunzi kwa kutofikia wastani wa shule

It makes sense! Ila kuna wengine, naturally, ndivyo walivyo. Hakuna namna unaweza kuwabadili.
Mkuu ukishakubali kumfundisha mtoto, tuna uhakika utaweza kumpa uelewa anaohitaji, maana ni taaluma yako. Mtoto mwenye matatizo ya maumbile ana shule zake zenye uwezo wa kumfundisha. Ukijifanya unaweza halafu uishie kumfukuza lazima serikali ife na wewe.

TZ sasa hivi ina mijitu haikupata elimu inayostahili, ikapata mtaji, sasa inamiliki shule na kujiita 'Managers'. Mtu kama huyo ana manage nini? Pesa! akiona pesa imepungua, anakaririsha wanafunzi ili walipe tena. Anaiba mitihani ili avute wateja na mingine inaishia hata kwa waganga kwa imani za kishenzi tu!
 
ELIMU: Serikali imezuia shule binafsi kumrudisha darasa, kufukuza mwanafunzi aliyefaulu mtihani darasa la 4, kidato cha 2 kwa kutofikia ufaulu wa shule husika.

Waraka wa Elimu Namba 7 wa Mwaka 2004 umepiga marufuku utaratibu wa shule zisizo za serikali kukaririsha Darasa, kufukuza au kuhamisha mwanafunzi aliyefaulu Mtihani wa Darasa la Nne, Kidato cha pili kwa kigezo cha wanafunzi hao kutofikia wastani wa ufaulu wa shule husika.

7e708db798fb5bf329c064e94cdd07e2.jpg
03b3099e858883e5301ecbaa6839a036.jpg
Kilio changu cha muda mrefu, Kumrudisha mtoto nyuma au kumfukuza ni kumnyima haki yake ya msingi ya elimu. Elimu ya msingi ni kuweka msingi tu sio kuwapata wanataaluma kama ilivyo kwenye vyuo vyuoni. Kumrudisha mwanafunzi nyuma au kumfukuza shule ni shule husika kushindwa kuwajibika. Kama mwanafunzi ana makosa ya msingi sheria zingine zitumike kumfukuza lakini sio hili la kushindwa kufikia maksi za shule
Kumrudisha mtoto nyuma au kumfukuza ni kumuongezea miaka mingi ya kufikia malengo yake
Hayo yalikuwa yakifanyika kwa faida ya kibiashara tu na wala haikuwa na tija kwa wanafunzi

Mbona Newton alikuwa hafanyi vizuri madarasa ya chini lakini alipofika madarasa ya juu katika hiyo hoyo elimu ya msingi alifanya wonders kwenye masomo yake na baadaye kuja kuwa mwanasayansi maarufu na muhimu duniani?

Hongera sana serikali, Hongera sana Wizara ya Elimu
 
Naunga mkono tamko asilimia 200. Hatuwezi kuwa na viwango private kwenye elimu. Kama vepe basi wasifanye hata hiyo mitihani ya taifa. Narudia kusema ni hatari sana elimu kuwa biashara.
 
System ya kutofukuza mtu aliyefeli jamani mwenzenu siielewi,naomba mnielewe.Namuelewa anayefukuza mtu aliyefeli na infact hamfuluzi,anajiondoa mwenyewe kwa kufeli.Nisiyemuelewa ni mtu anaye endelea kumlea mtu aliyefeli,amalize shule ili iweje?Nadhani aim ni excellency,sio kumaliza madarasa.
Mtu akiuliza kisomi, tunamjibu kisomi. Wewe umeuliza vizuri achana na mbumbumbu wa JF wengine wanaandika waliyoyaona shuleni kwao na wanadhani ndo dunia ilivyo. Ubongo wa sisimizi uko JF.

Kwanza fahamu kwamba elimu kitaifa siyo biashara. No single country ktk dunia hii inayofanya elimu iwe ni biashara. Kama ni huduma basi lazima iwe na viwango vya kitaifa. Kama kuna makosa ya viwango, umoja wa wamiliki wa shule ni sehemu ya wadau wanaostahili kujadili jambo hilo na si vinginevyo.

Tatizo wenye shule wameiona ni biashara, lakini hawataki kutimiza vigezo vya biashara. Wanajidai ni huduma lakini nyuma yake wafaidike na biashara, Nonsense! Kwa kuifanya ni biashara bubu, sasa wanatumia mbinu za hovyo!! Wanapokaririsha wanafunzi lengo lao siyo elimu bora, ni biashara. Wanavutia wateja kwa ushindi. Wengine ndo hao tuliowasikia Shinyanga, wanatia viboko wanafunzi kama ngamia. Wegine wizi wa mitihani ili itajwe ni ya kwanza kitaifa au ya pili, n.k.

Bahati mbaya kuna wazazi mbumbumbu wamesomesha shule hizo, waliosoma huko nao sasa ni sehemu ya mbumbumbu na wanaamini kufukuza wanafunzi kiliwajenga. Rubbish! Je, unajua kwamba kuna nchi Ulaya sasa hivi hawana mitihani ktk hatua hizo za elimu? Angalia mfumo wa Norway.
 
Hem kidogo labda sijaelewa vyema apa...
Ni marufuku kwa shule binafsi tu ila kwa zile za serikali kama kawa kama dawa au...?
Shule za serikali hazina ujinga huo. Mitihani inayofanya mtoto kurudia in ya la NNE na form two baas. Na iwe hivyo Kwa wote. Na kuna kitu waziri kasahau. Iwe marufuku kuwa na interviews za kuhamia. Because they save the same purpose.
 
yan darasa wote wafaulu eti mwanao peke yake afeli utasema walim hawajafanya kaz yao?? nonsense kabsa
kuna wengne ni vichwa maji mwache arudie akichoka ataamua kua seriuz
Takataka! Hata unavyoandika huonyeshi kama una elimu. Hili ndo tatizo, hata asiye na elimu naye anajadili elimu.
 
Aende shule za serikali basi, kwanini anang"ang'ania wanakokaririsha?
Unaamini serikali ina uzembe kama huo wa kwako? Mbona magari yanapangiwa mwendo barabarani, umejiuliza ni kwa nini? Umewahi kukataa kwamba hili ni la binafsi? Ingekuwa enzi ya watemi katili, ungezikwa ukiwa hai ili usiambukize familia ujinga.
 
Mimi hii kitu inanichanganya sana.Nashindwa kuelewa maana ya mitihani.Sasa kama ambaye hajiwezi anaruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kufeli mtihani husika, nini sasa mantiki ya mitihani?Si ingefutwa tu.Hii sio kupoteza fedha na wakati?Sasa naanza kuelewa huu ufaulu wa siku hizi wa mashaka.Nionavyo mimi,I stand to be corrected if I am wrong,system yetu ya elimu inajenga wahitimu wa madarasa,sio excellency.Very sad indeed.To me shule binafsi ziko sahihi kabisa,shule za serikali ziige mfano wao.
Wastani WA serikali kwa mwanafunzi kuendelea na masomo ya kidato Cha tatu kutoka form two ni afaulu masomo mawili kwa grade D au somo Moja kwa gradeC au zamani ilikuwa ni wastani WA 30 kwa masomo yote Shule nyingi za watu binafsi wanakuja na wastani wao mfano Kuna baadhi ya Shule zinaendeshwa wastani WA asilimia 60 hadi 65 huu ni uonevu kwa wanafunzi Shule hizi zinapenda kufundisha wanafunzi wenye uwezo mkubwa tu wale WA Hali ya chini kiakili hawatakiwi
 
Wastani WA serikali kwa mwanafunzi kuendelea na masomo ya kidato Cha tatu kutoka form two ni afaulu masomo mawili kwa grade D au somo Moja kwa gradeC au zamani ilikuwa ni wastani WA 30 kwa masomo yote Shule nyingi za watu binafsi wanakuja na wastani wao mfano Kuna baadhi ya Shule zinaendeshwa wastani WA asilimia 60 hadi 65 huu ni uonevu kwa wanafunzi Shule hizi zinapenda kufundisha wanafunzi wenye uwezo mkubwa tu wale WA Hali ya chini kiakili hawatakiwi
Siwatetei watu wa shule binafsi.Lakini on the other side, viwango vya shule zetu za serikali ni too low.What happened mpaka tukashusha viwango to 30% kwa mfano and now we say tumepandisha kiwango to D mbili na sijui C moja,huku quality ya mitihani na marking ikiwa too questionable.Mimi sina shaka yeyote kwamba upo mkakati wa makusudi wa kufaulisha wanafunzi.Nimeongea na Waalimu na wanafunzi wengi na wamenihakikishia kwamba this is true.Sasa tunamdanganya nani?Mkuu we are simply not serious with our education.Hivi mkuu huoni kwamba kuna shida,siku hizi siajabu kumuona kijana wa Form I akiwa hajui kusoma na hata siajabu pia kumuona kijana akiwa amemaliza Chuo Kikuu akiwa anababaisha babaisha kuongea Kiingereza na hata hajui kuandika barua ya kuombea kazi.Jamani what extra evidence do we need to prove that our education is mediocre. Hakuna sababu ya malumbano,elimu yetu ina matatizo makubwa na kama tutaendelea kujifanya iko sawa,we are heading for disaster.
 
Back
Top Bottom