Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,806
- 11,968
Ongezeko la vitendo vya ukatili wa jinsia na rushwa ya ngono kwenye vyuo vikuu inatajwa kuathiri tasnia ya elimu Nchini na matokeo yake ni kupatikana kwa wahitimu wasio na uwezo kutokana na baadhi yao kupata shahada zao pasi na kuzitolea jasho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju amesema hayo.
Kutoka na ongezeko la matukio ya aina hiyo katika Vyuo Vikuu limefanya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuzindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma, ndipo katika uzinduzi huo Mpanju akaeleza athari za vitendo hivyo.
“Matukio kama hayo yanasababisha kuzalisha wataalam ambao hawana vigezo, natoa wito kwa madawati kama haya kufanya kazi kwa usiri,” - Mpanju.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa James Mdoe amesema yakiwemo manyanyaso ya kijinsia au mengine akili haiwezi kufanya kazi, hivyo sio rahisi kwa wanafunzi kufikia ndoto zao.